Mwanamaji
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 2,905
- 4,518
Nakupinga hapo kwenye kuombea sare mechi ya leo. Ili Simba iwe salama kwenye mechi ijayo inatakiwa Al Ahly ashinde ili kupunguza presha kwenye mechi yao ijayo. Endapo Ahly atatoa sare au kufungwa leo, mechi ijayo itakua ni must-win kwa upande wao na kufanya mechi hiyo kuwa ngumu kwa Simba.
Nakuunga mkono mkuu.
Kuna watu wana mawazo mazuri kwamba Simba iongoze kundi (kwa Ahly kupoteza au kusare dhidi ya Merreikh)...
Hili lina madhara makuu mawili kwa Simba.
1. Kuongeza ugumu wa mechi kwa Simba dhidi ya Al Ahly.
Ahly akiwa na pointi chache kuliko Simba, atakuja kucheza kufa na kupona ili apate ushindi dhidi ya Simba. (Uwezo huu anao)
Ahly kupoteza pointi dhidi ya Merreikh kunaongeza demand ya points kutoka kwa Simba.
2. Kuongeza idadi ya washindani kwa Simba wanaowania nafasi mbili za kuvuka.
Merreikh akishinda leo maana yake atakua na points tatu lakini pia atakua ametuachia (Simba) msala wa Ahly aliyejeruhiwa.
Ahly akishinda Dar (narudia uwezo huu anao) maana yake timu tatu zinakua na points 3. Hii inahatarisha chances za Simba kwenye nafasi mbili za kuvuka.
NB:
Ni bora kukutana na Merreikh au AS Vita aliyejeruhiwa kuliko Ahly aliyejeruhiwa.
Kwa 70% ni kwamba Al Ahly anavuka hii hatua, kinachotafutwa kwa sasa ni anavuka na nani mmoja kati ya hawa watatu.
It is a fair bet Ahly atusaidie Simba kuwadhoofisha Vita na Merreikh, otherwise we are likely to pay a price (kupoteza point 4 au 6 kwa Ahly).