Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE AMINA MZEE & TAUHIDA GALLOS: DODOMA MJINI ICHAGUENI CCM, HAMTAJUTA KUICHAGUA CCM
Wabunge wa Viti Maalum (CCM), Mhe. Amina Ali Mzee na Mhe. Tauhida Gallos Nyimbo (MNEC) wamewasihi Wananchi wote wa Wilaya ya Dodoma Mjini kuchagua viongozi wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa Unaotarajiwa Kufanyika tarehe 27 Novemba, 2024.
Mbunge Amina Ali Mzee na Mbunge Tauhida Gallos Nyimbo wamefanya ziara tarehe 22 Novemba, 2024 katika Kata ya Miyuji na Kata ya Chamwino huku wakiwaombea Kura kwa Wananchi Wenyeviti wa Mitaa Saba (7) wanaogombea Wilaya ya Dodoma Mjini
Akizungumza na wananchi, Tauhida Gallos Nyimbo amewatambulisha Wagombea Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wanaotokana na CCM na kusema Akina Baba na Akina Mama hawatajuta kuichagua CCM kwahiyo waichague CCM kwa kura za kutosha.
Naye, Amina Ali Mzee, Mbunge wa Viti Maalum Vijana Tanzania amezidi sana kuwahamasisha Vijana nchini kote kujitokeza kupiga kura za kishindo ili Wagombea wanaotokana na CCM washinde kwa kishindo katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Unaotarajiwa Kufanyika tarehe 27 Novemba, 2024.