AKILI ZA MTU MWEUSI: Kuchangishana sherehe (kadi za mwaliko na magroup )

Niseme ukweli tu, kuna wakati niliteuliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya harusi, nilimuuliza mwenye harusi unataka kufanya harusi ya bajeti kiasi gani? Alijibu nataka kufanya harusi simple tu ya bajeti ya laki nane, wajumbe walimuuliza we una kiasi gani? Alijibu ana laki moja. Mwisho wa michango zilipatikana laki tatu pamoja na yake. Nilipangia bajeti hizohizo zilizopatikana, wali maharage bila nyama wala soda, maji ya kisima ikatoka hiyo. Ifike muda viongozi wa dini wawaache huru waumini kufunga ndoa kimtindo kulingana na bajeti zao, kuoa hata bila kufanya sherehe, inatosha kusainishwa cheti cha ndoa, jioni wanandoa watajua wale nini wenyewe
 
Ukitaka kuoa inabidi 100% uwe na mpunga wako ,kama bajeti ni 10m basi inabidi uwe na 10m kwa mfuko ,kama mtu anatataka kukuchangia iwe option na si lazima.
kabisa. Zamani muoji ndiye alijigharamia kulisha wahudhuriaji wa harusi yake bila kujali watahudhuria wangapi, upuuzi fulani ukaingia wa kuchangia, imeenda hivyo mpaka ikafikia kwenye madaraja ya kutoa kulingana na uwezo wako. Ni ufahari na anasa tu zimetawala harusi hizi zisizo na maadili ya kindoa na hazidumu ni show off tu huku watu wamekamuliwa vya kutosha japo ni hiari kutoa. Harusi zenyewe ni za kichoyo, wanaingia waliotoa mchango tu. Tena umezuka uvaaji wa wahudhuriaji wa kihuni na ukahaba ukumbini huku harusi ikifanyika usiku wa manane. Mambo ni mengi ya kukera kuhusiana na harusi hizi za kuchangia.
 
Hapo kwa viongozi wa dini hawahusiki na hii kadhia. Ndoa mfano ya kikatoliki gharama unayotakiwa kulipa kanisani hazidi elfu 50. Hapo ikijumuisha hela ya mafundisho ya ndoa na cheti. Sijajua madhehebu mengine kama kuna gharama yoyote.

Kwa waislamu najua ndio almost zero cost
 
Makanisa mengine inategemea na maono ya mchungaji wa mahali hapo. Wengine huchangisha mchango mdogo wa fedha kununua mchele, maharage, nyama, soda, matunda, maji na viungo bila kujali mwenye harusi kajiandaaje kwa bajeti yake na harusi huliwa hapohapo kanisani au ukumbini kutegemea na kamati imechangaje michango. Washirika humbeba muumini mwenzao kumfanyia harusi bila mchango mzito. Unakuta mchango ni mdogo elfu moja, mbili, haizidi elfu tano, mtu anakabidhiwa mke wakaanze maisha ya ndoa
 
Sure..umesema ukweli ila sasa mfumo ndo umetushape hivo mkuu.. hivi nimeungwa kwenye magrupu manne ya michango ya harusi na wato jamaa zangu.. wao ni employees ila mimi jobless..natafuta namba nileft.!
 
Nakazia, Huo Upumguani Ukome.
 
hivi ๐˜‚๐—น๐—ฎ๐˜†๐—ฎ ๐—ธ๐˜„๐—ฒ๐˜๐˜‚ ๐—ธ๐˜‚๐—ป๐—ฎ ๐˜‚๐—ท๐—ถ๐—ป๐—ด๐—ฎ ๐—ต๐˜‚๐˜‚ ๐—ฎ๐˜‚ ๐˜‚๐—น๐—ถ๐˜€๐—ต๐—ฎ๐˜„๐—ฎ๐—ต๐—ถ ๐—ธ๐˜‚๐—ผ๐—ป๐—ฎ ๐—ธ๐˜„๐—ฎ ๐—บ๐—ฎ๐˜๐—ฎ๐—ท๐—ถ๐—ฟ๐—ถ
 
Huna pesa wewe maskini ndio maana unalalamikia tumichango twa 20,000 hadi 50,000. ๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†
 
Unamkuta mtu mweusi anaangalia series yupo season ya 37 episode ya 108
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ