LOTH HEMA
JF-Expert Member
- Dec 6, 2015
- 18,611
- 27,615
Niseme ukweli tu, kuna wakati niliteuliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya harusi, nilimuuliza mwenye harusi unataka kufanya harusi ya bajeti kiasi gani? Alijibu nataka kufanya harusi simple tu ya bajeti ya laki nane, wajumbe walimuuliza we una kiasi gani? Alijibu ana laki moja. Mwisho wa michango zilipatikana laki tatu pamoja na yake. Nilipangia bajeti hizohizo zilizopatikana, wali maharage bila nyama wala soda, maji ya kisima ikatoka hiyo. Ifike muda viongozi wa dini wawaache huru waumini kufunga ndoa kimtindo kulingana na bajeti zao, kuoa hata bila kufanya sherehe, inatosha kusainishwa cheti cha ndoa, jioni wanandoa watajua wale nini wenyewe