Akili gani hii mtu ananunua costa milion 100 kwa ajili ya kupewa laki 1 kwa siku

Akili gani hii mtu ananunua costa milion 100 kwa ajili ya kupewa laki 1 kwa siku

Wacha nitoe niliyokutana nayo kiuhalisia kabisa ana kwa ana mbivu na mbichi kutoka jikoni.

1. Taasisi niliyokuwa natumika, kulikuwa na mbaba anabiashara ya malori ya kubeba mizigo kwenda mikoani. Muda wa kuanzia saa nne asubuhi, muda wa lanchi mchana na kuanzia saa kumi muda wa kurudi nyumbani... huyo baba alikuwa anaongea na simu za madereva na mafundi yaani alikuwa mkali kwenye simu hadi unahisi nikipita karibu yake atanisweka kibao au mbata. Utamsikia, nakwambia wewe na huyo utingo wako ntawaweka ndani na kabla sijawaweka ndani nawakata mapanga kwanza halafu linafuata tusi.

Wafanyakazi wenzie tulimzoea hasa kinamama, tukawa tunaambizana, biashara hizi za kufanya upande presa waachie wanaume wenyewe misiwezi, mali yako halafu kupata hela/malipo hadi ugombe/uwe mkali.


2. Huyu dada aka mshangazi, alizaliwa pekeyake na alilelewa na mama yake tuu hakuwahi kumjua baba yake wala ndugu upande wa baba. Mama yake alipofariki alimuachia nyumba hapo Sinza, akaja kuipiga bei ili apate mtaji afanye biashara......!!!🙄🙄🙄
Alianza kuuza mkaa anaagiza mkoani aulete Dar auze kwa jumla, akatapeliwa kaletewa magunia 10 yote chenga na unga wa mkaa... sehemu ya mtaji ukalala hapo. Akashauriwa anunue daladala DCM ya ruti ya Mbagala Kawe hiyo hela ya mauzo ya wiki anatoboa maisha. Kaingia wanguwangu sijui aliuziwa milioni ngapi ile daladala ila ilikuwa used na inafanya ruti hiyohiyo Mbagala Kawe, aliletewa hesabu ya wiki moja tuu ambayo nayo alilipia matengenezo ambayo hayakuisha baada ya hapo gari ikawa juu ya mawe haitengenezeki.
Pesa iliyobakia akajenga huko ukanda wa Tegeta nyumba haikuisha iko kwenye lenta haina milango wala madirisha akahamia...
Maisha yanatisha acha tuu.


3. Miaka 4 kabla sijastaafu nilimfata baba mmoja hapo kazini nikamwambia nataka nianzishe biashara ya uber ninunue ist moja used nitafute dereva niwe naingiza hela ya thupu. Akaniambia dada yangu Kasinde, biashara ya magari ni kichaa, sikushauri dada yangu hiyo biashara inataka ujitoe ufahamu kwelikweli. Kwanini usifungue duka la vyakula au madawa. Nikaachana na habari ya kununua it for uber, saa hii uongo maisha alhamulilah 🙏, can't complain.
Stori yako ni ya uongo tupu
 
Unaidharau laki moja huku unatafuta kiwanja tena cha hatua kumi na ...mbwa wewe...
Ungekua na pesa ungetafuta likiwanja skweamita hata elfu mbwa wewe ujenge bangaloo fala wewe umetoka kwenye bajaji ulipoitukana hio biashara vijana waliojiajir nayo sabbab unanskia uchungu kuwaona wenzio wanajishuhulisha wewe umekalia mapumbu kwa shemej hapo unasubir akultee chakula mbwa wewe, umehamia kwa wenye kosta, wao wana kosta, wewe una nini zaid yamapumbu christopher paul.
Mkuu mbona unhasira na Mimi sijakusababishia huo umasikini wako lakini pambana tu na Hali yako ndio maisha hayo🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Binadamu tuna akiri ya ajabu sana, na hiyo hela una kuta haijatokana na Costa. Sasa badala kuimarisha biashara iliyo mpa hiyo 100m, mtu anaenda kununua au kuingia kwenye biashara nyingine
Hahaha ni kituko🤣🤣🤣
 
Hii ni biashara nyingine kichaa yaani unawekeza milion 100 Kwa ajili ya laki 1 Kwa siku na hiyo pesa unalipata kkwa mbinde na siku nyingine utaletewa mpaka elfu 50 aisee huyu mtu anaakili timamu kweli yaani mwaka unaisha hata nusu ya Bei alionunulia kicosta chake haijarudi yaani hapo bado hata ajali haijapata ambapo inaweza kupata mzinga ukaambulia skrepa aisee mtu mweusi anasafari ndefu Sana ya utajiri duniani
Wewe umewekeza kiasi gani kwa biashara ipi? Usikute wewe hata basikeli mbovu huna alafu unamwita mtu anaenunua coaster eti "kichaa"
 
Kwan Bima kazi yake ni nn? Hv niweke 60/70m na najua chombo kinapiga kazi daily alafu nisikikatie bima? Kwanza iyo mizinga ipo kwenye vyombo vya moto tu? Huo mzinga wa mafremu ya kariakoo umeusahau? Kuungua? Fremu kuvunjwa (wizi). Kaa ukijua hamna baishara isiyokuwa na risk na ukichaa.
Hahaha kumbe inaizidi milion 100 akili Gani hii na bima umekata unalipia Kila mara inamaana uwekezaji umezidi milion 100 Ili upewe laki 1 aisee mtu mweusi akili hana🤣🤣🤣🤣
 
Hii ni biashara nyingine kichaa yaani unawekeza milion 100 Kwa ajili ya laki 1 Kwa siku na hiyo pesa unalipata kkwa mbinde na siku nyingine utaletewa mpaka elfu 50.

Aisee huyu mtu anaakili timamu kweli yaani mwaka unaisha hata nusu ya Bei alionunulia kicosta chake haijarudi yaani hapo bado hata ajali haijapata ambapo inaweza kupata mzinga ukaambulia skrepa aisee mtu mweusi anasafari ndefu Sana ya utajiri duniani.
Milioni 100 unachukua costa mbili na gari nyingine ndogo.
Bottom kine kila mtu ana investiment yake
 
Back
Top Bottom