BlackPanther
JF-Expert Member
- Nov 25, 2015
- 9,185
- 8,715
Na ndio sababu hata Possession Al Ahly waliachwa mbali sana na Bayern Munich na pale kwa jinsi ligi ya Germany ilivyo hata angekuwa Mainz 😅 angemtoa sana jasho Al Ahly kwani sisi soka letu Afrika mpaka mtu anakuwa bingwa ni mwendo wa fitna tu na ushirikina hamna mpira wa mana tunaocheza tofauti na wenzetu Ulaya.
Kuachwa mbali possession sio sababu, hata Bayern angecheza na Arsenal angemzidi mbali pia, Monaco, Ac milan, Chelsea..wote hawa wangecheza na Bayern or Barcelona wangeachwa mbali mno.
Tambua pia soka la kaskazini sio level yetu hata kidogo, sio watu wa fitna wala ushirikina kama wale wazee walioingia na kuku. Waarabu wako vizuri mno, wanajua kulitendea haki soka lao. Lakini kusema fitna na uchawi nitakubishia mpaka basi.
Binafsi, najivunia uwepo wa timu za kaskazini katika bara letu, otherwise tungeishia kupata aibu kwa wazungu.