Kuzini na nduguyo wa damu ndio uthibitisho wa kutomuamini Mungu? Kama ndivyo unavyoamini, ni akili ndogo sana hii.
Hizi nyingine ni taratibu za kibinadamu tulizorithi kupitia maandiko ya enzi, ndio maana hata kwenye dini, imani yetu kuu (Mungu) ni moja ijapokuwa namna, kanuni na miongozo ya kuabudu hutofautiana kulingana na taasisi (dini) tulizochagua ama kuchaguliwa kuzifuata ili kumjua Mungu.
Mimi binafsi, daima ninaamini kuna watu wa namna mbili:
1. Spiritual person: huyu anaamini katika nafsi, roho na kweli yake inayomuunganisha na nguvu anayoamini ni kuu katika tawala zote za ulimwengu na mbinguni (Mungu/miungu)
2. Religious person: yeye hujikita katika kuzingatia misingi, kanuni na taratibu za njia yake ya imani (dini/dhehebu).
Ikae kichwani hiyo.