Akumbukwe John Okello, Baba wa Taifa la Zanzibar. Bila huyu leo Zanzibar wangekuwa bado Utumwani

Akumbukwe John Okello, Baba wa Taifa la Zanzibar. Bila huyu leo Zanzibar wangekuwa bado Utumwani

Ila Okello anaonekana alikuwa ni mbabe na walimuogopa kama sio kumheshimu sana.
Mgeni,
ASP na Umma Party walikuwako wababe si Okello.

Okello alivuna kwenye "Mob Psychology."

Alikuwa mfano wa Musiba aliyekuwa anazungumza kwenye mitandao ya kijamii.

Ushamsikia tena Musiba?

Okello alipokutana na Hashil Seif (huyu ni comrade kasoma Cuba) ndani ya ndege Okello hakuweza kufanya lolote alisalimu amri.

Hakuweza kumkabili Hashil.

Wako wababe kutoka ASP ukihadithiwa unyama wao mwili utakusisimka.

Watu wenye uwezo wa kumzika mtu yu hai.

Nilikuwa nataka kuandika kuhusu kubakwa kwa binti mdogo wa Kihindi wakati mama yake anabakwa....

Nashindwa kuandika maneno ya huyu mama kuomba salama ya mwanae...

Aliyenihadithia ni kati ya hao washenzi...

Wengi mnaandika msiyoyajua.
 
Okello alipokutana na Hashil Seif (huyu ni comrade kasoma Cuba) ndani ya ndege Okello hakuweza kufanya lolote alisalimu amri.

Hakuweza kumkabili Hashil.
Na hawajui kuwa Hashil ni mmoja wa vijana waliokwenda Cuba kusomea guerilla warfare tactics. Vijana humu wangesikiliza na kuhoji kwa ustaarabu wangejifunza mengi lakini wao wamebaki na chuki tu dhidi ya watu fulani.
 
Ali Mwinyi Tambwe kapewa nishani ya mapinduzi baada ye kufa kwake.

Kwako Mzee Mohamed Said, Je Okello atapewa nishani yake lini ya kutangaza mapiduzi.

Okello ni baba wa mapinduzi Zanzibar hizo nyingine ni mbwembwe tu za wanasisa. Likini ukweli ni kuwa huyu Mgalatia amewaheshimisha wamakunduchi.
 
Frank...
Ilitakiwa apatikane mtu mgeni mwenye lafidhi ngeni masikioni mwa Wazanzibari ili ipatikane picha kuwa ASP imeleta wapiganaji kutoka nje hivyo kuzidisha hofu kwa wapinzani wao ZNP na ZPPP.
Hebu weka wazi kama hii ni kweli, je Okello alipatikanaje yaani walimtoa wapi kuja kutangaza. Na kwa nini wachague mkristo na sio muislamu.

Kuna kitu hakipo sawa kwenye maelezo yako
 
Ali Mwinyi Tambwe kapewa nishani ya mapinduzi baada ye kufa kwake.

Kwako Mzee Mohamed Said, Je Okello atapewa nishani yake lini ya kutangaza mapiduzi.

Okello ni baba wa mapinduzi Zanzibar hizo nyingine ni mbwembwe tu za wanasisa. Likini ukweli ni kuwa huyu Mgalatia amewaheshimisha wamakunduchi.
Siwezi kukubadili fikra yako kwa kuwa unatamani kuwa Okello ndiye awe aliyepanga mapinduzi na kuyatekeleza sababu tu unataka iwe hivyo kwa kuitukuza dini yako.

Lakini ukweli ni kinyume chake.
Kutangaza kuanguka kwa serikali hakumpi Okello kuwa mpangaji wa mapinduzi.

Ikiwa Okello ndiye mpangaji Kassim Hanga na Oscar Kambona watakuwa nani?

Vipi Julius Nyerere aliyeruhusu ardhi ya Tanganyika, Kipumbwi kutumika?

Nadhani unajua kuwa Okello hakutokea Kipumbwi.

Nadhani unajua pia haikutakiwa kabisa ifahamike kuwa ilikuwapo Kipumbwi.

Victor Mkello, Mohamed Omari Mkwawa, Abeid Mmasai, Lumumba...

Unajua historia za watu hawa?
Soma "Kwaheri Ukoloni..." uone upande wa pili wa mwezi.
 
Hebu weka wazi kama hii ni kweli, je Okello alipatikanaje yaani walimtoa wapi kuja kutangaza. Na kwa nini wachague mkristo na sio muislamu.

Kuna kitu hakipo sawa kwenye maelezo yako
Gitwa,
Nimeeleza tena na tena kuhusu Okello.

Okello hakuwa peke yake katika walioshiriki katika mapigano usiku ule wa mapinduzi.

Kulikuwa na Wamakonde wa Kipumbwi na ASP wenyewe.

Lakini ASP walitaka kuongeza "drama," katika tukio lile ndipo akachaguliwa Okello kuingia studio.

Serikali ilikuwa hapo haipo.
Si lazima uniamini.

Hakuzuii yeyote ukiwa unapenda kuona Okello ndiye aliyeleta Wamakonde kutoka Kipumbwi.
 
Mgeni,
ASP na Umma Party walikuwako wababe si Okello.

Okello alivuna kwenye "Mob Psychology."

Alikuwa mfano wa Musiba aliyekuwa anazungumza kwenye mitandao ya kijamii.

Ushamsikia tena Musiba?

Okello alipokutana na Hashil Seif (huyu ni comrade kasoma Cuba) ndani ya ndege Okello hakuweza kufanya lolote alisalimu amri.

Hakuweza kumkabili Hashil.

Wako wababe kutoka ASP ukihadithiwa unyama wao mwili utakusisimka.

Watu wenye uwezo wa kumzika mtu yu hai.

Nilikuwa nataka kuandika kuhusu kubakwa kwa binti mdogo wa Kihindi wakati mama yake anabakwa....

Nashindwa kuandika maneno ya huyu mama kuomba salama ya mwanae...

Aliyenihadithia ni kati ya hao washenzi...

Wengi mnaandika msiyoyajua.

Mzee acha hoja za kitoto,kwahiyo kama walikutana kwenye ndege ulitaka waanze kufyatuliana masase ama kupigana?mbona hii story yako ya kubumba inakosa mashiko.

Okello ni field marshal hata wikipedia imeandiika hivyo.

Unaweza tuelezea kuhusu ile picha ya karume akimshika mkono juu Okello ilimaanisha nini kwanini amshike mkono juu okello?
 
Okello john alishiriki mapinduzi kwa asilimia 100% , kwa sheria za kijeshi huwezi kushinda mapigano utangaze ushindi halafu ionekane baadae haukufanya chochote, alichofanya okello na makamanda wake kwenye redio ilikua kwanza kuwatangazia ushindi walioupata ulimwengu mzima lakini pili kuwaomba wote waliokimbia nchi warudi na hakuitwa karume tu ambae ni mmalawi hapana waliitwa wazanzibar wote waliokua uhamishoni warudi nyumbani kwani tayari mambo yalikua mazuri
 
John okello mjaluo kutoka Arua baada ya tangazo lile ndipo mipango ilifanywa ya wana ASP waliokimbia battle kurudi na bila hiyana aliwakabidhi nchi kama alivoahidi na aliweza kupewa cheo kwenye ulinzi wa nchi na baadae walipokorofishana na karume ndipo akafukwa zanzibar, akaondoka zake kurudi kwao lakini kimsingi aliiongoza zanzibar na historia imtambue
 
Karume hakupindua maana alikua Dar na hakua na jeshi hivo aliyepindua ni okello aliyekua na jeshi na ndio aliyekua na kikosi maalumu kilichofanya utekaji wa maeneo muhimu,
 
Kwenye mkonge, walimwenda wasukuma, wamakonde, wanyamwezi, wamwera, hadi wabena na wangoni walifika ndio maana tanga utawakuta akina ngonyani lakini hawapajui songea kabisa na kutoka Bara kuanzia kigoma huko, tabora , mwanza walitolewa wafanyakazi kwa njia ya treni kupitia reli ya kati, wamiliki wa mashamba ya mkonge waliamini watu wa pwani sio wachapakazi ni wavivu na ndio sababu za kutafuta nguvu kazi kutoka maeneo mengine nje ya pwani, hasa Tanga,
 
Hoja kubwa fieldmarshall John Okello atambuliwe kama mwanamapinduzi ambao ndio ukweli, maana ushahidi upo na japo historia inapotoshwa wazi wazi sema kosa kubwa alitaka kumpindua tena karume baada ya kuona mambo hayaendi ndio ukaombwa msaada Tanganyika akatimuliwa zanzibar na ukawa mwisho na kufinyangwa kwa historia yake,
 
Huyu ni Mmoja wa Mashujaa wa miaka ile aliyeshiriki kuwaondoa Makoloni huko Zanzibar. Kama ambavyo Bara nao walikuwa wameondoa wao.

Anasimulia mzee wangu ambaye alikuwa Mwalimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam miaka hiyo Che Guavera alikuja Tanzania mwaka 1965. Anasema Che alijaribu kuulizia habari za Mwanamapinduzi aliyesaidia kuipatia Zanzibar Uhuru wake John Okello.

Kwa his disappointment alishtuka kuambiwa the Man alifukuzwa mara baada ya kumaliza jukumu lililomleta Zanzibar kuwaondoa Waarabu waliokuwa wakiitawala Zanzibar.Aliwaokoa Waafrika kutoka kutawaliwa walipopata tu uhuru wakamfukuza.

John Okello Baba wa Taifa la Zanzibar ataendelea kukumbukwa kila tutakapoadhimisha Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Baada ya hapo John Okello alirudi kwao kwenda kuendeleza mapambano dhidi ya udhalimu na hatimaye alikuwa kama mtu wa kawaida tu pasipo makuu. Hakulipwa yeye wala familia yake. Kabla ya Mwaka 1967 Che Guevara kufariki aliwahi mtumia mzee wangu barua akimtaka amtafute John Okello wajiunge naye kwenye harakati huko Msumbiji na Angola.

Mzee hakujua aanzie wapi.
alisababisha mauaji ya watu wasio na atia hata yeye yuko anapambana na adhabu ya kablini moto kwenda mbele

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom