Al-Barzakh: Haya ndio Maisha ya Kaburini baada ya kufa

Al-Barzakh: Haya ndio Maisha ya Kaburini baada ya kufa

Endeleeni kujifariji na hadaa za ulimwengu mkifikiri hakuna source ya maisha.

Nani alikuwa na uhakika wa kuzaliwa? Kwani binadamu wa kwanza alitoka wapi?
Utabishaje na utaachaje kuamini vitabu vitakatifu kuhusu miongozo mbali mbali wakati hip sayansi imevikuta. Vitabu?

Ni pumzi tu ndio inatuzubaisha. Hakuna ajuaye dakika moja mbele nini kitamtokea.

Maisha ya mwanadamu yote in siri. Mitume ilipewa miongozo ili kujua Muumba anataka nini. Kila kitu kimeelezwa.
Endeleeni kubisha
 
Yaani binadamu ni dhaifu tu.

Hebu tazama namna nguvu za Muumba zinavyoregulate mambo. Chukua fumbo LA rizki na mgawanyo wa chakula kwa viumbe. Ona mimea, ona wadudu, ndege, binadamu na viumbe wasioonekana. Hill in somo tosha kwa wenye akili kwamba kuna source beyond horizon zinafanya haya mambo yaende kwa mpangilio maalumu.

Sasa jiulize kama hujui mini kitatokea dakika moja mbele, utabishaje miongozo inayoelezea mambo kabla hao wanasayansi mahiri hawajazakiwa
 
Mafarao na watu wenye pesa walikuwa wanafanyiwa Embalment na hiyo iliwafanya waishi. Hata wewe ukifanyiwa mwili wako hautaoza karne na karne. Ni aina ya preservation. Na ilikuwa na maana kubwa kwenye imani yao juu ya maisha baada ya kifo!
Mfano ni ROZALIA LAMBARDO
 
Kifo sio fulustop bali ni alama ya comma,rejea kufa na kufufuka kwa Bwana Yesu na akatuambia anakwenda kwa Baba kututengenezea makao,

Rejea maneno ya Bwana Yesu,Nitalivunha hekalu na kulijenga kwa siku tatu yaani atakufa na kufufuka siku ya tatu.

Rejea kupaa kwa Eliya alipochukuliwa na Kigali cha moto na kuondoka nae,

Rejea kupalizwa mbinguni kwa Bikira Maria,

NB:Yote yanathibitisha kuwepo kuwa kifo sio mwisho Ila kuna maisha mengine baada ya kifo.

Nina shuhuda mbili:

1.Niliona wingu likishuka mahali fulani na lilipoondoka mahali hapo mtu alikufa,wingu lilikuja kumchukua,huo ni ukaribisho mwema kwenda kwenye maisha mengine.

2.Naliona Malaika wakitua mfano wa radi,radi ilipiga na ilipotua chini mfano wa Malaika alitokea,na mahali hapo alikuwa anatarajiwa kupita mtu fulani na alipopita baadae alikufa,Malaika wale walikuja kumchukua.

Sasa maisha baada ya kifo,kwa watu wema unaenda Paradiso,sehemu kama iliyokuwa bustani ya Eden utaendelea na maisha hadi Bwana Yesu atakapowachukua kuwarudisha tena duniani kutawala nae kwa miaka 1000 na baada ya miaka 1000 kuisha utashuka mji mpya wa Jerusalem na hukumu itapita na wale wema wataingia Jerusalem kuishi milele.

Kwa watu waovu wakifa watasubiri kwenye udongo hadi siku ya hukumu na kuhukumiwa kuingia Jehanamu.
 
Endeleeni kujifariji na hadaa za ulimwengu mkifikiri hakuna source ya maisha.

Nani alikuwa na uhakika wa kuzaliwa? Kwani binadamu wa kwanza alitoka wapi?
Utabishaje na utaachaje kuamini vitabu vitakatifu kuhusu miongozo mbali mbali wakati hip sayansi imevikuta. Vitabu?

Ni pumzi tu ndio inatuzubaisha. Hakuna ajuaye dakika moja mbele nini kitamtokea.

Maisha ya mwanadamu yote in siri. Mitume ilipewa miongozo ili kujua Muumba anataka nini. Kila kitu kimeelezwa.
Endeleeni kubisha
Umekurupuka sana kujibu ujinga. Umeona ulichonukuu kilikuwa ni jibu la swali gani? Ukiwa emotional ni rahisi kufanya makosa ya kijinga kama haya. Ukiisha tulia soma tena mtiririko halafu uje uandike tena comment ndefu kuliko hii
 
Hizi ni hekaya tuu, ukifa kwanza joto la mwili hushuka damu huganda, unapata rigor mortis, baadae bacteria wa utombo mkubwa wanaanza kukutafuna. Ila ikumbukwe wewe huna fahamu yani ndio basi tena mwili wako utatumika kusaidia maisha mengine humu duniani.
Mikwara ya ukifa sijui kuna adhabu[emoji1787][emoji1787][emoji1787] watu wanachomwa moto hilo kaburi wataliona wapi, watu wanaliwa na simba kabuti hilo wataliona wapi
 
Tunapokufa -Tunalala Usingizi mzitooo mpaka siku ya Ufufuko tukapate Staiki ya matendo yetu!! ( tunavyolala usiku ni Nusu kifo) Wale waliokufa wakiwa watenda mema wanaenda moja kwa moja kwenye makazi ya Mungu wao waliokuwa wakimwabudu inavyostaili na Kumtumikia...Je wafu wanalala usingizi au wanaanza teseka mara tu wakifa?? Kwa Wakristo na Waislam turejee kwenye hadithi inayoitwa

Al-Kahf- Seven Sleepers - Wikipedia..​

akuna sijui majoka yanayotesa wafu wala adhabu zinazoitwa adhabu za kaburini-Tukifa ni mizoga tu kama mizoga ya wanyama wengine Roho zetu kama zilivyo za Malaika(kwa wanaotenda na kuishi MEMA) na za Watenda Maovu(roho zao zitakuwa kama za Mashetani) na hapo utaanza ishi kiroho Mwili sio wako tena milele.kwa leo niishie hapo. Wewe ishi furahia maisha mwabudu Mungu wako, Timiza wajibu wako kama Binadamu, Kumbuka kuwa hapa Duniani wewe ni Msafiri siku yako ikifika Utaucha huu Mwili na Ulimwengu na Roho yako itasubiria hukumu wakati huo utoitaji Oxygen wala maji wala Upepo kupoza joto la ardhini
Hamna usingizi mzito ukifa tuu baada ya dakika chache seli zako huanza kufanya anerobic respiration, inatengeneza accetic acid, unapata rigor mortis then bacteria wa tumbo wanaanza kukutafuta na kutengeneza magesi ndio maana tumbo hujaa gas. Ukiendelea bacteria wanakutafuna mpaka unaoza [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]. Sasa hiyo kiama itakuwaje wakati lazima uoze. Ukiliwa na mnyama ndio basi tena unageuka choo
 
Yaani binadamu ni dhaifu tu.

Hebu tazama namna nguvu za Muumba zinavyoregulate mambo. Chukua fumbo LA rizki na mgawanyo wa chakula kwa viumbe. Ona mimea, ona wadudu, ndege, binadamu na viumbe wasioonekana. Hill in somo tosha kwa wenye akili kwamba kuna source beyond horizon zinafanya haya mambo yaende kwa mpangilio maalumu.

Sasa jiulize kama hujui mini kitatokea dakika moja mbele, utabishaje miongozo inayoelezea mambo kabla hao wanasayansi mahiri hawajazakiwa
Jambo moja, binafsi naamini kwamba kuna source beyond horizon. Hili ni wazi, maana hata sayansi imeshindwa kutoa majibu zaidi ya nadharia kwenye mambo mengi ya maisha yetu hapa ulimwenguni.
Mimi wasiwasi wangu ni kwenye hizi dini, pindi watu wanapobeba mambo mazima mazima bila kutumia akili. Nakupa mfano: unakuta imani fulani inatoa hukumu moja kwa moja kwamba imani fulani watu wake ni wa motoni tu licha ya watu wa imani hiyo kuutambua uwepo wa Mwenyezi Mungu, kisa tu wana practise tofauti na hiyo imani nyingine. Huu kwangu ni upotofu.
 
Kufa ni nini? Kufa ni hali ya roho kuepukana na kiwiliwili, au kufa ni kukatika matumizi ya roho kwa kiwiliwili na kukosa kiwiliwili ambayo ndio ala yake na kumuepusha mtu na mali yake na watoto wake na mke wake.

Kufa kunakata utamu wa maisha ya kiulimwengu na kwenda ulimwengu mwingine. Mtu ambaye alikuwa akifurahia maisha ya ulimwengu kwa kufanya ufedhuli amepata khasara baada ya kufa.

Na yule ambaye alikuwa akifurahi kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu basi atapata neema kubwa na inakamilika kufaulu kwake.

Watu wengi hudhania ya kwamba mtu anapokufa na akazikwa amemaliza kila kitu na amepumzika na ulimwengu, wala halimjii yeye jambo lolote.
Kudhani hivyo ni kosa kubwa bali hakika mwanadamu baada ya kufa kwake anaingia katika maisha mapya, maisha ya barzakh na kutoka maisha ya barzakh huenda kwenye maisha ya akhera ambayo ndiyo maisha ya mwisho na ya milele.

View attachment 2140429

Bar-zakh ni maisha ya baadaye; maisha baada ya haya tuliyonayo hivi sasa hapa duniani.

Maisha hayo kuanzia mtu anapokufa huitwa ni ‘Maisha Ya Barzakh’.
Barzakh ni kipindi baina ya wakati wa mauti na Qiyaamah. Na kila maiti atapitia katika maisha hayo, awe Muislam au Mkristo au asiye na dini, awe mwema au mwovu, na katika kipindi hicho kunakuwa na fitna na mitihani ya kaburi ambako mtu anajiwa na Malaika wawili na kuhojiwa na kisha hufuatia neema au adhabu za kaburini. Inajulikana kuwa kuna makazi matatu; makazi ya Dunia (Daarud-duniya), makazi ya Barzakh (Daarul-Barzakh) na makazi ya kudumu (Daarul-Qaraar).

Maisha ya kaburini ni kile kipindi anachokaa mtu baada ya kufa kwake mpaka kufufuliwa kwake. Kipindi kati ya parapanda la kwanza ambalo ni amri ya kufa viumbe vyote na parapanda la pili ambalo ni amri ya kufufuliwa viumbe vyote vitakavyotakiwa vifufuke, Huitwa Barzakh.

Katika kipindi hichi cha maisha ya dunia ni mambo gani yanayoendelea katika nafsi ya mwenye kufa? Wengi kwa kujiliwaza katika wakati huo hufikiria kuwa watu wakifa wanakuwa mapumzikoni. Na watu ambao hawaamini siku ya mwisho huamini kuwa kifo ndio mwisho wa maisha ya watu na iliyobaki ni kuoza na kuwa chumvi chumvi zitakazotumika ardhini.

Katika kipindi cha Barzakh roho za watu wema zitakaa pahali pazuri kungojea malipo yao ya Peponi, Ama zile za watu waovu zitakuwa mahabusu zikingojea siku ya hukumu yao. Ama kuhusu mtu muovu yeye atakaa katika kaburi lake kwa khofu na fadhaa.

Maisha ya Barzakh ni maisha yanayotofautiana kabisa na maisha ya dunia, na hakuna ajuaye hakika kamili ya maisha haya na namna yalivyo isipokuwa Mwenyezi MUNGU pekee.

Jiandae na maisha ya barzakh ambayo hayana salama ila kwa wacha-Mungu

View attachment 2140430
Hii ni sayansi au masimulizi tu ya alpha lela ulela?
 
Faidika na Darsa la FaizaFoxy...

Unachanganya mambo sana usiyoyaelewa.

1) Kufa sio kuwa "Barzakh" kama unavyotaka kutuaminisha. Neno Kifo kwa lugha ya Kiarabu ni full stop. Kama unajua kidogo kusoma Kiarabu, hata vibao au saini zao za barabarani kwa Kiarabu zinaandikwa "Kif", kwa maana "stop". Kiswahili ndio tunakazia na kusema "Kifo".

2) Barzakh ni kizuizi "berrier", kwa maana wa uhai hayupo kwenye umauti na wa umauti hayupo kwenye uhai. Kati yetu ni hicho kizuizi (barzakh".

3) Umauti ni hali "state" nyingine ya kutokua hapa kwenye uhai, kuwepo kwenye umauti. Mfano tu, ni kama hali ya kuwa macho (conscious inatawala) na kuwa usingizini (subconscious inatawala). Tofauti ni kuwa upo hai hata ukilala.

Binafsi siamini katika adhabu za kaburi. Kwanza kwa kuwa hazijatajwa kwenye Qur'an, sijaziona. Pili Hadith iliyozitaja siikubali.

Ikiwa kuna adhabu ya kaburini basi Allah itakuwa "katudanganya" (AstaghafiruAllah) anaposema kwenye Qur'an kuwa kuna siku ya kiama (Kusimamishwa) kuhukumiwa? Sasa iweje tena tuhukumiwe kabla ya Kiama?

Naamini kuwa tunapotoka kwenye uhai kuingia kwenye umauti na hadi siku ya Kiama hakutakuwa na feeling za muda kama vile tupo hai. Itakua ni mano wa watu wa Pangoni, kisa cha kwenye Qur'an) au alielala miaka 10 kisa cha Qur'an).

Kifo, kinachokufa ni hiki kiwiliwili (body) chetu, nafsi haifi bali inaingia kweye umauti. Qur'an inahakikisha hili kwa kutukumbusha kuwa "kila nafsi itauonja umauti".

Hata sehemu tu ya kiwiliwili inaweza kufa na nafsi bado haijaingia kwenye umauti. Mfano ukikatika mkono au mguu, unakuwa umekufa huo mkono au mguu lakini nafsi bado haijaonja umauti.
Asante kwa darasa, japo ni mwamini wa upande wa pili wenu lakini nimekuelewa mno.
 
Mosi bandiko haliko jukwaa sahihi.

Pili kuna aliyewahi kushuhudia hizo adhabu atuthibitishie?
 
Kifo sio fulustop bali ni alama ya comma,rejea kufa na kufufuka kwa Bwana Yesu na akatuambia anakwenda kwa Baba kututengenezea makao,

Rejea maneno ya Bwana Yesu,Nitalivunha hekalu na kulijenga kwa siku tatu yaani atakufa na kufufuka siku ya tatu.

Rejea kupaa kwa Eliya alipochukuliwa na Kigali cha moto na kuondoka nae,

Rejea kupalizwa mbinguni kwa Bikira Maria,

NB:Yote yanathibitisha kuwepo kuwa kifo sio mwisho Ila kuna maisha mengine baada ya kifo.

Nina shuhuda mbili:

1.Niliona wingu likishuka mahali fulani na lilipoondoka mahali hapo mtu alikufa,wingu lilikuja kumchukua,huo ni ukaribisho mwema kwenda kwenye maisha mengine.

2.Naliona Malaika wakitua mfano wa radi,radi ilipiga na ilipotua chini mfano wa Malaika alitokea,na mahali hapo alikuwa anatarajiwa kupita mtu fulani na alipopita baadae alikufa,Malaika wale walikuja kumchukua.

Sasa maisha baada ya kifo,kwa watu wema unaenda Paradiso,sehemu kama iliyokuwa bustani ya Eden utaendelea na maisha hadi Bwana Yesu atakapowachukua kuwarudisha tena duniani kutawala nae kwa miaka 1000 na baada ya miaka 1000 kuisha utashuka mji mpya wa Jerusalem na hukumu itapita na wale wema wataingia Jerusalem kuishi milele.

Kwa watu waovu wakifa watasubiri kwenye udongo hadi siku ya hukumu na kuhukumiwa kuingia Jehanamu.
Huko kuona uliona ukiwa umelala au uliona live mkuu

Huo mji wa yerusalem ni yerusalem hii hii tulio nayo ambayo haipo hata kwenye miji 10 bora duniani? Hii ambayo kwa sehemu ni bora hata mji wa dar es laam?
 
Back
Top Bottom