Kifo sio fulustop bali ni alama ya comma,rejea kufa na kufufuka kwa Bwana Yesu na akatuambia anakwenda kwa Baba kututengenezea makao,
Rejea maneno ya Bwana Yesu,Nitalivunha hekalu na kulijenga kwa siku tatu yaani atakufa na kufufuka siku ya tatu.
Rejea kupaa kwa Eliya alipochukuliwa na Kigali cha moto na kuondoka nae,
Rejea kupalizwa mbinguni kwa Bikira Maria,
NB:Yote yanathibitisha kuwepo kuwa kifo sio mwisho Ila kuna maisha mengine baada ya kifo.
Nina shuhuda mbili:
1.Niliona wingu likishuka mahali fulani na lilipoondoka mahali hapo mtu alikufa,wingu lilikuja kumchukua,huo ni ukaribisho mwema kwenda kwenye maisha mengine.
2.Naliona Malaika wakitua mfano wa radi,radi ilipiga na ilipotua chini mfano wa Malaika alitokea,na mahali hapo alikuwa anatarajiwa kupita mtu fulani na alipopita baadae alikufa,Malaika wale walikuja kumchukua.
Sasa maisha baada ya kifo,kwa watu wema unaenda Paradiso,sehemu kama iliyokuwa bustani ya Eden utaendelea na maisha hadi Bwana Yesu atakapowachukua kuwarudisha tena duniani kutawala nae kwa miaka 1000 na baada ya miaka 1000 kuisha utashuka mji mpya wa Jerusalem na hukumu itapita na wale wema wataingia Jerusalem kuishi milele.
Kwa watu waovu wakifa watasubiri kwenye udongo hadi siku ya hukumu na kuhukumiwa kuingia Jehanamu.