Wogombea wengi wa urais zanzibar kwa tiketi ya ccm naona wanafanya mzaha sana na sijui hata kama wanajua majukumu wanayotaka kubebeshwa. Mtu aistoria ya na elimu ndogo, hana historia ya kutatua lolote kwa kidiplomasia, ameshindwa kupata kura za uwakilishi katika jimbo lake huko nyuma kwa sababu watu hawaamini kama ana sifa za uongozi, hana ujuzi au elimu ya uongozi na siasa za nje, hajui lolote juu ya mahusiano ya nchi za kimataifa, historia yake katika nyadhifa alizowahi kuongoza ni failure tupu, uhodari aliokuwa nao ni kupiga domo tu haalafu anataka kuwa rais, Wengine nao wanataka uraisi kwa kutumia makoti ya baba zao. Kwa kuwa tu baba zao waliwahi kuwa maraisi basi wanafikiri na wao wanastahiki kuwa maraisi. Wanadhani zanzibar inaendeshwa kwa mfumo wa dynasty.