Akumbukwe John Okello, Baba wa Taifa la Zanzibar. Bila huyu leo Zanzibar wangekuwa bado Utumwani

Comment yako Ina make sense.
 

Msikilize hapo akiongea akiwa na Karume.

Kijana mdogo sana miaka 29 akapindua nchi. Bila Okello Zanzibar ingekua bado chini ya Sultani.

Okello tutakukumbuka Daima, haijalishi umekufa ila kumbukumbu yako haitafutika.

wazanzibari wenyewe wanamkumbuka Sultan wanatamani angelikuepo baada ya kupata kisago kizito kutoka kwa CCM kwa miaka karibu 60 sasa.
 
Ohh naisi.
Je mzee Karume alikuwepo kisiwani wakati was mapinduzi akishiriki bega kwa bega?
Pengine hakuwepo! Ndo maana anaskika okelo akimwita.je alikuwa wapi?
Na kwanini amekimbia?
Na Ni kwanini aitwe yeye badala ya wengine ?

Mzee Karume hakushiriki kwenye harakati za Mapinduzi, Uraisi wa Zanzibar aliupata kwa kupitia Mgongo wa Nyerere
 
Hakuna jambo kama hilo. Lafudhi inatisha watu iweje? Mbona hapo ameongea lafudhi yake ni ya kawaida tu? So Zanzibar walikuwa wana sauti nyororo na walikuwa woga hata wa sauti tu?
Komeo...
Inaweza kuwa tabu kuelewa.
Mimi naeleza kama nilivyotafiti namna tangazo la Okello lilivyoshtua pamoja na vitisho vyake vya kuua watu.

Ikiwa huamini hakuna tatizo.
 
Komeo...
Inaweza kuwa tabu kuelewa.
Mimi naeleza kama nilivyotafiti namna tangazo la Okello lilivyoshtua pamoja na vitisho vyake vya kuua watu.

Iliwa huamini hakuna tatizo.
Mimi nadhani John Okello apewe hadhi yake pasina Husda au Kinyongo. Bila huyu pengine mpaka leo Zanzibar isingekuwa huru.
 
Mi nadhani John Okello apewe hadhi yake pasina Husda au Kinyongo. Bila huyu pengine mpaka leo Zanzibar isingekuwa huru.
Chizi...
Nimeeleza hapa kuwa mapinduzi ya Zanzibar huwezi kuyaeleza kwa kuanza na usiku wa tarehe 11 Januari kuamkia tarehe 12 na kufika asubuhi serikali ya Mohamed Shamte ikawa imeanguka.

Mipango ya kupindua serikali ilianza nyuma sana na sehemiu kubwa ya kufanikisha mapinduzi imetoka Tanganyika ikihusisha vyombo vyake vya usalama.

Unaijua Kambi ya Kipumbwi?
Unaujua mchango wa Kassim Hanga na Kambona?

Vipi kuhusu Engen au Aboud MmasaI?

Soma kitabu cha Harith Ghassany, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,'' kitabu hiki kitakufungulia mengi.

Kitabu hiki kitakupeleka kwa walioshiriki mapinduzi ambo wewe majina yao hujapata kuyasikia hata siku moja.

Ali Mwinyi Tambwe kapewa nishani ya mapinduzi baada ye kufa kwake.

Wapo walioshtuka kusikia kuwa alishiriki katika mapinduzi kwa kuwa hakuna popote katika historia ya mapinduzi ambako ametajwa.

Hawa wako wengi sana.
 

End justifies the begining. Wengine walifeli hadi mpaka hapo okelo alipo oongoza mapinduzi na yakafanikiwa huku hao unaosema maplanner wakiwa wamejificha gest house tanganyika kama panya wajifichavyo mafichoni.

All in all okello apewe heshima yake katika mapinduzi ya zenji bila yeye yaaingetokea.

Kwanini hamtaki kumpa heshima yake badala yake wanapewa heshima waliojificha mashimoni wakati mwanaume akiongoza mapambano. ?
 
Maelezo yako yana upungufu.
Inawezekanaje mtu ambaye hakushiriki kuongoza mission apewe kutangaza ushindi ?
Wakati mission inaendelea kiongozi alikua na John Okello muda huo alikua wapi ?

Kwa akili ya kawaida watu wanaogopa sauti au wanaogopa mtu aliyeleta ushindi Kwa kutuma silaha ?
Inawezekana vp kiongozi aliyeongoza mapinduzi hayo ampe sifa Mpita njia ambaye hakushiriki !

Nikipata ufafanuzi wa hoja hizi ndipo nitakuelewa, nje ya hapo tusipindishe maneno tumtambue tu Jemedari J. Okello.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…