Alafu nyie watoto wa kishua, sio kila mtoto wa uswahilini ni kibaka. Wakati mwingine, please show us some respect

Alafu nyie watoto wa kishua, sio kila mtoto wa uswahilini ni kibaka. Wakati mwingine, please show us some respect

1. Nilikuwa maeneo ya parking ya Magari pale kitengo cha mifupa MOI mwaka 2014, nikiwa ninamsubiria mgonjwa ndugu yangu, jamaa alikuwa ofisini kwake, akaja akakagua kama mlango wa gari lake umefungwa vizuri, kisha huyo bila salamu akarudi tena ofisini kuendelea na shughuli zake.

NB: Sio kila kijana anayetokea Mbagala, Temeke, Kivule, Buza, Keko, Tandale, Vingunguti ni mwizi au kibaka. Wengine dressing codes zao ni za hovyo kwa sababu ya umasikini tu lakini hizo tabia za udokozi hawana hata kidogo.

2. Mdogo wangu graduate wa kidato cha 4 alipewa Jukumu la kumsindikiza mgeni (mzungu wa Norway) aende Kariakoo shimoni kushangaa shangaa kidogo, lakini yule aliyempa dili (mtoto wa kishua) akawa ana msisitiza mara kwa mara ya kuwa "hakikisha haukimbii na camera zake, alafu usimuombe ombe hela" sasa dogo akawa ananiuliza "brother hivi huyu jamaa mbona ananiona kama vile mimi ni kibaka?"

Nyie wenye Good life watoto wa kishua, please show us some respect aisee. Sio kila kijana wa uswazi ni mwizi au kibaka, ndio maana wengine ni ndugu zetu lakini tunaogopa hata kuwatembelea huko Ununio na Mbweni kwa maana kwa mavazi yetu tu mtatuona kama vile wezi.

~ SIPENDI SIASA ~
Hawa watoto waliolaaniwa (Kishua) baba zao ndiyo vibaka wa mali zetu za umma, laana wanazopata baba zao kutokana na wizi wa umma wanakuja kutulaumu sie.
 
Mimi niko huwa niko tofauti kidogo. Kwenye shughuli zangu huwa naongeza umakini kwa mtu aliyevaa vizuri na watu wa dini pia nakua nao makini.

Kibaka apige mlege ili ukimtoa baruti umkamate kiurahisi?

Hata sendo au ndala vibaka ni nandra kuvaa wawapo kazini.
Upo kama mimi mkuu,

Wale wanaovaa vizuri sana na mtu anayejifanya wa dini sana huwa nakuwa naye makini mara mbili zaidi.

Kwa bahati mbaya sana asilimia kubwa ya wale wanaojifanya wa dini sana huwa sio watu wazuri , wengi wanaficha mambo yao kwa mgongo wa dini.

Mtu aliyepo smart sana kimavazi kwa asilimia kubwa kuna madhaifu ambayo anayaficha. Mara nyingi unakuta financially sio stable, au ana mapungufu katika utendaji wa kazi , hivyo anaficha madhaifu yake kwa looks.

Ni mara chache ukute tajiri au mtu competent akihangaika na mavazi.

Kwa hiyo ndugu hao unaokutana nao ni maskini wenye hela.
 
Watoto wa uswahilini hawa maskini wenzetu ndo wanazingua niliwahi kumsalimia demu wa kiswazi eti akanijibu "Koma hii ngoma ya gari"

Nikakumbuka wimbo wa Profesa J wa zali la Mentali na mimi nikajibu kimashairi nikaimba ile verse
"Nikasema Inshaallah hii yote sababu fukara🎶
"Nisije nikakubaka nitupwe sero niwe kafara🎶
Zali la mentali🎶🎶🎶 Dada habari naomba niulize swali, maskini koma hii ngoma ya ghali.
🎶🎶🎶🎶 Naitwa Vicky nina miaka 22 toka familia ya kitajiri.
 
Upo kama mimi mkuu,

Wale wanaovaa vizuri sana na mtu anayejifanya wa dini sana huwa nakuwa naye makini mara mbili zaidi.

Kwa bahati mbaya sana asilimia kubwa ya wale wanaojifanya wa dini sana huwa sio watu wazuri , wengi wanaficha mambo yao kwa mgongo wa dini.

Mtu aliyepo smart sana kimavazi kwa asilimia kubwa kuna madhaifu ambayo anayaficha. Mara nyingi unakuta financially sio stable, au ana mapungufu katika utendaji wa kazi , hivyo anaficha madhaifu yake kwa looks.

Ni mara chache ukute tajiri au mtu competent akihangaika na mavazi.

Kwa hiyo ndugu hao unaokutana nao ni maskini wenye hela.
Uwe na hela uvae nguo Moja wiki hizo zitakue hela za ndagu Raha ya utajiri pesa itumike maana pesa kazi yake kutumia
 
Kijana vaa vzuri uonekane mtu wa maana, acha ku justify ujinga wako kwasababu zisizo mashiko... Pia acha wizi kwasababu personality ndio uhalisia wa ulivyo kwa kiasi kikubwa... Jirekebishe otherwise utakosa mema ya nchi
Asalamaleko
 
Back
Top Bottom