"A girl is the product of her society"... This is 100% rightA girl/woman is a product of her society. 99.9 ya namba tunazoombwa na strangers ni kwaajili ya mtongozo, unnecessarily ! Kabla hatujalaumu wanawake, hebu “sisi” wanaume tujikague.
Kitu ambacho una overlook ni kwanini wanawake “wanatoa namba na hawapokei simu” Umeshasikia mara ngapi msichana anakuwa bullied only kwasababu amekataa kusimama barabarani kumpa ME namba/attention or whatever alicho aim? Kitu hujui ni kuwa wanawake tumejitengenezea “surviving mechanism” katika huu ulimwengu wa kiume. Kadogo2 huko juu amesema kuna mazingira haiwezekani kuacha kutoa namba, as a woman nimemuunga mkono and other women can relate.
Looks like nimepata another Natafuta Ajira wakuargue nae kila thread ya wanaume vs wanawake! 😀
Yes, traditionally in any society men are the pioneers/leaderz and women are followers, I mean they flows with social setting whims that men have initially created.
Ndio maana kwenye comment yangu ya awali kabisa nimesema sitaki kuwalaumu sana wanawake maana wao sio chanzo Cha tatizo,
...ila nitawalaumu wanawake kwa kushindwa kutoka nje ya box, maana si mara zote mwanaume akikiomba namba basi mtaishia kwenye mtongozo, muda mwingine wewe mwanamke unaweza ukajikuta unanufaika bila kitarajia.
Mfano, Mimi Kuna kipindi Fulani wakati nauza mitumba nilichukua namba ya dada mmoja hivi, lengo lilikuwa ni Hilo Hilo kuja kumtongoza.
Katika maongezi yetu hata Kabla sijamtongoza akaniambia yeye ni mke wa mtu, akanikata na mood kabisa ya kumtongoza maana huwa sidate wake za watu, Mimi naona ni heri nikadate baamedi kuliko mke wa mtu.
Sasa yule dada baada ya Mimi kupunguza mawasiliano na yeye, akawa mara nyingi yeye ndio ananitafuta, akaja akaniambia ana mtoto wa dada yake amemaliza form four kafeli yupo tu nyumbani hivyo akataka aniunganishe nae nimfundishe kufanya biashara ya mitumba... Na Mimi sikuwa na baya lolote nikafanya hivyo.
Sasa kwa scenario hii unaweza ukaona jinsi gani yeye ndio alinufaika na Mimi licha ya kwamba Mimi ndio nilimuomba namba yake na Wala hata sikutimiza ile dhamira yangu.
Kuhusu wanawake kuwaignore wanaume Kama surviving mechanisms dhidi ya usumbufu wanauopata huko mabarabarani, hapo ninawaunga mkono kabisa, na mwanaume yeyote anaye muharasse mwanamke aidha kwa kumtukana au kumtishia kisa tu amekataa kuitika baada ya kupigiwa mruzi, mwanaume huyo anastahili kuchukuliwa hatua Kali sana, maana wewe mwanamke ukiitwa na mwanaume kusimama au kutosimama ni uamuzi wako, binafsi hata Mimi huwa naichukia sana hii tabia ya wanaume wenzangu.
Suala la kutoa namba halafu baadae unapigiwa simu hapokei, unatumiwa meseji haujibu bila hata kujua mtu huyo anataka nini kwako huo ni ushamba.