Frank Ritte
Member
- Oct 21, 2022
- 68
- 97
Ovyoo...Chizi...
Nimeeleza hapa kuwa mapinduzi ya Zanzibar huwezi kuyaeleza kwa kuanza na usiku wa tarehe 11 Januari kuamkia tarehe 12 na kufika asubuhi serikali ya Mohamed Shamte ikawa imeanguka.
Mipango ya kupindua serikali ilianza nyuma sana na sehemiu kubwa ya kufanikisha mapinduzi imetoka Tanganyika ikihusisha vyombo vyake vya usalama.
Unaijua Kambi ya Kipumbwi?
Unaujua mchango wa Kassim Hanga na Kambona?
Vipi kuhusu Engen au Aboud MmasaI?
Soma kitabu cha Harith Ghassany, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,'' kitabu hiki kitakufungulia mengi.
Kitabu hiki kitakupeleka kwa walioshiriki mapinduzi ambo wewe majina yao hujapata kuyasikia hata siku moja.
Ali Mwinyi Tambwe kapewa nishani ya mapinduzi baada ye kufa kwake.
Wapo walioshtuka kusikia kuwa alishiriki katika mapinduzi kwa kuwa hakuna popote katika historia ya mapinduzi ambako ametajwa.
Hawa wako wengi sana.
Sawa uhusika wake ni upi hata kupewa radio kutangaza mapinduzi?.