Al-Barzakh: Haya ndio Maisha ya Kaburini baada ya kufa

Kufa ni nini? Kufa ni hali ya roho kuepukana na kiwiliwili, au kufa ni kukatika matumizi ya roho kwa kiwiliwili na kukosa kiwiliwili ambayo ndio ala yake na kumuepusha mtu na mali yake na watoto wake na mke wake.

Kufa kunakata utamu wa maisha ya kiulimwengu na kwenda ulimwengu mwingine. Mtu ambaye alikuwa akifurahia maisha ya ulimwengu kwa kufanya ufedhuli amepata khasara baada ya kufa.

Na yule ambaye alikuwa akifurahi kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu basi atapata neema kubwa na inakamilika kufaulu kwake.

Watu wengi hudhania ya kwamba mtu anapokufa na akazikwa amemaliza kila kitu na amepumzika na ulimwengu, wala halimjii yeye jambo lolote.
Kudhani hivyo ni kosa kubwa bali hakika mwanadamu baada ya kufa kwake anaingia katika maisha mapya, maisha ya barzakh na kutoka maisha ya barzakh huenda kwenye maisha ya akhera ambayo ndiyo maisha ya mwisho na ya milele.

View attachment 2140429

Bar-zakh ni maisha ya baadaye; maisha baada ya haya tuliyonayo hivi sasa hapa duniani.

Maisha hayo kuanzia mtu anapokufa huitwa ni ‘Maisha Ya Barzakh’.
Barzakh ni kipindi baina ya wakati wa mauti na Qiyaamah. Na kila maiti atapitia katika maisha hayo, awe Muislam au Mkristo au asiye na dini, awe mwema au mwovu, na katika kipindi hicho kunakuwa na fitna na mitihani ya kaburi ambako mtu anajiwa na Malaika wawili na kuhojiwa na kisha hufuatia neema au adhabu za kaburini. Inajulikana kuwa kuna makazi matatu; makazi ya Dunia (Daarud-duniya), makazi ya Barzakh (Daarul-Barzakh) na makazi ya kudumu (Daarul-Qaraar).

Maisha ya kaburini ni kile kipindi anachokaa mtu baada ya kufa kwake mpaka kufufuliwa kwake. Kipindi kati ya parapanda la kwanza ambalo ni amri ya kufa viumbe vyote na parapanda la pili ambalo ni amri ya kufufuliwa viumbe vyote vitakavyotakiwa vifufuke, Huitwa Barzakh.

Katika kipindi hichi cha maisha ya dunia ni mambo gani yanayoendelea katika nafsi ya mwenye kufa? Wengi kwa kujiliwaza katika wakati huo hufikiria kuwa watu wakifa wanakuwa mapumzikoni. Na watu ambao hawaamini siku ya mwisho huamini kuwa kifo ndio mwisho wa maisha ya watu na iliyobaki ni kuoza na kuwa chumvi chumvi zitakazotumika ardhini.

Katika kipindi cha Barzakh roho za watu wema zitakaa pahali pazuri kungojea malipo yao ya Peponi, Ama zile za watu waovu zitakuwa mahabusu zikingojea siku ya hukumu yao. Ama kuhusu mtu muovu yeye atakaa katika kaburi lake kwa khofu na fadhaa.

Maisha ya Barzakh ni maisha yanayotofautiana kabisa na maisha ya dunia, na hakuna ajuaye hakika kamili ya maisha haya na namna yalivyo isipokuwa Mwenyezi MUNGU pekee.

Jiandae na maisha ya barzakh ambayo hayana salama ila kwa wacha-Mungu

View attachment 2140430
Kwahiyo ni Bora kuliwa na Simba au kumezwa na mamba?
 
unamaanisha kama hadithi inaongelea jambo ambalo halipo kwenye quran huikubali? tupe mfano wa hadithi inayokwenda tofauti na quran.
Sikusema "jambo ambalo halipo kwenye Qur'an". Umeyatoa wapi maneno hayo? nimeandika wazi kabisa juu hapo, inayopingana na Qur'an.

Mfano si hiyo hadith ya adhabu ya kaburi, hujanissoma nini juu huko? Umekurupuka?
 
Sikusema "jambo ambalo halipo kwenye Qur'an". Umeyatoa wapi maneno hayo? nimeandika wazi kabisa juu hapo, inayopingana na Qur'an.

Mfano si hiyo hadith ya adhabu ya kaburi, hujanissoma nini juu huko? Umekurupuka
kwa kuikataa hadithi huoni kama unapingana na qurani yenyewe? kwa maana hadithi ni maneno ya mtume rehma na amani ziwe juu yake.
 
Endeleeni kujifariji na hadaa za ulimwengu mkifikiri hakuna source ya maisha.

Nani alikuwa na uhakika wa kuzaliwa? Kwani binadamu wa kwanza alitoka wapi?
Utabishaje na utaachaje kuamini vitabu vitakatifu kuhusu miongozo mbali mbali wakati hip sayansi imevikuta. Vitabu?

Ni pumzi tu ndio inatuzubaisha. Hakuna ajuaye dakika moja mbele nini kitamtokea.

Maisha ya mwanadamu yote in siri. Mitume ilipewa miongozo ili kujua Muumba anataka nini. Kila kitu kimeelezwa.
Endeleeni kubisha
Mkuu na wewe unaamini kwenye hizi dini za waarabu na Wazungu? Ambapo hakuna mtume au nabii mweusi.
 
Acha usanii wako wewe, kaburini hakuna maisha, mwili unaoza fahamu zinaondoka unakuwa sawa na mtu aliyelala usingizi "fo fo fo"

Kama unalalaga fo fo fo ukiwa hujitqmbui na unaamka basi jua hata ukifa utaamka hivyo hivyo

Kifo ni fumbo nq mfano wake ni usingizi unaopitia maisha yako ya kila siku

SOMO KUBWA HAPA LA IMANI
 
Kufa ni nini? Kufa ni hali ya roho kuepukana na kiwiliwili, au kufa ni kukatika matumizi ya roho kwa kiwiliwili na kukosa kiwiliwili ambayo ndio ala yake na kumuepusha mtu na mali yake na watoto wake na mke wake.

Kufa kunakata utamu wa maisha ya kiulimwengu na kwenda ulimwengu mwingine. Mtu ambaye alikuwa akifurahia maisha ya ulimwengu kwa kufanya ufedhuli amepata khasara baada ya kufa.

Na yule ambaye alikuwa akifurahi kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu basi atapata neema kubwa na inakamilika kufaulu kwake.

Watu wengi hudhania ya kwamba mtu anapokufa na akazikwa amemaliza kila kitu na amepumzika na ulimwengu, wala halimjii yeye jambo lolote.
Kudhani hivyo ni kosa kubwa bali hakika mwanadamu baada ya kufa kwake anaingia katika maisha mapya, maisha ya barzakh na kutoka maisha ya barzakh huenda kwenye maisha ya akhera ambayo ndiyo maisha ya mwisho na ya milele.

View attachment 2140429

Bar-zakh ni maisha ya baadaye; maisha baada ya haya tuliyonayo hivi sasa hapa duniani.

Maisha hayo kuanzia mtu anapokufa huitwa ni ‘Maisha Ya Barzakh’.
Barzakh ni kipindi baina ya wakati wa mauti na Qiyaamah. Na kila maiti atapitia katika maisha hayo, awe Muislam au Mkristo au asiye na dini, awe mwema au mwovu, na katika kipindi hicho kunakuwa na fitna na mitihani ya kaburi ambako mtu anajiwa na Malaika wawili na kuhojiwa na kisha hufuatia neema au adhabu za kaburini. Inajulikana kuwa kuna makazi matatu; makazi ya Dunia (Daarud-duniya), makazi ya Barzakh (Daarul-Barzakh) na makazi ya kudumu (Daarul-Qaraar).

Maisha ya kaburini ni kile kipindi anachokaa mtu baada ya kufa kwake mpaka kufufuliwa kwake. Kipindi kati ya parapanda la kwanza ambalo ni amri ya kufa viumbe vyote na parapanda la pili ambalo ni amri ya kufufuliwa viumbe vyote vitakavyotakiwa vifufuke, Huitwa Barzakh.

Katika kipindi hichi cha maisha ya dunia ni mambo gani yanayoendelea katika nafsi ya mwenye kufa? Wengi kwa kujiliwaza katika wakati huo hufikiria kuwa watu wakifa wanakuwa mapumzikoni. Na watu ambao hawaamini siku ya mwisho huamini kuwa kifo ndio mwisho wa maisha ya watu na iliyobaki ni kuoza na kuwa chumvi chumvi zitakazotumika ardhini.

Katika kipindi cha Barzakh roho za watu wema zitakaa pahali pazuri kungojea malipo yao ya Peponi, Ama zile za watu waovu zitakuwa mahabusu zikingojea siku ya hukumu yao. Ama kuhusu mtu muovu yeye atakaa katika kaburi lake kwa khofu na fadhaa.

Maisha ya Barzakh ni maisha yanayotofautiana kabisa na maisha ya dunia, na hakuna ajuaye hakika kamili ya maisha haya na namna yalivyo isipokuwa Mwenyezi MUNGU pekee.

Jiandae na maisha ya barzakh ambayo hayana salama ila kwa wacha-Mungu

View attachment 2140430

Kitabu cha biblia takatifu kimeelezea tofauti na mtazamo huu.
Maandiko yanasema
Baada ya kufa binadamu anarudi mavumbini alikotoka na roho (pumzi ya uhai) inarudi kwa Mungu.
Mhubiri : 12 : 7 - Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.
 
Hakuna ushahidi wa kisayansi wa maisha baada ya kifo, lakini imani ya maisha ya baada ya kifo ina nguvu kati ya watu wa kidini na pia baadhi ya watu wasio wa kidini. Sayansi yenyewe inafika hatua haina majibu kwasababu kuna watu wanafukuliwa na wanakutwa miili yao haijaoza na ilihali walizikwa karne zilizo pita.

MUNGU kwakuwa amekupa muongozo wa akili ni sawa na mwanafunzi anayepatiwa kitabu asome lakini hana uhakika kama mmtihani utakuwepo au hautakuwepo, mwenye uhakika wa hilo ni mwalimu pekee, na mtihani pia umewekwa kuwa siri ili wewe uitumikishe akili yako

Mfano wako ni Akili za kitoto
 
Acha usanii wako wewe, kaburini hakuna maisha, mwili unaoza fahamu zinaondoka unakuwa sawa na mtu aliyelala usingizi "fo fo fo"
Usingizi katika mwili uliooza au sio!!??
Kubabaika huku ni dhahiri unajua kuna maisha baada ya kufa!
La msingi umejiandaaje katika usingizi wako katika mwili uliooza???
 
Faidika na Darsa la FaizaFoxy...

Unachanganya mambo sana usiyoyaelewa.

1) Kufa sio kuwa "Barzakh" kama unavyotaka kutuaminisha. Neno Kifo kwa lugha ya Kiarabu ni full stop. Kama unajua kidogo kusoma Kiarabu, hata vibao au saini zao za barabarani kwa Kiarabu zinaandikwa "Kif", kwa maana "stop". Kiswahili ndio tunakazia na kusema "Kifo".

2) Barzakh ni kizuizi "barrier", kwa maana wa uhai hayupo kwenye umauti na wa umauti hayupo kwenye uhai. Kati yetu ni hicho kizuizi (barzakh".

3) Umauti ni hali "state" nyingine ya kutokua hapa kwenye uhai, kuwepo kwenye umauti. Mfano tu, ni kama hali ya kuwa macho (conscious inatawala) na kuwa usingizini (subconscious inatawala). Tofauti ni kuwa upo hai hata ukilala.

Binafsi siamini katika adhabu za kaburi. Kwanza kwa kuwa hazijatajwa kwenye Qur'an, sijaziona. Pili Hadith iliyozitaja siikubali.

Ikiwa kuna adhabu ya kaburini basi Allah itakuwa "katudanganya" (AstaghafiruAllah) anaposema kwenye Qur'an kuwa kuna siku ya kiama (Kusimamishwa) kuhukumiwa? Sasa iweje tena tuhukumiwe kabla ya Kiama?

Naamini kuwa tunapotoka kwenye uhai kuingia kwenye umauti na hadi siku ya Kiama hakutakuwa na feeling za muda kama vile tupo hai. Itakua ni mano wa watu wa Pangoni, kisa cha kwenye Qur'an) au alielala miaka 100 kisa cha Qur'an).

Kifo, kinachokufa ni hiki kiwiliwili (body) chetu, nafsi haifi bali inaingia kweye umauti. Qur'an inahakikisha hili kwa kutukumbusha kuwa "kila nafsi itauonja umauti".

Hata sehemu tu ya kiwiliwili inaweza kufa na nafsi bado haijaingia kwenye umauti. Mfano ukikatika mkono au mguu, unakuwa umekufa huo mkono au mguu lakini nafsi bado haijaonja umauti.
Kumbe kwenye suala hadithi za imani yenu umechagua zipi za kuziamini?!vipi na wale bikra 72 wenye macho ya mviringo?
 
Faidika na Darsa la FaizaFoxy...

Unachanganya mambo sana usiyoyaelewa.

1) Kufa sio kuwa "Barzakh" kama unavyotaka kutuaminisha. Neno Kifo kwa lugha ya Kiarabu ni full stop. Kama unajua kidogo kusoma Kiarabu, hata vibao au saini zao za barabarani kwa Kiarabu zinaandikwa "Kif", kwa maana "stop". Kiswahili ndio tunakazia na kusema "Kifo".

2) Barzakh ni kizuizi "berrier", kwa maana wa uhai hayupo kwenye umauti na wa umauti hayupo kwenye uhai. Kati yetu ni hicho kizuizi (barzakh".

3) Umauti ni hali "state" nyingine ya kutokua hapa kwenye uhai, kuwepo kwenye umauti. Mfano tu, ni kama hali ya kuwa macho (conscious inatawala) na kuwa usingizini (subconscious inatawala. Tofauti ni kuwa upo hai hata ukilala.

Binafsi siamini katika adhabu za kaburi. Kwanza kwa kuwa hazijatajwa kwenye Qur'an, sijaziona. Pili Hadith iliyozitaja siikubali.

Ikiwa kuna adhabu ya kaburini basi Allah itakuwa katudanya (AstaghafiruAllah) anaposema kwenye Qur'an kuwa kuna siku ya kiama (Kusimamishwa) kuhukumiwa? Sasa iweje tena tuhukumiwe kabla ya Kiama?

Naamini kuwa tunapotoka kwenye uhai kuingia kwenye umauti na hadi siku ya Kiama hakutakuwa na feeling za muda kama vile tupo hai. Itakua ni mano wa watu wa Pangoni, kisa cha kwenye Qur'an) au alielala miaka 10 kisa cha Qur'an).

Kifo, kinachokufa ni hiki kiwiliwili (body) chetu, nafsi haifi bali inaingia kweye umauti. Qur'an inahakikisha hili kwa kutukumbusha kuwa "kila nafsi itauonja umauti".

Hata sehemu tu ya kiwiliwili inaweza kufa na nafsi bado haijaingia kwenye umauti. Mfano ukikatika mkono au mguu, unakuwa umekufa huo mkono au mguu lakini nafsi bado haijaonja umauti.

Pedagogic at Heart
Kwa hiyo hata sharia ni batiri sio maana kuna kiama!
 
There is no next life when you dead is over, what left is memory of the people shared with you and some time they mind create a 3D picture and think the dead is awake to greet or punish for those who believe
 
Back
Top Bottom