Al-Barzakh: Haya ndio Maisha ya Kaburini baada ya kufa

 
Faidika na Darsa la FaizaFoxy...

Unachanganya mambo sana usiyoyaelewa.

1) Kufa sio kuwa "Barzakh" kama unavyotaka kutuaminisha. Neno Kifo kwa lugha ya Kiarabu ni full stop. Kama unajua kidogo kusoma Kiarabu, hata vibao au saini zao za barabarani kwa Kiarabu zinaandikwa "Kif", kwa maana "stop". Kiswahili ndio tunakazia na kusema "Kifo".

2) Barzakh ni kizuizi "berrier", kwa maana wa uhai hayupo kwenye umauti na wa umauti hayupo kwenye uhai. Kati yetu ni hicho kizuizi (barzakh".

3) Umauti ni hali "state" nyingine ya kutokua hapa kwenye uhai, kuwepo kwenye umauti. Mfano tu, ni kama hali ya kuwa macho (conscious inatawala) na kuwa usingizini (subconscious inatawala. Tofauti ni kuwa upo hai hata ukilala.


Binafsi siamini katika adhabu za kaburi. Kwanza kwa kuwa hazijatajwa kwenye Qur'an, sijaziona. Pili Hadith iliyozitaja siikubali.

Ikiwa kuna adhabu ya kaburini basi Allah itakuwa katudanya (AstaghafiruAllah) anaposema kwenye Qur'an kuwa kuna siku ya kiama (Kusimamishwa) kuhukumiwa? Sasa iweje tena tuhukumiwe kabla ya Kiama?

Naamini kuwa tunapotoka kwenye uhai kuingia kwenye umauti na hadi siku ya Kiama hakutakuwa na feeling za muda kama vile tupo hai. Itakua ni mano wa watu wa Pangoni, kisa cha kwenye Qur'an) au alielala miaka 10 kisa cha Qur'an).

Kifo, kinachokufa ni hiki kiwiliwili (body) chetu, nafsi haifi bali inaingia kweye umauti. Qur'an inahakikisha hili kwa kutukumbusha kuwa "kila nafsi itauonja umauti".

Hata sehemu tu ya kiwiliwili inaweza kufa na nafsi bado haijaingia kwenye umauti. Mfano ukikatika mkono au mguu, unakuwa umekufa huo mkono au mguu lakini nafsi bado haijaonja umauti.

Pedagogic at Heart
 
Huzikubali hadithi hata kama ni sahihi?
 
Na wewe kipi kinachokufanya upinge kitu usichokuwa na uhakika nacho mpaka unashupaza mishipa ya shingo?
Wapi nimepinga, hebu onyesha sehemu niliyopinga. Kitu kisicho na proof yoyote ya either kufanya kikubalike au proof ya kufanya kisikubalike ni uzwazwa kuwalazimisha watu kwamba unavyoamini wewe ndiyo ukweli kamili.
 
Tunapokufa -Tunalala Usingizi mzitooo mpaka siku ya Ufufuko tukapate Staiki ya matendo yetu!! ( tunavyolala usiku ni Nusu kifo) Wale waliokufa wakiwa watenda mema wanaenda moja kwa moja kwenye makazi ya Mungu wao waliokuwa wakimwabudu inavyostaili na Kumtumikia...Je wafu wanalala usingizi au wanaanza teseka mara tu wakifa?? Kwa Wakristo na Waislam turejee kwenye hadithi inayoitwa

Al-Kahf- Seven Sleepers - Wikipedia..​

akuna sijui majoka yanayotesa wafu wala adhabu zinazoitwa adhabu za kaburini-Tukifa ni mizoga tu kama mizoga ya wanyama wengine Roho zetu kama zilivyo za Malaika(kwa wanaotenda na kuishi MEMA) na za Watenda Maovu(roho zao zitakuwa kama za Mashetani) na hapo utaanza ishi kiroho Mwili sio wako tena milele.kwa leo niishie hapo. Wewe ishi furahia maisha mwabudu Mungu wako, Timiza wajibu wako kama Binadamu, Kumbuka kuwa hapa Duniani wewe ni Msafiri siku yako ikifika Utaucha huu Mwili na Ulimwengu na Roho yako itasubiria hukumu wakati huo utoitaji Oxygen wala maji wala Upepo kupoza joto la ardhini
 
Ni sahihi uliyosema hapa🙏🏽
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…