Alafu nyie watoto wa kishua, sio kila mtoto wa uswahilini ni kibaka. Wakati mwingine, please show us some respect

Alafu nyie watoto wa kishua, sio kila mtoto wa uswahilini ni kibaka. Wakati mwingine, please show us some respect

Watoto wa uswahilini hawa maskini wenzetu ndo wanazingua niliwahi kumsalimia demu wa kiswazi eti akanijibu "Koma hii ngoma ya gari"

Nikakumbuka wimbo wa Profesa J wa zali la Mentali na mimi nikajibu kimashairi nikaimba ile verse
"Nikasema Inshaallah hii yote sababu fukarašŸŽ¶
"Nisije nikakubaka nitupwe sero niwe kafarašŸŽ¶
Wakishua wanazingua sana mzee..
 
1. Nilikuwa maeneo ya parking ya Magari pale kitengo cha mifupa MOI mwaka 2014, nikiwa ninamsubiria mgonjwa ndugu yangu, jamaa alikuwa ofisini kwake, akaja akakagua kama mlango wa gari lake umefungwa vizuri, kisha huyo bila salama akarudi tena ofisini kuendelea na shughuli zake.

NB: Sio kila kijana anayetokea Mbagala, Temeke, Kivule, Buza ni mwizi au kibaka. Wengine dressing codes zao ni za hovyo kwa sababu ya umasikini tu lakini hizo tabia za udokozi hawana hata kidogo.

2. Mdogo wangu graduate wa kidato cha 4 alipewa Jukumu la kumsindikiza mgeni (mzungu wa Norway) aende Kariakoo shimoni kushangaa shangaa kidogo, lakini yule aliyempa dili (mtoto wa kishua) akawa ana msisitiza mara kwa mara ya kuwa "hakikisha haukimbii na camera zake, alafu usimuombe ombe hela" sasa dogo akawa ananiuliza "brother hivi huyu jamaa mbona ananiona kama vile mimi ni kibaka?"

Nyie wenye Good life watoto wa kishua, please show us some respect aisee. Sio kila kijana wa uswazi ni mwizi au kibaka, ndio maana wengine ni ndugu zetu lakini tunaogopa hata kuwatembelea huko Ununio na Mbweni kwa maana kwa mavazi yetu tu mtatuona kama vile wezi..
Ngoja niuchune na yangu moyoni.Sad!
 
Watanzania tuna kitu kimoja muonekano wako mtu anavokuangalia uso na mavazi anaanza kujenga fikra tofaut kichwan kwake

Huku mtaan jiran mwenye gar anapewa Salam za kutosha yaan utafikiri wanatoa msaada wa kula
Watu kama hawa wakikutana na Kichaa Dodoma watamuogopa na kudhania ni mtu wa usalama wa Taifa..
 
Kijana vaa vzuri uonekane mtu wa maana, acha ku justify ujinga wako kwasababu zisizo mashiko... Pia acha wizi kwasababu personality ndio uhalisia wa ulivyo kwa kiasi kikubwa... Jirekebishe otherwise utakosa mema ya nchi
Mema ya nchi sio kwa mavazi. Mema ya nchi ni kwa connection. Vaa vizuri bila kuwa na connection uone jinsi utakavyosugua gaga..
 
I'm married to the streets. I know all that sh!t Mzee..
ndo shida sasa

watu wanadhani kuishi kwenye umaskini kunawafanya wawe na upekee fulani

sio kila mwenye pesa ana dharau na sio kila anaekudharau anakudharau kwasababu ya umasikini wako

ukishajiwekea imani za ajabu kichwani basi utaishi kama digi digi

halafu dharau ni issue ya kawaida, unadhani wenye pesa hawakutani nayo?
 
Back
Top Bottom