Wewe ni Nafs yenye kiwiliwili, Nafs huitwa roho (spirit) pia.
Nafs inabeba himaya yako ya mwili na ya kiroho. Unachoona, unachosikia, unachofanya, unachonusa, unachoonja. Vyote hivyo vinabaki kwenye himaya (arsh) ya Nafs yako. Na nafs zinazokuwa kwenye kiwiliwili chako ni tatu tofauti (soma kuhusu Qareen), moja ni yako mahsusi na moja ni ile ya kishetani na moja ni ile ya mema. Hizi mbili daima zinaishawishi nafs yako, moja kutenda mema, moja kutenda ya kishetani. Wale wenye self control ndio huishinda nafs ya kishetani, inaposalim amri na kuwa njema basi hapo umevuka darja la majaribio ya Shetani na unakuwa mtu mwema sana.
Ukiisoma Qur'an kwa kina inaelezea hayo, pia kuna Hadith ya Mtume Muhammad Salla Allahu Alayhi Wasalaam imeeelea Qareen, alielezea kuhusu Qareen wake kuwa amesilim.
Kuna bwege mmoja aliulizia hapo juu, aliisoma aya, akona kuna "wawili wametajwa" akauliza "hao wawili ni nani", haielewi Qur'am na haelewi kuhusu Qareen, nikaona ni poyoyo hata nikimuelezea hatoelewa kwa kuwa Hamuamini Allah, Haiamini Qur'an na hamuamini wala kumjuwa Mtume Muhammad salaa Allahu alayhi Wasalaam ni nani. Anafikiri alikuja kwa ajili ya Waislaam tu, haelewi kuwa Mtume Muhammad ni Rahma kwa walimwengu wote. Na yeye akiwemo, angemsoma tu amuelewe, angempenda akitaka asitake.
2) Mimi sio hao. Mimi Naamini Qur'an, naamini na Hadith zile ambazo hazipingani na Qur'an. Siiamini kila inayoitwa "hadith" kuwa ni ya kweli, kwa kuwa zingine ni uzushi tu.