Nafikiri kuna jambo hujalielewa bado. Hawa watu wanaconnections huko Mtwara ambazo zinawasaidia kutekeleza mashambulizi yao na inaonekana wapo mda tu wakizurura wakisubiri wenye silaha zao waje waanze kazi. Ukarimu wetu wa watanzania kukaribisha kila mtu na kumuachia huru bila kumfatilia ndio umetufikisha hapa. Waliofanya mashambulizi kama wameondoka nchini hio ni advantage kubwa, kwa sababu lengo ni kuzuia wao ku advance forward. Sasa Jeshi letu litaanza kushuhulika na hizo connections zao at the same time wanasubiriwia wavuke tena.
Sasa kama unajua Msumbiji jeshi lao linamaliza hasira kwa wananchi tena vipi tushirikiano nao? mimi nasema Msumbiji imejitakia hili kutokea, inaonekana wanapuuzia hili swala labda kwa vile linatokea vijijini na wamekalia kulinda miji tu. Uzembe huu wa Msumbiji JWTZ inatakiwa iingie ndani ya msumbiji kumaliza hii ishu, hakuna haja ya kuwangoja wavuke tena, ni kuwafuata tu mana msumbiji hawana mashirikiano.