Kwani uimara wa ccm unatokana na nguvu ya ushawishi kisiasa, au ni muundo wa katiba unaompa rais nguvu kuliko katiba? Na mara zote mwenyekiti wa ccm huwa ndio rais ambaye anaweza kuviagiza vyombo vya dola kufanya atakacho, na vyombo vya dola hutii chochote hata kama ni kinyume cha sheria na katiba. Kwa mazingira yalivyo bila machafuko au nguvu kutoka nje, inakuwa ngumu kuitoa ccm madarakani kwa kura. Huu uimara wa ccm ni kama ule wa KANU ya kenya iliyokuwa madarakani, baada ya kutolewa madarakani ilipotea ghafla.