Alama ya jicho moja: Je, ni ishara katika vikundi vya siri, ishara katika Uungu (Ukristo), ishara ya Mungu wa Misri au uwakilisho wa mpinga Kristo??

Alama ya jicho moja: Je, ni ishara katika vikundi vya siri, ishara katika Uungu (Ukristo), ishara ya Mungu wa Misri au uwakilisho wa mpinga Kristo??

ALL SEEING EYE, EYE OF
ROVIDENCE
- 2






ALAMA YA JICHO KATIKA JAMII ZA SIRI (FREEMASONRY/ILLUMINANT)
NA MAANA YAKE.










Wasalaam,


Screenshot_20210422-094101.png




Na vipi kuhusu Vikundi vya siri Chini ya illuminant na alama hii ya Jicho, ??


Basi vipi kuhusu Illuminati?
Maelezo ya mwanzo ya vikundi hivi na asili, iliyoanzishwa huko Bavaria 1776 , utumiwaji wa alama hii katika vikundi vingi vya siri ikaunganishwa na uwekaji wa alama hii katika mihuri ya nembo za mataifa makubwa ambapo inaelezwa serikali zake zina mkono na mwongozo wa shetani

Screenshot_20210422-094003.png


Ni kweli kwamba Illuminati wanaongoza vikundi vingi vya siri kama Freemasonry na vinginevyo ambavyo mara kadhaa vilitumia Jicho la Providence kama ishara yao kwa Mbunifu Mkuu (Mungu), kufuatia mwongozo wa makanisa mengine mengi wakati huo


Na ni kwawaida kwa vikundi hivi kujinasibu katika sehemu mbalimbali yakuwa havina tofauti na dini nyingine kuwa vinaabudu Mungu mmoja lakini si ajabu kuona members wao pia wakitukuza uwepo wa shetani na hivi ndivyo tujuavyo kikawaida.


Kinyume na imani hizo nyingine inaelezwa katika makundi haya ya siri, watu wengi wanaamini hiyo ishara ipo kuwakilisha jicho la Lusifa au Shetani ambaye nguvu zake zisizo za kawaida huathiri kila kitu kinachotokea ulimwenguni.

Na hivyo ndivyo Tujuavyo katika makundi haya kuwa ruled under Satan, Jicho hili lipo huwekwa juu ya Pyramid au Ndani yake huaminika kama Ndiyo nyenzo na utambulisho wa supernatural power yao , Au system of controll

Screenshot_20210422-093207.png


Jicho hili la Providence pia ni ishara muhimu sana ya haya makundi ya siri (illuminant) ambayo kawaida ina utukufu wake, na pia jicho hilo , Freemason chini ya Illuminant wanamtaja Mungu wao mwenye nguvu zote kama 'Mbunifu Mkuu wa Ulimwengu' na ishara hiyo hutumiwa kukumbusha kila Mwanachama wa siri kukumbuka mawazo yake pamoja na matendo ambayo yanazingatiwa na Mungu wakati wote.


Na kumbuka habari ya makundi haya ya Siri yaongozayo Duniani kwa sasa yapo chini ya Shetani mwenyewe kama Mungu wao mkuu, hivyo jicho hili ni kama Uangalizi wa Lucifer dhidi ya Dunia yetu.
Na hapa ndipo ikaja taarifa kuhusu uhusihwaji wa alama hizi na mataifa makubwa ya dunia katika mihuri yao.

Screenshot_20210424-040929.png


Na katika zama zetu za kisasa Wasanii na watu mashuhuri ambao wamekuwa wakihusishwa na kuwa Chini ya Vikundi vya Siri mara nyingi Freemasons N.k wameonekana wakionesha sehemu mbali ishara ya Jicho hili ,All seeing Eye , Watu wameshutumu wakina Madonna, Jay-Z , Beyonce , Lady Gaga , Justin Bieber, na wengineo wengi wakiwemo viongozi wengi
Screenshot_20210424-040121.png



Screenshot_20210424-040102.png


Hata hivyo ishara ya Jicho hili pia imeonekana katika Tattoo za watu mashuhuri wengi sana wengi wakidai ni utambulisho wa shetani., jicho la Shetani.


Screenshot_20210424-040905.png


Lakini wasanii na Watu maarufu waliotumia ishara hii wote wameshtumiwa kwa kutumia Ishara za kiIlluminati, pamoja na Jicho la Providence wameonekana wapo chini ya makundi ya Shetani na ndiye anayewapa Nguvu ya umaarufu wao, pesa,mvuto na kadhalika Heshima kwa kuonyesha ishara ni kitu muhimu sana kwao

Hivyo ishara hii ni kama utukuzo wa kazi ya Satan


Screenshot_20210425-155346.png


Screenshot_20210425-154927.png






ITAENDELEA



ALAMA YA JICHO NA UWAKILISHO WA MPINGA KRISTO ( MASIH DAJAL/ANTI CHRIST)









daVinci XV


Screenshot_20210422-092536.png
 
ALL SEEING EYE, EYE OF
ROVIDENCE
- 3

Tunaendelea


ALAMA YA JICHO NA UWAKILISHO WA MPINGA KRISTO ( MASIH DAJAL/ANTI CHRIST)
 
ALL SEEING EYE, EYE OF PROVIDENCE - 1





Wasalaam,

View attachment 1762279

Kila mmoja alama hii aliitafsiri vile ajuavyo yeye huku madaai ya kuhusishwa na vikundi vya Illuminant /Freemasonry yakishamiri zaidi.

Wengi wetu tumeichukulia kama alama ya mficho, kama zilivyo alama nyingi za kuficha na yenye ishara za siri.

'EYE OF PROVIDENCE' Alama ya jicho lililowekwa ndani ya pembetatu (pyramid) ni ishara ambayo imehusishwa na nadharia nyingi sana,

Alama ya jicho hilo sio tu linaonekana kwenye makanisa mengi na majengo ya Masons na vikundi vya siri ulimwenguni, pia inaoneka nyuma dola moja ya Marekani na vile vile kama Muhuri Mkubwa wa Marekani

Alama hii imesemwa kwenye nadharia nyingi za kushangaza na zisizo za kawaida

View attachment 1762302

Mfano

- kama upatikanaji wake kwenye nembo na vielelezo(dola) vya serikali ya Marekani,

- Alama na Ishara ipatikanayo kumwakilisha mungu katika dini (Ukristo)

- Upatikanaji wake katika vielelezo na nembo za Vikundi vya Siri (ilumminant)

- Kitambulisho cha Mungu wa Kipagani wa Misri ya kale, na Pia alama hii Uhusishwaji wake na Mpinga kristo (Anti christ)

Hizo ni miongoni mwa nadharia kuhusu Alama hiyo.

View attachment 1762298

Kwa hivyo, asili ya Jicho la Providence ni nini,??
kwa nini inatusugulisha sana???
na kwanini inaunganishwa mara kwa mara na ushetani na makundi ya (Freemason/Illuminati) na hizo nadharia nyinginezo????

Leo tutangalia japo kwa uchache miongoni mwa nadharia hizi kuhusu Alama ya Jicho hilo

TUENDELEE

JICHO KAMA ISHARA YA MUNGU KATIKA DINI (UKRISTO)

Hapo awali alama hii ya Jicho lilikuwa kama ishara ya Kikristo, na matumizi yake yanaweza kupatikana katika kazi nyingi za sanaa za kidini hasa katika kipindi cha Renaissance na alama hii ilikuwa ikiwakilisha Mungu. Mfano wa kazi ya sanaa ya kipindi hiko ni kama ile Tafrija ya Bwana YESU kazi ya mchoraji nguli wa kiitaliano Pontormo ya 1525 huko Emmaus.

Katika mchoro huo unaonyesha Alama ya Jicho hili na inaelezwa ikaangaza katika Tafrija ya mlo huo.
Ilibuniwa kama ishara ya uangalizi wa huruma ya Mungu juu ya binadamu.

View attachment 1762282

Chanzo kingine muhimu cha Alama hii kilikuwa katika kitabu cha nembo kiitwacho Iconologia, kilichochapishwa mwanzo mwaka 1593.

Katika matoleo ya baadaye, 'Jicho la Providence' lilionyeshwa kama sifa ya mfano wa 'Utoaji wa Kimungu', yaani wema wa Mungu kwa waadamu
Na ilibuniwa kama ishara ya uangalizi wa huruma ya Mungu juu ya binadamu.

Lakini kama ujuavyo alama ya jicho hili imeambatanishwa na Pembetatu (Pyramid) katika mingi kati ya mionekano yake.

Hakuna mtu anayejua ni nani aliyeibuni hivyo hapo awali, lakini ni nani aliyeiunda nje ya mipangilio ya kanuni za kidini zilizokuwepo hapo awali. ,,?

Inaelezwa pembetatu ilikuwa ni ishara ya utambulisho ya muda mrefu ya Utatu wa Kikristo ule wa Baba, Mwana na Roho Mtakatifu,
Miale ya mwangaza ambayo mara nyingi huonyeshwa ikitoka kwenye JICHO hilo, inaelezwa pia ni ishara iliyokuwepo hapo zamani ya mng'ao wa Mungu katika taswira ya Kikristo.
Lakini asili ya jicho hilo ni nini???
Huyo huyo Mungu alikuwa ameonyeshwa kwa njia nyingi za mficho hapo awali pia.

JICHO MOJA ISHARA NA ALAMA YA MUNGU WA KALE WA MISRI HORUS.

View attachment 1762292



Lakini walikuwa Wamisri wa zamani ambao inasemwa ndiyo walikuwa waanzilishi wa alama hiyo jicho Waliyoitengeza vyema karne nyingi nyuma.

kwa mfano, Alama za macho zillichorwa kwenye majeneza ya wafu ambayo kwao walikuwa na maana ishara hiyo iliruhusu wafu kuona kupata nuru ya muelekeo katika maisha yao ya baadaye.

View attachment 1762285

Na moja ya alama maarufu zaidi ya Misri ni Jicho la Horus.

Horus alikuwa mungu wa kale wa anga wa Misri ambaye kwa kawaida alionyeshwa kama Ndege(falcon) na mfanano pengine kama wa mbwa mwitu au peregrine.

Jicho lake la kulia lilihusishwa na mungu wa jua aitwaye Ra.

View attachment 1762290

Alama ya jicho hilo la Horus ipo katika muundo wa mchanganyiko wa jicho la mwanadamu na Ndege,,,na lina nyusi pamoja na alama ya shavu.
Kulingana na hadithi za zamani za Wamisri, Mungu-Mfalme Horus ,{mara nyingi huonyeshwa kama Ndege(falcon) au kichwa cha ndege( falcon)} alitolewa macho vitani na mjomba wake Set.

Kwa msaada wa Thoth, baadaye aliponya macho yake Horus.
Na Jicho la Horus, hivyo lilikuwa ishara ya kinga, mara nyingi pia kutumiwa kama hirizi, Watu walikuwa na vijisanamu vidogo vya Alama hiyo vya kutosha kwa mtu kubeba mfukoni mwake kama njia ya ulinzi.

View attachment 1762291

Hii na hieroglyphs zingine za Wamisri kuhusu Alama ya, ziliendelea kuathiri picha za Ulaya za wakati wa Renaissance na kufifisha Alama hiyo kama ishara ya Mungu. Na Wakati huo, wasomi na wasanii walipendezwa na maandishi ya Misri, kuhusu Alama hii nao waliamini kwamba yalitafsiri uwakilisho wa Mungu

View attachment 1762297

Na kuhusu Pyramids kwenye Nadharia hii ya jicho moja kuwakilisha jicho la Horus ikajibiwa ni utambulisho au uwakilisho wa Pyramids za huko misri ambazo zilikuwa ni desturi yao kujenga Pyramids na Kuzika humo miili ya viongozi wao , kuhifadhi vitu vya thamani na mambo mengine na shughuli nyingine nyingi nyingi.

ALAMA JICHO KATIKA VIELELEZO VYA TAIFA LA MAREKANI

Miaka michache mwanzo , mwaka 1782 Muhuri Mkubwa wa Marekani ulionyeshwa
(mfano kwenye fedha na kwingineko)

View attachment 1762294
Thomas Jefferson, Benjamin Franklin na John Adams walikuwa wamependekeza maoni yao juu ya muundo mihuri hio, lakini Charles Thomson, Katibu wa Baraza la Continental (congress), ambaye alikuja na Alama hiyo ya pyramidi na Jicho la Providence, katika ya mambo ya muhuri, kwa kushirikiana na mwanasheria mdogo na msanii anayeitwa William Barton.

View attachment 1762295

Piramidi hiyo katika mihuri hii ya marekani ni ile ambayo haijakamilika (Iliyokatwa juu) ilikusudiwa kuashiria "STRENGTH and DURATION", na Levels 13 za kuwakilisha majimbo 13 asilia ya Marekani.

Alama hiyo ya jicho , pia kama ilivyotumika kwingine kutoka kipindi kama hicho huko Uingereza na Ufaransa na inaelezwa ilikuwa ishara ya kawaida kwa uangalizi wa huruma wa Mungu kwaa mataifa hayo (wanadamu).

Katika moja ya mifano hiyo inaelezwa kulikuwa na Freemasonry/, Illuminanti iliyohusika na uchaguzi wa ishara hiyo na kuziingiza katika serikali hizo.

View attachment 1762299

ITAENDELEA





ALL SEEING EYE, EYE OF
ROVIDENCE
- 2





ALAMA YA JICHO KATIKA JAMII ZA SIRI (FREEMASONRY/ILLUMINANT)
NA MAANA YAKE.










daVinci XV

View attachment 1762277

View attachment 1762280
Mambo ya Babylon ya Nabukadneza

Kitabu cha Daniel kimeeleza kwa kina.
 
ALL SEEING EYE, EYE OF
ROVIDENCE
- 3







ALAMA YA JICHO NA UWAKILISHO WA MPINGA KRISTO ( MASIH DAJAL/ANTI CHRIST)



Screenshot_20210424-035543.png



Dajjal au Mpinga kristo (ant christ) ameonekana pia katika simulizi ya Kiislamu. Anasemekana atakuja kutoka maeneo kadhaa tofauti, lakini kwa ujumla kutoka Mashariki, kawaida kati ya Syria au Iraq kulinganishwa na uelewa wa Kikristo juu ya kuonekana kwa Mpinga Kristo katika simulizi ya Kikristo.

Huyu mwamba ni katika miongoni mwa makundi ya Upande wa Lucifer ambaye atakuja kudanganya wanaadamu kwamba, yeye ndiye Yesu (Issa)


Kwa kufanya baadhi ya Miujiza na watu kumwamini.

Screenshot_20210424-035816.png


Maeneo kadhaa yanahusishwa na kuibuka kwa Dajjal, lakini kawaida, imeelezwa atatokea kutoka mashariki,

Kwa muonekano wa kawaida huelezewa kama kipofu katika jicho moja, na wengine husema kuwa ana jicho moja, inaelezwa Kumiliki jicho hilo lenye kasoro mara nyingi humwezesha kama kutoa nguvu (miujiza) katika malengo yake ya kupotosha Ulimwengu kama Masih Fake na hapa Ndipo makundi haya Shetani yanapochukua Alama hii ya Jicho kumwakilisha Baba yao huyu.

Screenshot_20210424-035640.png


Anasimuliwa atazuguka ulimwenguni kote akiingia kila mji , Kama Masihi wa uwongo, inaaminika kwamba wengi watadanganywa naye na watajiunga katika msafara wake, kati yao Wayahudi, Wabedouins, watu wa kawaida(dini tofauti tofauti), wachawi wengine.


Zaidi Dajjal (Anti christ) atasaidiwa na jeshi la shetani, na inaelezwa wafuasi wake wengi wa kuaminika watakuwa Wayahudi

Dhana hii ya Wayahudi kuwa wengi zaidi katika wafuasi wengi wa Dajjal labda ni mabaki kutoka kwa hadithi za Kikristo za Mpinga Kristo.
Dajjal ataweza kufanya miujiza, kama vile kuponya wagonjwa, kufufua wafu (Hapa zitatumika nguvu za Shetani), na Miujiza mingimingi.

Screenshot_20210424-035849.png


Miujiza yake inafanana na ile iliyofanywa na Yesu. Na hapo ndipo watu wengi watakapomuamini kama Masih halisi na kupotezwa nae, Nguvu ya jicho lake ambalo nadharia hii inalihusisha kama Jicho ambalo ni Alama katika makundi na watawala wa Dunia kumuwakilisha.


Mwishowe, Dajjal(antichrist) atakufa pale atakaporudi Yesu na kumuua Katika tafsiri nyingi inasemwa atakufa kwa kumtazama tu Yesu.

Screenshot_20210424-035605.png

Lakini wakati huo tayari ashakusanya kundi kubwa la watu katika Upande wa shetani
Na kwa kutambua mchango wake Jicho lake likawa kama identity na Heshima ya Kazi yake katika makundi haya.


Hiyo ni Miongoni mwa nadharia zinazoelezewa kuhusu Jicho hilo. katika Upande huu.









daVinci XV


Screenshot_20210424-035816.png
 
Itabidi tushushe nyingine mkuu ,, ikihusisha vitabu vya ufunuo ,Daniel na Mengineyo

Well said mkuu...

Nafukua mambo ya personal and physical presence of God Almighty. Acha tuone inakuwaje!
 
Misri ya kale ndio chimbuko la dini ya kiislamu na kiyahudi na kikristu
 
Mwamba anataka tumpiganie Mungu wa Abraham, Isaac na Jacob. Hajui kwamba huyu Mungu anajipigania mwenyewe. Na hajawahi kushindwa jambo lake.

Alishindwa Nabukadneza Mfalme wa Babylonian, aliyekuwa na taasisi za kufundisha uchawi, ulozi, kuongea na wafu, kusoma nyota nk ndio itokee leo? HAIWEZEKANI.

IMG_20210627_163112.jpg


IMG_20210627_163817.jpg


IMG_20210627_163938.jpg
 
Back
Top Bottom