John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Kundi la Al-Shabab nchini Somalia lilitumia dola milioni 24 mwaka 2021 kununua silaha, kulingana ripoti ya Taasisi ya Hiraal lenye makao yake Mjini Mogadishu.
Ripoti hiyo pia inadai kuwa Al-Shabab ambao wana ufungamano na Al-Qaeda, ina kusanya mapato ya karibu dola milioni 180 kila mwaka.
Ripoti hiyo iliyopewa jina la Al-Shabab’s Arsenal - From Taxes to Terror inasema kundi hilo linatumia mbinu mbalimbali kupata silaha, ikiwa ni pamoja na ununuzi wa moja kwa moja kutoka soko la ndani, na kutoka kwa wafanyabiashara wa silaha walio na kandarasi ya kununua na kusambaza silaha kutoka nje ya nchi, hasa Yemen.
Taasisi ya Hiraal pia inasema kwamba waasi wanadhibiti sehemu kubwa ya Somalia na kudumisha kiwango cha ushawishi kwa raia kupitia mchanganyiko wa ushawishi, utawala na kulazimisha.
Source: bbc