Al-Shabaab ni mwanafunzi wa Al-Qaeda.
Wanapigana nia yao kuanzisha utawala utakaofuata misingi ya Kiislamu yaani Sharia, ikiwezekana dunia nzima iwe chini ya Sharia.
Al-Qaeda waliwahi kuitawala Afghanistan na waliweka miongozo ya Sharia, na maisha yalikuwa yanakwenda kama kawaida.
Ndio maana nimeandika hao ni Waisilamu wenye msimamo mkali, na katu hawataki kuchamganyika na watu wasiofuata Sharia.
Ukiangalia mchamgo wangu wa kwanza nimesema wazi Kabisa kuwa wao wanapenda Jamii yote ifuate Sharia na hawataki jambo jingine.
Ndio maana hawajawahi kufanya fujo katika nchi ya Irani kwakuwa ni nchi inayofuata Sharia.
Waislamu wanaoshambuliwa ni Wale ambao hawa fuati miongozo ya Sharia, kwani kwao wanaonekana kama Wasaliti wa Dini ya Kiislamu.
Utambue kuwa Uislamu sio dini pekee, hapo haujakamilika.
Uislamu ni Dola kamili yenye mamlaka ya kutawala watu, kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Uislamu hauitambui Katiba ya nchi bali unaitambua Qurani na Sunna za mtume TU.
Uislamu ni lazima uambatane na utekelezaji wa Sharia ndio maana Waislamu wanadai Mahakama ya Kadhi, kama utimilifu wa imani yao.
Hivyo kwa mujibu wa Al-Shabaab Tanzania hakuna Uislamu na Waislamu kamili, kwani wanafuata Katiba iliyotungwa na binadamu badala ya Sharia iliyoagizwa na Mungu yaani Allah.
(tuendelee kuchangia kwa nia ya kuelimishana)