kimsboy naona anajibu kwa hisia zake binafsi zaidi na sio kwa uhalisia wa ujumla wa mada husika.
Ni kwamba amekosea.
Kinadhalia hii hali inatokana na msuguano wa kitamaduni.
Al-Shababu ni Jamii yenye kufuata taratibu fulani za maisha yanayo wapendeza wao wenyewe.
Hivyo ni haki yao ya msingi kabisa ya kila jamii kuthamini utamaduni wao wa maisha.
Sasa inapotokea kuingiliwa na taratibu za jamii nyingine, ni lazima kuwe na uhiari wa makubalino kati ya pande mbili zinazokutana.
Kama ni kila jamii ifuate taratibu zake za kimaisha au kuwa na mwingiliano katika taratibu fulani kati yao.
Inapotokea jamii moja kuilazimisha jamii nyingine kiuufuata utamaduni mwingine kwakuwa tu jamii hiyo ina nguvu au uungwaji mkono kwa uwingi, basi hapo mgogoro unaanza kutokea.
Na madhara ya mgogoro wa aina hii matokeo yake ndio haya tunayoyaona yakifanyika na wanamgambo wa Al-Shabaab, Al-Qaida nk.
Ukiwaangalia Al-Shabaab wakiwa katika jamii yao unawaona hawana madhara Kabisa. Wanashirikiana na Jamii yao kujenga uchumi bila shida yoyote ile.
Hapo ndipo linapokuja Somo la
" Umuhimu wa Kuheshimu Tamaduni za Wengine "
Ni Somo refu kidogo, mtu anaweza kuanza na maandishi ya msomi mmoja namkumbuka kwa jina moja tu, anaitwa ndugu, Huntington.
Katika kitabu chake kinachoitwa
" The Clash of Civilization "
Kwako
kokontiko