Al Ahly wanastahili kucheza hata UEFA Champions League

Al Ahly wanastahili kucheza hata UEFA Champions League

Na ndio sababu hata Possession Al Ahly waliachwa mbali sana na Bayern Munich na pale kwa jinsi ligi ya Germany ilivyo hata angekuwa Mainz 😅 angemtoa sana jasho Al Ahly kwani sisi soka letu Afrika mpaka mtu anakuwa bingwa ni mwendo wa fitna tu na ushirikina hamna mpira wa mana tunaocheza tofauti na wenzetu Ulaya.


Kuachwa mbali possession sio sababu, hata Bayern angecheza na Arsenal angemzidi mbali pia, Monaco, Ac milan, Chelsea..wote hawa wangecheza na Bayern or Barcelona wangeachwa mbali mno.

Tambua pia soka la kaskazini sio level yetu hata kidogo, sio watu wa fitna wala ushirikina kama wale wazee walioingia na kuku. Waarabu wako vizuri mno, wanajua kulitendea haki soka lao. Lakini kusema fitna na uchawi nitakubishia mpaka basi.

Binafsi, najivunia uwepo wa timu za kaskazini katika bara letu, otherwise tungeishia kupata aibu kwa wazungu.
 
vipi wameshinda ngapi?

Kufungwa ni kawaida Hata Barcelona yangu ilifungwa, chelsea ilifungwa, arsenal ilifungwa, A. Madrid ilifungwa n.k..sasa cha ajabu hapo ni nini!! Na isitoshe first time kukutananao.

Mkubali tu Al ahly na Wydad Casablanca ndio wafalme wa mpira barani Afrika..naongezea Raja Casablanca, Esperance, Mamelody, Zamalek na Pyramids ya Egypt.
 
Yes, no doubts

Nipo sebuleni kwangu naangalia mpira wa Al ahly vs Bayern Munich aiseee siamini kama kuna timu kutoka Africa inaweza cheza kwa kujituma katika level hiii. Timu za Tanzania zina safari kubwa ambayo itawachukua miongo kadhaaa kuwafikia hawa jamaaa.

Congratulations kwa league ya Misri, mpira ni pesa, mpira ni uwekezaji. Mpira sio press conference kila siku. Kufika level kunahitaji vision na sio ubabaishaji wa mitandaoni eti mnalinda brand. Huu ndio mpira sasa, hawa jamaa wanaweza cheza hata UEFA na kuna timu za kijinga jinga zinachezea goals za kutosha.

Ni hayo tu.
Mkuu, hao Wajerumani walikuwa wanajihadhari na mpira wetu wa Kiafrika.
Al Ahly wangecheza Kiulayaulaya wangenyeshewa mvua ya magoli zaidi ya Asenali.
Nashauri tu Afrika tuwe na mtindo wetu wa asili wa mchezo huu. Wasitulazimishe mitindo yao ambayo sasa Marekani ya Kusini imewamaliza kisoka.
 
Back
Top Bottom