Umeeleza ukweli kabisa na ulichoeleza si wewe tu bali wakriso wote ndio wako hivyo kwamba wanaangalia yale yanayo wapendeza na ndiyo kipimo cha usahihi wa dini yao(ndiyo sababu kubwa wao kushikamana na ukristo) na si kuangalia ukweli ni upi ukweli hata kama haukupendezi,hivyo kwao si muhimu hizo ahadi nzuri zimetoka kwenye msingi wa ukweli au si kweli bali muhimu ni ahadi nzuri na mambo yenye kuwapendeza na kuwaridhisha.
UKWELI unao uongelea ni dhana mtambuka.
Ukweli wa mtu mmoja unaweza kuwa Uwongo kwa mtu mwingine pia.
Kwa mfano.
Dawa ya Mseto inaweza kumtibu mtu fulani ugonjwa wa Malaria na ikashindwa kumtibu mtu mwingine mwenye ugonjwa huohuo wa Malaria.
Au dawa hiyo hiyo ikamtibu mgonjwa fulani kwa kipindi fulani lakini baada ya muda fulani ikashindwa kumtibu tena ugonjwa uleule.
Huu ni utafiti wa Kisayansi.
Hivyo ndugu, ukweli wako sio lazima uwe ukweli wa mtu mwingine.
Na hata hao Al-Shabaab wanajiona wanafuata Ukweli wa maisha unavyotakiwa uwe.
Na ndio maana wanalazimisha na wengine wawe kama wao, na wafanye kama wao.
Yesu Kristo ni Binadamu pekee aliye weza kusimama hadharani na kusema kuwa yeye hana Dhambi na hakuna anayembishia kwa kipindi chote.
Na akasema pia Yeye ndiye NURU ya Ulimwengu, na ni NJIA, KWELI na UZIMA na hadi leo hakuna anayepinga.
Fulamu zinazotungwa kuonesha Matendo ya Yesu zote zinathibitisha maneno haya hadi hii leo.
KWELI nyingi zilizoonekana hapo awali zimefikia mahali zimeshindwa kujithitisha kuendelea ubora wake na zimekufa.
Leo dawa ya Chloroquine, haitibu tena Maralia.
Watu wengine maarufu wa zamani wanazuiwa kuoneshwa matendo yao hadharani kwa kuogopa fedheha.
Yesu Kristo ndio kabaki binadamu pekee ambaye ni Mfano wa binadamu wa kuigwa na wengine.
Na nakuambia ndiye, binadamu pekee wa kumsikiliza na kumwamini.
Kwakuwa ukimtazama usoni unasema hakika wewe ndiwe NURU, NJIA KWELI na UZIMA na chochote unachokisema ni sahihi.
Hapo Ndipo Lilipo Chimbuko na Nguzo ya Ukristo na Wakristo.
"Wameshika Chenye Nguvu"
Panahitajika Hekima Kubwa Kuelewa Hayo Maelezo na Mifano Niliyotoa Hapa.