Akopea nyumba ya jirani Milioni 200 kwa Hati Feki. Malalamiko yalifika hadi Ikulu danadana nyingi

Akopea nyumba ya jirani Milioni 200 kwa Hati Feki. Malalamiko yalifika hadi Ikulu danadana nyingi

Kuna mama anaitwa Zaidia Ijango ana taaasisi yake fake ya kulea watoto yatima maeneo ya sinza madukani nae amefoji documents anataka kudhulumu.nyumba aliyopanga kwa mdu mrefu
 
huyu anafatilia mal za babu yake? hivi sheria inawatambua wajukuu kwenye mirathi ?
 
Kama amekopea nyumba ya jirani kwa hati feki tatizo ni la benki waliomkopesha na sio mwenye nyumba as long as ana hati halali. Unless kuna vitu havisemwi lakini benki ni taasisi kubwa na wanafanya due diligence ya uhalali wa nyaraka kabla hawajatoa mkopo kwa mhusika.​
 
Kwa zama hizi huwezi kutengeneza hati mbili kwenye kiwanja kimoja. Database inakataa kutoa hati ya pili.

Jamaa alifanya zama za zamani zamani kabla ya hati zote kuingizwa kwenye system
Naomba kukuuliza iwapo wazazi wamefariki bila kuelekezwa hati miliki kwahiyo haijulikani ilipo
Je inawezekana nyumba kukatiwa hati upya inachukua muda gani na inagharimu kiasi na utaratb ukoje
 
Naomba kukuuliza iwapo wazazi wamefariki bila kuelekezwa hati miliki kwahiyo haijulikani ilipo
Je inawezekana nyumba kukatiwa hati upya inachukua muda gani na inagharimu kiasi na utaratb ukoje
Una uhakika hiyo nyumba inasoma majina yao!? Jiridhishe kwanza alafu mambo mengine ndiyo yaendelee!!
 
Daa inauma sanàa...pole familia wame take asvantage ya umasikini wa huyo dogo.....
 
Mtu mmoja ambaye ametajwa kwa jina la Mkwabi Nyanda akishirikiana na Mkewe wanadaiwa kugushi nyaraka za hati ya nyumba ya Jirani yao eneo la Kinondoni Jijini Dar es salaam na kutumia hati feki kukopea benki Jijini Arusha Tsh. milioni 150 mwaka 2016 na kisha milioni 200 mwaka 2017 na kupelekea benki hiyo sasa kutaka kuuza nyumba huku Familia inayomiliki nyumba hiyo ikisema haihusiki na mkopo huo wala haiutambui.

Kijana Dotto Said(19) ambaye nyumba hiyo ni ya Babu na Bibi yake amesema katika mapambano ya kuinusuru nyumba ya Familia isiuzwe amefika hadi Ikulu kupeleka barua aliyomuandikia Rais ambako aliambiwa Rais ameiona barua yake na ameagiza aiandike barua kama hiyo kwa Waziri wa Ardhi (nakala iende TAKUKURU, kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, kwa IGP na DPP) ili atatuliwe shida yake haraka kwakuwa tayari benki imewataka waondoke ili nyumba iuzwe kwakuwa Mahakama imetoa maamuzi kuwa benki iuze nyumba hiyo.

Dotto amesema “Tulishafungua kesi ya kugushi kwenye Kituo cha Polisi Oysterbay (Dar es salaam), baada ya upelelezi Mtuhumiwa akabainika yupo Arusha, Polisi wakataka Tsh. milioni 1.5 kwenda kumkamata Arusha tukawapa wakaenda na gari Dogo Askari watatu wakamkamata wakati wanarudi nae kuja Dar es salaam Askari wanasema wamefika Mombo Hotelini Mtuhumiwa alikuwa ananuka wakamwambia aende chooni akajisaidie baadaye akatoroka kupitia dirishani”

“Wakarudi Arusha kumkamata Mkewe na walipofika Dar Mke akakiri kwenye mkopo benki waligushi ambapo yeye alisimama kama Zainab (Bibi yangu) na Mumewe akasimama kama Abraham (Babu yangu) lakini baadaye Mke kaachiwa, ombi langu tunaomba benki ituachie nyumba yetu, benki imtafute aliyewatapeli kwasababu yupo, tunamuomba Mh.Rais, Waziri na Watanzania wote watusaidie”

Baada ya Ayo TV kurusha habari hii kwa urefu kwenye Youtube ya MilardAyo siku chache zilizopita, leo July 01,2024, Dotto amesema wameitwa kukutana na Waziri wa Ardhi, Jerry Silaa ofisini kwake na amewaahidi kuwasaidia wapate haki yao “Tunaishukuru Ayo TV, tumeonana na Waziri amesema ameiona habari Ayo TV na pia nimeambiwa Rais Dkt. Samia nae ameiona habari Ayo TV na ameagiza kwa msisitizo tusaidiwe, nitawajulisha jambo litakapofikia na kitakachojiri”

View attachment 3030557
Hapo kuna harufu ya rushwa ,benki hawawezi pokea hati feki. bank huwa zinafanya morgage ambazo zinasajiriwa ardhi .

waende mahakamani
 
Una uhakika hiyo nyumba inasoma majina yao!? Jiridhishe kwanza alafu mambo mengine ndiyo yaendelee!!
Nitajiridhisha wapi Sasa na ndo wamefariki tayari Ila Nina uhakika tu kua nyumba ni yao Ila hiyo hati ndo haionekani
 
Chukua no ya kiwanja nenda Aridhi watakwambia inasoma nani!!
Unaweza kunipa namba yako?
Swala ni kwamba Sina detail yoyote wazazi wamefariki ghafla hatukuzungumza chochote sababu haikutarajiwa.....nachofaham ni namba ya nyumba tu nisaidie tafadhal nijue pa kuanzia
 
Naomba kukuuliza iwapo wazazi wamefariki bila kuelekezwa hati miliki kwahiyo haijulikani ilipo
Je inawezekana nyumba kukatiwa hati upya inachukua muda gani na inagharimu kiasi na utaratb ukoje

taratibu za mirathi lazima zifanyike.

kisha msimamizi wa mirathi aende wizara ya ardhi atapewa utaratibu wa kupata hati mpya
 
Unaweza kunipa namba yako?
Swala ni kwamba Sina detail yoyote wazazi wamefariki ghafla hatukuzungumza chochote sababu haikutarajiwa.....nachofaham ni namba ya nyumba tu nisaidie tafadhal nijue pa kuanzia

wauulize jirani zako namba ya viwanja vyao.

ukitazama hati za jirani zako, utaona site plan inaonesha namba ya kiwanja chenu
 
wauulize jirani zako namba ya viwanja vyao.

ukitazama hati za jirani zako, utaona site plan inaonesha namba ya kiwanja chenu
Oh nashkuru sana, kwahiyo unamaanisha kwenye hati za jirani yangu naweza kupata namba ya kiwanja chetu
 
taratibu za mirathi lazima zifanyike.

kisha msimamizi wa mirathi aende wizara ya ardhi atapewa utaratibu wa kupata hati mpya
Sawa nimeelewa kua mambo ni mawili ya lazima 1.taratibu zairathi
2.wilayani kitengo Cha ardhi
Naomba kuuliza swali la mwisho,
Je,unaposema taratibu za mirathi ni kama zipi na wahusika/zinawahusisha nani na
nani ni lazima wahusike kuzikamilisha

Kwa maana ya kwamba kabla ya kifo Cha mama kulikua na kikao na mrithi na msimamizi akachaguliwa....Ila maandishi na kila taarifa ndo kaondoka nayo mzazi
 
Back
Top Bottom