Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Ikiwa ni mwezi wa tatu wa vita kati ya wapalestina na Israel bado vita vikali vinapiganwa katika ya jiji la Gaza na makombora kurushwa na kudondoka Tel Avivi la karibuni likiwa lile la jana.
Hali hiyo imelazimisha viwanja vyote vya Israel kutokuwa salama kwa safari za anga kupelekea wafanyakazi zaidi ya 600 kupewa likizo za lazima bila malipo.
Upande wa kaskazini ya nchi hiyo nako vita vimewahamisha maelfu ya wayahudi kwenda kuishi kwenye mahoteli kama kambi za wakimbizi.Hiyo ni kutokana na Hizbollah kupiga maeneo hayo pamoja na mifumo ya ulinzi wa anga ya Iron dome.
Kwa kusini ya Israel wanajeshi wa Houth ndani ya Yemen wamekuwa wakizilenga meli zote zenye mafungamano na Israel au zinazoelekea nchini huko katika juhudi zao za kuwatetea wapalestina.Meli hata zisizokuwa na mafungamano na Israel na hazielekei huko lakini zimekosa imani na eneo hilo la bahari nyekundu.Mashirika karibu yote makubwa yanayotumia mfereji wa Sueza yameamua kutumia njia ndefu ya kuzunguka Afrika Kusini ili kujilinda na makombora na droni za Houth.
Katika hali hiyo ya vita nchi kama Malawi na Kenya zina mpango wa kupeleka vibarua nchini Israel kujaza mapengo ya vibarua kama hao kutoka Thailanda waliokimbia sehemu zao za kazi ambazo ziko karibu na Gaza.
Inashangaza malengo ya nchi hizi ni yapi kuhusiana na kupeleka raia wao maeneo hayo ya vita.
Jee nia ni kusaidia Israel ambayo uchumi wake umepata pigo, ni tamaa ya kipato kwa raia wake maskini au ni kupuuza malalamiko na nia za wapalestina kutetea maeneo yao hayo wanayokusudia kupeleka raia zao?.
pindi watakapopata madhara ya vita nani atalaumiwa ?