Al-Barzakh: Haya ndio Maisha ya Kaburini baada ya kufa

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ushirikina haumsumbui mtu ambae anaamini kwamba kuna mungu mmoja bali ni kwa yule anayemfanya huyo mungu ana waungu wengine au kuwafanya viumbe wa Allah kuwa ni waungu..ni suala la mda tu cku ukija kuona yakini kwenye jicho lako utakuja uyakumbuke haya kwamba ilikua mtu aloakikuambia alikufa akafufuka au ni ya kweli..
Allah akuongoze
 
Kwani wakati upo tumboni mwa mama yako ulijua Nini kinaendelea?
ebu tuambie Kama ulikuwa unajua upo wapi.
Mi nilifkr kuna mtu ametoka kuzimu ili kutupa mchongo of what is going on huko down , kumbe story tuuu....!!

Muwe mnaenda straight to the poit
 
Kufa nini?. Kufa ni kurudi katika hali ya kuto kuwepo.
 
1---Anga inayoizunguka dunia.
2---paradise (the ultimate abode of justice).

Yesu Yupo kwenye ipi hapo??
Mbingu ya tatu. Anatuandalia mbingu na nchi mpya!

2 Wakorintho 12:2
"Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu"

Yohana 14:1-25
"Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi muwepo. Nami niendako mwaijua njia. Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi tunaijuaje njia? Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi..."

Yesu ndiye njia ya kumwona Mungu. Bahati mbaya hakuna njia nyingine kwa sababu hakuna mwingine aliyelipa adhabu ambayo wanadamu wanapaswa kuilipa kwa kuvunja amri za Mungu. Dini haitakuwa na msaada utakaposimama mbele za Mungu kutoa hesabu ya maisha yako. Vivyo hivyo na mimi na kila mwanadamu!

Ufunuo 20:12
"Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao."
 
Huenda sikujieleza ndivyo. Ila ni kwamba katika maandalizi ya safari ya mwisho, tunatakiwa tuwaaandae vizuri na manukato pia sababu huwa wanatembeleana.

Umepata wapi kwamba huwa wanatembeleana??!!
 
Mbingu ya tatu. Anatuandalia mbingu na nchi mpya!

2 Wakorintho 12:2
"Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu"

Yohana 14:1-25
"Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi muwepo. Nami niendako mwaijua njia. Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi tunaijuaje njia? Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi..."

Yesu ndiye njia ya kumwona Mungu. Bahati mbaya hakuna njia nyingine kwa sababu hakuna mwingine aliyelipa adhabu ambayo wanadamu wanapaswa kuilipa kwa kuvunja amri za Mungu. Dini haitakuwa na msaada utakaposimama mbele za Mungu kutoa hesabu ya maisha yako. Vivyo hivyo na mimi na kila mwanadamu!

Ufunuo 20:12
"Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao."

Inaonekana huwa unasoma Biblia bila kutafakari kilichoandikwa.

2 wakorintho 12:2 haisemi kwamba mtu aliyenyakuliwa kwenda mbingu ya 3 ni Yesu, anasema; "Namjua mtu mmoja KATIKA kristo---", sasa hapo Yesu anaingiaje??.

Yohana 14:1-25, Hapa Yesu anajitangaza kwa wanafunzi wake kwamba yeye ndio njia ya ukweli na uzima na mtu haendi kwa Baba (Mungu) bila kupitia yeye Yesu, maana yake ni hii; mafundisho ya Yesu kama wanafunzi wake wangeyashika basi mioyoni mwao itaingia imani ya Mungu na hivyo watafika "mbinguni" kwa Mungu kiimani na roho zao zitakuwa salama, sio kwamba kupitia njia ya Yesu hao wanafunzi watanyakuliwa mbinguni kimwili kama jinsi inavyoaminika kimakosa kwamba Yesu alipaa kimwili katika mbingu kimwili ya tatu. Fundisho hilo la Yesu kwa njia moja au nyingine limefundishwa na takriban manabii wote waliotumwa na Mungu.

Ufunuo 20:12---- hii aya inaungana na Mathayo 19:28 ikisema kwamba Yesu atakaa katika kiti cha enzi akiyahukumu makabila 12 ya wana waIsraeli tu na sio makabila ya watu wengine, Mnyamwezi na Mmanyema nk hatumo humo hivyo Yesu sio wa kwetu bali ni wa Waisraeli.
 
2 wakorintho 12:2 haisemi kwamba mtu aliyenyakuliwa kwenda mbingu ya 3 ni Yesu, anasema; "Namjua mtu mmoja KATIKA kristo---", sasa hapo Yesu anaingiaje??.
Si uliuliza Yesu yuko mbingu ipi nika kwambia alipo na hayo maandiko nimekupa kuonyesha mbingu ya tatu zio utunzi wangu. Ni wapi nimesema aliyekwenda mbingu ya tatu ni Yesu?
 
Yohana 14:1-25, Hapa Yesu anajitangaza kwa wanafunzi wake kwamba yeye ndio njia ya ukweli na uzima na mtu haendi kwa Baba (Mungu) bila kupitia yeye Yesu,
Ndio ukweli wenyewe!

maana yake ni hii; mafundisho ya Yesu kama wanafunzi wake wangeyashika basi mioyoni mwao itaingia imani ya Mungu na hivyo watafika "mbinguni" kwa Mungu kiimani na roho zao zitakuwa salama,
Haya ni maelezo yako ya kutunga mwenyewe. Ukitaka kujua alichomaanisha soma mistari kabla na mazungumzo yaliyofuata.

Yohana 14
"1 Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. 2Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. 3Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo"

Yesu anawaandaliaje makao ya kiroho? Na anawakaribishaje kiroho? Unahitaji kuwa mpindishaji maneno wa kiwango cha PhD kusema Yesu alimaanisha anawaandalia makao kiroho na atakuja awakaribishe kiroho. Kwa maneno ya Yesu na mitume wake ni wazi mbinguni ni mahali na sio "mbinguni" kama unavyotaka tuamini.

Mbinguni ni mahali, na Yesu anaandaa makao na atakuja kutuchukua na Biblia ina maelezo ya kutosha kuhusu haya yote. Unless huijui Biblia huwezi kusema unayoyasema!

Pili maneno yako Mungu kwenye mabano yanataka kumaanisha Yesu ni mwanadamu na pengine nabii tu. Mistari inayofuata inakataa nadharia hii.

Yohana 14
"Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha. 9Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba? 10Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu?"

Kwamba ukimwona Yesu umemwona Baba. Na kuwa Baba na Yesu ni umoja kiasi kwamba ukimwona Yesu badi umemwona Baba kwa sababu Yesu yupo ndani ya Baba na Baba ndani ya Yesu!

Mfano dhaifu lakini unaotoa mwanga ni fikiria bilauri mbili. Halfu bilauri ya kwanza ipo ndani ya nyingine na ya pili ipo ndani ya ya kwanza. Haiwezekani ispokuwa kama tunaongelea bilauri ambayo ni moja japo ni mbili. Narudia tena ni mfano dhaifu lakini unatoa mwanga kuwa anachosema Yesu na kile unataka tuamini ni tofauti!

Mwisho usisahau swali lako lilikuwa Yesu yuko wapi ili akwambie kuhusu kufa na kufufuka. Sasa wajua kuwa aliacha maneno yake. Yafuate hayo nawe utaishi. Yesu pekee ndiye njia na uzima. Ukimwamini, ujapokufa utaishi na hutakuwa na sababu ya kutahayari siku ya hasira ijapofika!
 
Si uliuliza Yesu yuko mbingu ipi nika kwambia alipo na hayo maandiko nimekupa kuonyesha mbingu ya tatu zio utunzi wangu. Ni wapi nimesema aliyekwenda mbingu ya tatu ni Yesu?

"Namjua mtu katika kristo"--- maneno hayo yanamaanisha kuna mtu na yupo kristo ambaye ndanimo yupo huyo mtu aliyekuwepo kwenye mbingu ya 3.

Swali ni hili; Yesu (kristo) yupo kwenye mbingu gani??
 
Ndio ukweli wenyewe!

Haya ni maelezo yako ya kutunga mwenyewe. Ukitaka kujua alichomaanisha soma mistari kabla na mazungumzo yaliyofuata.

Yohana 14
"1 Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. 2Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. 3Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo"

Yesu anawaandaliaje makao ya kiroho? Na anawakaribishaje kiroho? Unahitaji kuwa mpindishaji maneno wa kiwango cha PhD kusema Yesu alimaanisha anawaandalia makao kiroho na atakuja awakaribishe kiroho. Kwa maneno ya Yesu na mitume wake ni wazi mbinguni ni mahali na sio "mbinguni" kama unavyotaka tuamini.

Mbinguni ni mahali, na Yesu anaandaa makao na atakuja kutuchukua na Biblia ina maelezo ya kutosha kuhusu haya yote. Unless huijui Biblia huwezi kusema unayoyasema!

Pili maneno yako Mungu kwenye mabano yanataka kumaanisha Yesu ni mwanadamu na pengine nabii tu. Mistari inayofuata inakataa nadharia hii.

Yohana 14
"Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha. 9Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba? 10Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu?"

Kwamba ukimwona Yesu umemwona Baba. Na kuwa Baba na Yesu ni umoja kiasi kwamba ukimwona Yesu badi umemwona Baba kwa sababu Yesu yupo ndani ya Baba na Baba ndani ya Yesu!

Mfano dhaifu lakini unaotoa mwanga ni fikiria bilauri mbili. Halfu bilauri ya kwanza ipo ndani ya nyingine na ya pili ipo ndani ya ya kwanza. Haiwezekani ispokuwa kama tunaongelea bilauri ambayo ni moja japo ni mbili. Narudia tena ni mfano dhaifu lakini unatoa mwanga kuwa anachosema Yesu na kile unataka tuamini ni tofauti!

Mwisho usisahau swali lako lilikuwa Yesu yuko wapi ili akwambie kuhusu kufa na kufufuka. Sasa wajua kuwa aliacha maneno yake. Yafuate hayo nawe utaishi. Yesu pekee ndiye njia na uzima. Ukimwamini, ujapokufa utaishi na hutakuwa na sababu ya kutahayari siku ya hasira ijapofika!

Kama hujui Yesu alikuwa ni mtaalamu wa kauli za mafumbo kama utasoma maandiko ya Yesu literally lazima utapotea sana, Wewe unataka tuamini Yesu ni Mungu wakati unasahau kabisa kwamba akiwa msalabani akiugulia kwa uchungu wa mateso aliyopewa na "viumbe wake" (kutokana na imani yako kwamba Yesu ni Mungu), alilia kwa uchungu; Eloi Eloi lamasabatchtan, Yaani Ewe Mungu, ewe Mungu mbona waniacha!!, sasa hapo kama Yeye ni Mungu na huyo Eloi ni nani??!!

Manabii wote ni njia ya ukweli na uzima na watu hawaendi kwa Mungu isipokuwa kwa kushika njia za nanabii, njia maana yake ni mafundisho ya kweli ya kumjua Mungu na uzima ni uzima wa roho, mafundisho ya Yesu ndio injili na anaposema Baba yumo ndani yake na yeye yumo ndani ya Baba na mtu aliyemuona yeye kamuona baba maana yake ni hiyo hiyo ya kimfano (metaphorical) na si vinginevyo kwa maneno mengine Yesu alikuwa ni Muwakilishi wa Mungu hivyo watu kwa kumfuata Yesu ni sawa na kumfuata Mungu lakini Yesu ni Yesu na Mungu ni Mungu.

Sehemu kadhaa ndani Biblia Yesu anakiri katumwa na Mungu kwa wana wa israeli hivyo yeye ni mtume wa Mungu na sio zaidi ya hapo.

Mungu gani kazaliwa na mtu, kanyonyeshwa na mtu, katahiriwa, katoroshwa ili asiuawe na mfalme Herode, je Herode ana nguvu kuliko huyo Mungu??, Mungu anateswa msalabani kama jambazi!!, anahisi njaa, anajaribiwa na shetani, anakesha kwa kusujudu akilia kumuomba "Mungu mwingine" amuepushe na kikombe cha mauti ya msalabani, anafunga saumu kwa siku 40, Mungu anasalitiwa, Mungu hajui msimu wa matunda na anaulaani mti bila sababu!!,---- huyo ni mtu na kamwe hawezi kuwa Mungu mtu mwenye sifa dhaifu za kibinadamu, na ndio maana jina lake jingine ni Mwana wa Adamu kumaanisha ni mtu.
 
Kufa ni nini? Kufa ni hali ya roho kuepukana na kiwiliwili, au kufa ni kukatika matumizi ya roho kwa kiwiliwili na kukosa kiwiliwili ambayo ndio ala yake na kumuepusha mtu na mali yake na watoto wake na mke wake.

Kufa kunakata utamu wa maisha ya kiulimwengu na kwenda ulimwengu mwingine. Mtu ambaye alikuwa akifurahia maisha ya ulimwengu kwa kufanya ufedhuli amepata khasara baada ya kufa.

Na yule ambaye alikuwa akifurahi kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu basi atapata neema kubwa na inakamilika kufaulu kwake.

Watu wengi hudhania ya kwamba mtu anapokufa na akazikwa amemaliza kila kitu na amepumzika na ulimwengu, wala halimjii yeye jambo lolote.

Kudhani hivyo ni kosa kubwa bali hakika mwanadamu baada ya kufa kwake anaingia katika maisha mapya, maisha ya barzakh na kutoka maisha ya barzakh huenda kwenye maisha ya akhera ambayo ndiyo maisha ya mwisho na ya milele.

View attachment 2140429

Bar-zakh ni maisha ya baadaye; maisha baada ya haya tuliyonayo hivi sasa hapa duniani.

Maisha hayo kuanzia mtu anapokufa huitwa ni ‘Maisha Ya Barzakh’.
Barzakh ni kipindi baina ya wakati wa mauti na Qiyaamah. Na kila maiti atapitia katika maisha hayo, awe Muislam au Mkristo au asiye na dini, awe mwema au mwovu, na katika kipindi hicho kunakuwa na fitna na mitihani ya kaburi ambako mtu anajiwa na Malaika wawili na kuhojiwa na kisha hufuatia neema au adhabu za kaburini.

Inajulikana kuwa kuna makazi matatu; makazi ya Dunia (Daarud-duniya), makazi ya Barzakh (Daarul-Barzakh) na makazi ya kudumu (Daarul-Qaraar).

Maisha ya kaburini ni kile kipindi anachokaa mtu baada ya kufa kwake mpaka kufufuliwa kwake. Kipindi kati ya parapanda la kwanza ambalo ni amri ya kufa viumbe vyote na parapanda la pili ambalo ni amri ya kufufuliwa viumbe vyote vitakavyotakiwa vifufuke, Huitwa Barzakh.

Katika kipindi hichi cha maisha ya dunia ni mambo gani yanayoendelea katika nafsi ya mwenye kufa? Wengi kwa kujiliwaza katika wakati huo hufikiria kuwa watu wakifa wanakuwa mapumzikoni.

Na watu ambao hawaamini siku ya mwisho huamini kuwa kifo ndio mwisho wa maisha ya watu na iliyobaki ni kuoza na kuwa chumvi chumvi zitakazotumika ardhini.

Katika kipindi cha Barzakh roho za watu wema zitakaa pahali pazuri kungojea malipo yao ya Peponi, Ama zile za watu waovu zitakuwa mahabusu zikingojea siku ya hukumu yao. Ama kuhusu mtu muovu yeye atakaa katika kaburi lake kwa khofu na fadhaa.

Maisha ya Barzakh ni maisha yanayotofautiana kabisa na maisha ya dunia, na hakuna ajuaye hakika kamili ya maisha haya na namna yalivyo isipokuwa Mwenyezi MUNGU pekee.

Jiandae na maisha ya barzakh ambayo hayana salama ila kwa wacha-Mungu

View attachment 2140430
Mbona mwanandani imechimbwa pembeni?
 
Aliishawahi kufa na kufufuka? Kuna watu waliowahi kufufuliwa na YESU lakini Biblia haijasema Lolote kuhusu habari za wafu,kwa hiyo hizo Ni folktales au myth busters
 
Porojo tupu. Imeandikwa "Roho ndio itiayo mwili uzima, mwili haufai kitu". Roho itamrudia yeye aliyeiumba na mwili utarudi udongoni ulipotoka.
 
Ndo unavyojidanganya hivo kama quran ina miaka 1500 na ukaidanganya nafsi yako pia..Hiyo quran inayoizungumzia ni maneno ya Allah na na nimuongozo ambao ameupangalia billions of years kabla ata wewe mwanadamu hujafikiriwa kuumbwa sio hio miaka 1500 unayosema ..hyo miaka elfu na miatano unayosema ndo ilipokamilika kuteremshwa tu..isome dini upate kuelewa,,
Allah akuongoze
hahaaaa kichwani umejaza ujinga
 
Faidika na Darsa la FaizaFoxy...

Unachanganya mambo sana usiyoyaelewa.

1) Kufa sio kuwa "Barzakh" kama unavyotaka kutuaminisha. Neno Kifo kwa lugha ya Kiarabu ni full stop. Kama unajua kidogo kusoma Kiarabu, hata vibao au saini zao za barabarani kwa Kiarabu zinaandikwa "Kif", kwa maana "stop". Kiswahili ndio tunakazia na kusema "Kifo".

2) Barzakh ni kizuizi "barrier", kwa maana wa uhai hayupo kwenye umauti na wa umauti hayupo kwenye uhai. Kati yetu ni hicho kizuizi (barzakh".

3) Umauti ni hali "state" nyingine ya kutokua hapa kwenye uhai, kuwepo kwenye umauti. Mfano tu, ni kama hali ya kuwa macho (conscious inatawala) na kuwa usingizini (subconscious inatawala). Tofauti ni kuwa upo hai hata ukilala.

Binafsi siamini katika adhabu za kaburi. Kwanza kwa kuwa hazijatajwa kwenye Qur'an, sijaziona. Pili Hadith iliyozitaja siikubali.

Ikiwa kuna adhabu ya kaburini basi Allah itakuwa "katudanganya" (AstaghafiruAllah) anaposema kwenye Qur'an kuwa kuna siku ya kiama (Kusimamishwa) kuhukumiwa? Sasa iweje tena tuhukumiwe kabla ya Kiama?

Naamini kuwa tunapotoka kwenye uhai kuingia kwenye umauti na hadi siku ya Kiama hakutakuwa na feeling za muda kama vile tupo hai. Itakua ni mano wa watu wa Pangoni, kisa cha kwenye Qur'an) au alielala miaka 100 kisa cha Qur'an).

Kifo, kinachokufa ni hiki kiwiliwili (body) chetu, nafsi haifi bali inaingia kweye umauti. Qur'an inahakikisha hili kwa kutukumbusha kuwa "kila nafsi itauonja umauti".

Hata sehemu tu ya kiwiliwili inaweza kufa na nafsi bado haijaingia kwenye umauti. Mfano ukikatika mkono au mguu, unakuwa umekufa huo mkono au mguu lakini nafsi bado haijaonja umauti.
Asante sana kwa elimu yako unayotupatia bure.
 
Back
Top Bottom