Akina dada, kwanini mnakubali kutoa namba kisha mkipigiwa simu hampokei?

Akina dada, kwanini mnakubali kutoa namba kisha mkipigiwa simu hampokei?

Mbona msiwaombe hao business woman mnatuomba sie chakaramu… yaani sina Biashara na wewe.. sikufahamu na sihitaji kuongeza Idadi ya marafiki wa kiume kwenye simu yangu sasa hiyo fursa iko wapi

Mkiombwa hela mje mfungue uzi hapa.. likuepukalo lina heri ukiona mtu harespond you call jua hayuko interested na wewe.. Mbona kuna wenginee wanapewa namba na wanazungumza.

Yaani wanaume mnashangaza tukianza kuongea na kila tunaempa namba si itakuwa tumejaza simu fikiria kwa wiki umekutana na wanaume wapya 20 na wote wameomba namba… kwaiyo ufanye kazi ya kuwajibu na kupokea simu zao ambazo wanatuma sms mambo, hello, niambie…

Kama hujajibiwa wala kupokelewa simu within 1 week achana na huyo kiumbe ujue hayuko interested na wewe

Kwanza wanaume mnaomba namba kwa kila mdada unakuta kijana ameomba namba kwa siku wadada Kama 10 wote anawatafuta sijui huwa mnajisikiaje[emoji174]
Wasipokuelewa hapa wakapimwe mkojo.
 
Haupati faida kwa kunisingizia majambo, tafadhali kuwa mkweli kuwa ulinipotezea, kiri haya kwa wana jukwaa ili tuanze upya! 😀

(kiswahili changu kama cha ChatGPT)
Labda hukusikia simu inavyoita kwasababu wewe ni Binti Kiziwi, lakini nilipiga sana simu.
 
A girl/woman is a product of her society. 99.9 ya namba tunazoombwa na strangers ni kwaajili ya mtongozo, unnecessarily ! Kabla hatujalaumu wanawake, hebu “sisi” wanaume tujikague.

Kitu ambacho una overlook ni kwanini wanawake “wanatoa namba na hawapokei simu” Umeshasikia mara ngapi msichana anakuwa bullied only kwasababu amekataa kusimama barabarani kumpa ME namba/attention or whatever alicho aim? Kitu hujui ni kuwa wanawake tumejitengenezea “surviving mechanism” katika huu ulimwengu wa kiume. Kadogo2 huko juu amesema kuna mazingira haiwezekani kuacha kutoa namba, as a woman nimemuunga mkono and other women can relate.

Looks like nimepata another Natafuta Ajira wakuargue nae kila thread ya wanaume vs wanawake! 😀
Sasa kutoa namba na kuto respond unapopigiwa au tumiwa sms ndio surviving mechanism?.

Surviving mechanism ni kukataa kutoa namba from the first place kama utaona huyu mwanaume sio wa taste yako.

Mwanamke kutongozwa sio jinai wala udhalilishaji, na kama haujavutiwa na uyo mwanaume unamkatalia tu ombi lake.
 
Baada ya stori mbili tatu ukaombwa namba na umetoa mwenyewe bila kushikiwa kisu, manati wala bunduki, lakini cha ajabu ni wiki ya pili sasa simu hujawahi kupokea hata siku moja na ikipigwa inaita vizuri tu. Meseji ndo kabisaa kama huzioni vile.

Sasa ulikua unatoa namba ya nini?
Hauna hela wewe
 
Si mnasema si vizuri kutanguliza pesa mbele sasa hapa inakuaje tena? Na ukishampata akikuomba hela mbeleni utaendelea kumpa au ndio inakua bye bye??
Akiwa mtu wakuomba hela sana anamrahisishia mwanaume kujua huyu ni wa hit and run
 
Pole, mvumilie. Mimi huwa nashangaa wale wanaume wakiomba namba wasipopewa wanaporomosha mvua ya matusi, hawa nao unawaweka kundi gani?
Kwenye kundi la wapumbavu.
 
Si usubiri ujibiwe au upigiwe?
Unakuwa unamtakia nini na haraka haraka hiyo!!!

Ila wengine eti wanapima na wengine wanapimisha na aliyenaye😅

Kwa wa Dada wengi unga muamala hata buku 20 sema ya maji.. usikilizie huku uki......

Vaa vizuri nenda BOT au benki zenye kuzungusha 💲 pozi kama unachekelea. rusha status andika "mkutano wa mameneja umeenda vizuri.. Kazi iendelee.." nunua cha kuvaa kwenye kola kishike mkononi iwe kama umeshika ID yako.

Kumbuka kuweka privacy aone mlengwa tu 😅😅
Huu ni uhuni😂
 
Huu ni uhuni😂

Wanawake wengi tunapenda wasio kama maboga, Moyo ukipewa chalenjiz na heshima iwepo zoo hapo utafurahia sanaaaa..
Na kupendwa ila mwanaume tumia akili.

Sio kila dk masimu kama huyo, ukipigiwa pokea zooo ukiringa makusudi or upo bizi basi meseji au masimu ka dk chache muhimu

Lege Lege wa kuambiwa na kufata kila jambo aisee utapoteza nyapu akikaa nawe basi kuna kitu anataka..

Chalenji 😘 huku mahaba moto motooooo
 
Asante kwa kunielewaga, na pole sababu hutopenda kila ninachochangia.

Nilichosema ni mtazamo wa kike zaidi, ni wanawake tu watauelewa, nikisema ni wanawake wangapi walishakutwa na aibu ya kutoa namba ya uongo na ikapigwa hapo hapo bila shaka ni wengi, katika kutafuta namna bora ya kusurvive ndio tukaja na hiyo mbwinu.

Halafu suala la namba kuna watu wanabetianaga kabisa, kuwa pale nachukua namba, kutokumpa namba ni kubleach ego yake mbele ya wenzake, kwani ni ngumu kiasi gani kumfanya mtu ajisikie vizuri kwa muda? Matokeo atapambana nayo baadae kwasababu sio waomba namba wote huwa wapo serious wengine wapo mazoezini…..

Naongea real life situations, kuna uzi humu mkaka analalamika hana confidence, wakumshauri wakamshauri, mwingine kaja akamshauri anza kwa kutongoza wadada na kuomba namba you will gain your confidence, hii ni case moja ndogo, Je tujiulize ni ngapi na huwa zinatutokea mara ngapi.

Kuna sababu nyingi za msingi za kumpa mtu namba akiomba, hapo bado haujakutana na yule uliyeamua kumpokelea simu ukamjibu kuwa “sipo interested “ na mahusiano na wewe….. Mara nyingi tu tunakula vichambo.

Bottom line wanaume hamko perfect, let women be!
Sawa sasa ile ishu yetu vp? Mana namba yako niliyonayo haipatikani Madam lake 🤗

Ebu un lock kidogo bana
 
Wanawake wengi tunapenda wasio kama maboga, Moyo ukipewa chalenjiz na heshima iwepo zoo hapo utafurahia sanaaaa..
Na kupendwa ila mwanaume tumia akili.

Sio kila dk masimu kama huyo, ukipigiwa pokea zooo ukiringa makusudi or upo bizi basi meseji au masimu ka dk chache muhimu

Lege Lege wa kuambiwa na kufata kila jambo aisee utapoteza nyapu akikaa nawe basi kuna kitu anataka..

Chalenji 😘 huku mahaba moto motooooo
Huenda upo sahihi
 
Mentality ya kitoto na ya kishamba? Haya bwana hayo ni mawazo yako nayaheshimu. Uwe na siku njema!
Kwangu Mimi binafsi naiona hivyo aisee, lakini kama nilivyosema awali ni kutokana na aina ya jamii tuliyonayo.
 
Kwann ulazimishe kumuomba namba kama vip mpe yako akikupigia ni sawa akipotezea ni sawa wanaume lazima tuache ushamba wa namna hi ii
 
Back
Top Bottom