Che mittoga
JF-Expert Member
- Mar 28, 2017
- 12,658
- 16,205
Al-Shabaab ni mwanafunzi wa Al-Qaeda.Eti, mtu ameona video mmoja ya kipropoganda na anajitokeza kusema hawa magaidi wako sawa!
Al Shabab ni off-shoot ya Al-Qaeda, kama ilivyo Daesh (Islamic State), Boko Haram n.k. na makundi mengine ya kigaidi. Kinacho waunganisha hao wote ni mlengo yao ya Kiwahabbi yenye msimamo mkali - wameshikilia neno ya mstari ya msahafu na sio nia iliomo kwenye mstari! Quran imetamka wazi kuwa "La Ikraa fi Deen" - Hamna kulazimisha kwenye dini , lakini makundi hayo yanawalizimisha watu kufuata itikadi zao yaliyojaa umwagaji damu! Wanalipua mabomu kwenye makusanyiko ya watu na kusababisha vifo ya watu wasio na hatia! Waislamu wengi wameuliwa na mabomu ya magaidi wakiwa msikitini wakisali sala ya Ijumaa! [na huku kwenye video wanahamasisha watu wasali!!!!!]
Uhalisia ya maisha kwenye sehemu wanazotawala ni watu kuishi na hofu. Daesh pia walitoa video nyingi za kipropoganda - hospitali na huduma ya kijamii, lakini leo wafuasi wake wakiwa kambini kule Syria wanasema ilikuwa ni uzushi tu! Njaa, shida na magonjwa yalitawala! Somalia haina kitu ambayo ifanye mabeberu waingilie. Tatizo yao ni chuki za kikabila - clan warfare, iliyosababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe! Wasomali ni waislamu safi na wameshikilia uislamu hata kabla ya Al Shabab. Sasa kwenye hii nchi ya kiislamu Al Shabab inapigania nini? Lengo lao ni kupata mamlaka tu ambayo wataitumia vibaya!
Wanapigana nia yao kuanzisha utawala utakaofuata misingi ya Kiislamu yaani Sharia, ikiwezekana dunia nzima iwe chini ya Sharia.
Al-Qaeda waliwahi kuitawala Afghanistan na waliweka miongozo ya Sharia, na maisha yalikuwa yanakwenda kama kawaida.
Ndio maana nimeandika hao ni Waisilamu wenye msimamo mkali, na katu hawataki kuchamganyika na watu wasiofuata Sharia.
Ukiangalia mchamgo wangu wa kwanza nimesema wazi Kabisa kuwa wao wanapenda Jamii yote ifuate Sharia na hawataki jambo jingine.
Ndio maana hawajawahi kufanya fujo katika nchi ya Irani kwakuwa ni nchi inayofuata Sharia.
Waislamu wanaoshambuliwa ni Wale ambao hawa fuati miongozo ya Sharia, kwani kwao wanaonekana kama Wasaliti wa Dini ya Kiislamu.
Utambue kuwa Uislamu sio dini pekee, hapo haujakamilika.
Uislamu ni Dola kamili yenye mamlaka ya kutawala watu, kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Uislamu hauitambui Katiba ya nchi bali unaitambua Qurani na Sunna za mtume TU.
Uislamu ni lazima uambatane na utekelezaji wa Sharia ndio maana Waislamu wanadai Mahakama ya Kadhi, kama utimilifu wa imani yao.
Hivyo kwa mujibu wa Al-Shabaab Tanzania hakuna Uislamu na Waislamu kamili, kwani wanafuata Katiba iliyotungwa na binadamu badala ya Sharia iliyoagizwa na Mungu yaani Allah.
(tuendelee kuchangia kwa nia ya kuelimishana)