Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Inataonyeshwa vidhibitisho na wahusika. MUHUMU: mwenye nyumba hana kosa anaweza kuombwa kuwa shahidi wa kuthibitisha hati ni feki
Nawajua tabia zenu 😀Hahaha wakati umesoma na kukulia kwetu. Nadhani wewe nakufaham kweli sijawahi kukuona tacri kahawa machame?
Na Mahakama inatowaje hukumu yenye mgogoro wa hati bila ya kumwita msajili wa hati kutoka Aridhi ili kuitambua hiyo hati kama ni fake au original!!??
Naomba kukuuliza iwapo wazazi wamefariki bila kuelekezwa hati miliki kwahiyo haijulikani ilipoKwa zama hizi huwezi kutengeneza hati mbili kwenye kiwanja kimoja. Database inakataa kutoa hati ya pili.
Jamaa alifanya zama za zamani zamani kabla ya hati zote kuingizwa kwenye system
Una uhakika hiyo nyumba inasoma majina yao!? Jiridhishe kwanza alafu mambo mengine ndiyo yaendelee!!Naomba kukuuliza iwapo wazazi wamefariki bila kuelekezwa hati miliki kwahiyo haijulikani ilipo
Je inawezekana nyumba kukatiwa hati upya inachukua muda gani na inagharimu kiasi na utaratb ukoje
Hapo kuna harufu ya rushwa ,benki hawawezi pokea hati feki. bank huwa zinafanya morgage ambazo zinasajiriwa ardhi .Mtu mmoja ambaye ametajwa kwa jina la Mkwabi Nyanda akishirikiana na Mkewe wanadaiwa kugushi nyaraka za hati ya nyumba ya Jirani yao eneo la Kinondoni Jijini Dar es salaam na kutumia hati feki kukopea benki Jijini Arusha Tsh. milioni 150 mwaka 2016 na kisha milioni 200 mwaka 2017 na kupelekea benki hiyo sasa kutaka kuuza nyumba huku Familia inayomiliki nyumba hiyo ikisema haihusiki na mkopo huo wala haiutambui.
Kijana Dotto Said(19) ambaye nyumba hiyo ni ya Babu na Bibi yake amesema katika mapambano ya kuinusuru nyumba ya Familia isiuzwe amefika hadi Ikulu kupeleka barua aliyomuandikia Rais ambako aliambiwa Rais ameiona barua yake na ameagiza aiandike barua kama hiyo kwa Waziri wa Ardhi (nakala iende TAKUKURU, kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, kwa IGP na DPP) ili atatuliwe shida yake haraka kwakuwa tayari benki imewataka waondoke ili nyumba iuzwe kwakuwa Mahakama imetoa maamuzi kuwa benki iuze nyumba hiyo.
Dotto amesema “Tulishafungua kesi ya kugushi kwenye Kituo cha Polisi Oysterbay (Dar es salaam), baada ya upelelezi Mtuhumiwa akabainika yupo Arusha, Polisi wakataka Tsh. milioni 1.5 kwenda kumkamata Arusha tukawapa wakaenda na gari Dogo Askari watatu wakamkamata wakati wanarudi nae kuja Dar es salaam Askari wanasema wamefika Mombo Hotelini Mtuhumiwa alikuwa ananuka wakamwambia aende chooni akajisaidie baadaye akatoroka kupitia dirishani”
“Wakarudi Arusha kumkamata Mkewe na walipofika Dar Mke akakiri kwenye mkopo benki waligushi ambapo yeye alisimama kama Zainab (Bibi yangu) na Mumewe akasimama kama Abraham (Babu yangu) lakini baadaye Mke kaachiwa, ombi langu tunaomba benki ituachie nyumba yetu, benki imtafute aliyewatapeli kwasababu yupo, tunamuomba Mh.Rais, Waziri na Watanzania wote watusaidie”
Baada ya Ayo TV kurusha habari hii kwa urefu kwenye Youtube ya MilardAyo siku chache zilizopita, leo July 01,2024, Dotto amesema wameitwa kukutana na Waziri wa Ardhi, Jerry Silaa ofisini kwake na amewaahidi kuwasaidia wapate haki yao “Tunaishukuru Ayo TV, tumeonana na Waziri amesema ameiona habari Ayo TV na pia nimeambiwa Rais Dkt. Samia nae ameiona habari Ayo TV na ameagiza kwa msisitizo tusaidiwe, nitawajulisha jambo litakapofikia na kitakachojiri”
View attachment 3030557
Nitajiridhisha wapi Sasa na ndo wamefariki tayari Ila Nina uhakika tu kua nyumba ni yao Ila hiyo hati ndo haionekaniUna uhakika hiyo nyumba inasoma majina yao!? Jiridhishe kwanza alafu mambo mengine ndiyo yaendelee!!
Chukua no ya kiwanja nenda Aridhi watakwambia inasoma nani!!Nitajiridhisha wapi Sasa na ndo wamefariki tayari Ila Nina uhakika tu kua nyumba ni yao Ila hiyo hati ndo haionekani
Unaweza kunipa namba yako?Chukua no ya kiwanja nenda Aridhi watakwambia inasoma nani!!
Naomba kukuuliza iwapo wazazi wamefariki bila kuelekezwa hati miliki kwahiyo haijulikani ilipo
Je inawezekana nyumba kukatiwa hati upya inachukua muda gani na inagharimu kiasi na utaratb ukoje
Unaweza kunipa namba yako?
Swala ni kwamba Sina detail yoyote wazazi wamefariki ghafla hatukuzungumza chochote sababu haikutarajiwa.....nachofaham ni namba ya nyumba tu nisaidie tafadhal nijue pa kuanzia
Oh nashkuru sana, kwahiyo unamaanisha kwenye hati za jirani yangu naweza kupata namba ya kiwanja chetuwauulize jirani zako namba ya viwanja vyao.
ukitazama hati za jirani zako, utaona site plan inaonesha namba ya kiwanja chenu
Sawa nimeelewa kua mambo ni mawili ya lazima 1.taratibu zairathitaratibu za mirathi lazima zifanyike.
kisha msimamizi wa mirathi aende wizara ya ardhi atapewa utaratibu wa kupata hati mpya
Oh nashkuru sana, kwahiyo unamaanisha kwenye hati za jirani yangu naweza kupata namba ya kiwanja chetu