Quran 75:
(
1) Ninaapa kwa Siku ya Kiyama!
Ninaapa na natilia mkazo kiapo hichi kwa Siku ya Kiyama, na hiyo ni kweli iliyo thibiti;
(
2) Na ninaapa kwa nafsi inayo jilaumu!
Na ninaapa na natilia mkazo kiapo hichi kwa nafsi inayo mlaumu mtu kwa dhambi zake na upungufu wake, ya kwamba bila ya shaka yoyote mtafufuliwa baada ya kukusanywa mafupa yenu yaliyo tawanyika.
(
3) Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake?
Hivyo mtu anadhani baada ya kuwa Sisi tulimuumba naye hakuwa kitu chochote, tutakuja shindwa kuyakusanya mafupa yake yaliyooza na yakatapanyika?
(
4) Kwani! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake!
Hasha! Sisi tuna uweza wa kuviweka sawa hata vifupa vya vidole vyake vilivyo vurugika, wachilia mbali mafupa yake makubwa makubwa ya mwili wake.
(
5) Lakini mtu anataka tu kuendelea na maasi kwa siku zilioko mbele yake.
Hivyo mtu anakanya kufufuliwa? Anataka abakie katika uasi wake katika siku zote zilizo mbakilia katika umri wake ulio salia?
(
6) Anauliza: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama?
Anauliza kwa kuona haiwezi kutokea saa ya Kiyama: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama?
(
7) Basi jicho litapo dawaa!
Jicho litapo tahayari kwa kufazaika na kushtuka,
(
8) Na mwezi utapo patwa!
Na mwangaza wa mwezi ukapotea,
(
9) Na likakusanywa jua na mwezi!
Na jua likakusanyika na mwezi kuchomoza magharibi,
(
10) Siku hiyo mtu atasema: Yako wapi makimbilio?
Mtu hapo atasema: Yako wapi makimbilio kuikimbia hii adhabu?
(
11) La! Hapana pa kukimbilia!
Huachi, ewe mtu, kutafuta makimbilio? Leo huna pa kukimbilia wewe,
(
12) Siku hiyo pa kutua ni kwa Mola wako Mlezi tu.
ila kwa Mola wako Mlezi peke yake, ndipo penye matulivu ya waja, Peponi au Motoni.
(
13) Siku hiyo ataambiwa aliyo yatanguliza na aliyo yaakhirisha.
Siku hiyo mtu ataambiwa vitendo vyake alivyo vitanguliza na alivyo viakhirisha.
(
14) Bali mtu ni hoja juu ya nafsi yake.
Bali mtu yeye mwenyewe ni hoja iliyo wazi juu ya nafsi yake inayo mkazania kwa anayo yatenda na anayo yaacha.
(
15) Na ingawa atatoa chungu ya udhuru.
Na ijapo kuwa atajitolea chungu nzima ya udhuru na akazieneza, hawezi kabisa kuepukana na hoja hizo