Albamu mpya ya Burna Boy ni moto mkali sana

Albamu mpya ya Burna Boy ni moto mkali sana

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Posts
21,113
Reaction score
65,124
Saa hizi niko mtandaoni nasikiliza Album ya Burna Boy ya "Twice As Tall" na nimefurahishwa nayo kupita kiasi.Niseme tu, nadhani huyu jamaa ana kipaji kikubwa na kila siku anazidi kukomaa tu. Humu ndani wametokea wasanii wakubwa duniani kama Youssou N'Dour, Christ Martin (Vocalist wa Cold-Play) na Naughty By Nature.

Kuimba na wasanii wakubwa kama hawa na kwenda nao vizuri kwa mahadhi ya kiafrika siyo kazi rahisi. Nilidhani album yake ya African Giant ndiyo kazi yake bora sana ya muda wote, lakini hii Twice As Tall ni nzuri zaidi. Naamini wasanii wetu wana kitu kikubwa cha kujifunza kutoka kwa Burna Boy.

Nilikuwa najiuliza kwanini wasanii wenye uwezo mkubwa kama Sauti Sol hawatambuliwi kama inavyotakiwa hapa Afrika Mashariki, lakini naamini baada ya hii Album kutoka Sauti Sol watapata kutambulika kimataifa na kupata heshima wanayoistahili. Msanii mkubwa kama Burna Boy kuwashirikisha Sauti Sol kwenye Album kubwa hivi inaashiria kwamba ameukubali uwezo wao.

Burna Art.jpg
 
Hii album itafika mbali zaidi ya African Giant..
Kwanza Diddy kaipa promo kubwa sana .
Ni one of the best album for 2020.
So far my favourite tracks kwa hii album ni
Wonderful, way too big na time flies.
Kwenye hii time flies saut Sol wamefanya unyama sana.
Burna boy anajua sana .
 
Nimeisikiliza sana jana hizo tracks...
 
Mimi hii album nimeiskiliza ila niliangalia ktk angle ya production,yaani biti ya nyimbo zote zimetulia masikioni na zipo ktk viwango vya juu nikajaribu kusikiliza hits songs za nchi yetu nikaja kugundua tuna safari ndefu ya kuproduce nyimbo zenye ubora.

Mpaka najiuliza hivi kwa nini wasiwalipe hela nzuri Master Jay na P Funky hasa upande wa mixing ili wapate nyimbo zenye ubora.

Biti zetu kusema kweli hazipo kwenye std nzuri.Nyimbo nilizo zikubali ile ya Naughty by Nature na Twice as tall ft Youssou N'dour.
 
Biti zetu kusema kweli hazipo kwenye std nzuri.Nyimbo nilizo zikubali ile ya Naughty by Nature na Twice as tall ft Youssou N'dour.
Ukiona jamii inang'ang'ana kumdhihaki msanii mwenye uwezo mkubwa kama Lady Jay Dee "Komando" kwa kumlinganisha na mtoto kama Zuchu basi fahamu kwamba kuna tatizo pahala (Like Seriously!!!) . Shida ni kwamba tunachanganya kati ya umaarufu na kipaji na hata hao watangazaji wa burudani wenye dhamana ya kukuza muziki wetu huko redioni hawajui kabisa muziki. Nakumbuka Burna Boy anavyoanza miaka hiyo kuna mtangazaji wa redio kubwa alisema hamuelewi kabisa jamaa, niliishia kusikitika tu.

Burna boy kila siku anakomaa na anajifunza sana, walimu wake wa muziki (Mentors) ni Femi Kuti na Angelique Kidjo sasa mtu kama huyu akifikisha One Billion Streams utashangaa kweli ??? Ukweli ni kwamba muziki ni kama taaluma nyingine na inahitaji kukaa chini na kujifunza kila siku, kitu ambacho watanzania wengi hatutaki kabisa kukisikia (Sauti Sol wanajitahidi sana kwenye hili). Tunaweza kupata Views nyingi You-Tube lakini tusiweze kuacha alama yoyote ile kwenye tasnia ya muziki hapa barani Afrika.
 
Ukiona jamii inang'ang'ana kumdhihaki msanii mwenye uwezo mkubwa kama Lady Jay Dee "Komando" kwa kumlinganisha na mtoto kama Zuchu basi fahamu kwamba kuna tatizo pahala (Like Seriously!!!) . Shida ni kwamba tunachanganya kati ya umaarufu na kipaji na hata hao watangazaji wa burudani wenye dhamana ya kukuza muziki wetu huko redioni hawajui kabisa muziki.

Burna boy kila siku anakomaa na anajifunza sana, walimu wake wa muziki (Mentors) ni Femi Kuti na Angelique Kidjo sasa mtu kama huyu akifisha One Billion Streams utashangaa kweli ??? Ukweli ni kwamba muziki ni kama taaluma nyingine na inahitaji kukaa chini na kujifunza kila siku, kitu ambacho watanzania wengi hatutaki kabisa kukisikia (Sauti Sol wanajitahidi sana kwenye hili). Tunaweza kupata Views nyingi You-Tube lakini tusiweze kuacha alama yoyote ile kwenye tasnia ya muziki hapa barani Afrika.
Hiyo kwenye industry yetu naona ishakuwa kawaida,Diamond kila siku analinganishwa,Jide mwenyewe kishalinganishwa na wasanii wote wa kike ila,ukikaa chini na kufanya utafiti,Jide kiatu chake hamna anayeweza kukivaa,Jide atabaki kuwa Jide.

Mimi sijazungumzia upande wa wasanii mimi nimezungumzia production ya nyimbo.

Wasanii wabongo hawa waheshimu maproducer na ndio maproducer wengi wanaojua wameamua kukaa pembeni,ukizisikiliza biti ktk hii album alafu uje kwenye hizi hits songs zetu kuna utofauti mkubwa,yaani sisi biti zetu zipo hovyo.
 
Nakuelewa vizuri kabisa mkuu, ndiyo maana nikasema muziki ni taaluma kama taaluma nyingine, inahitaji utaalamu wa hali ya juu zaidi ya "kuimba tu" ili kufanya kazi ya msanii ifanye vizuri sokoni. Production ni sehemu (A Single Component) tu ya muziki ambayo inabeba kazi ya msanii: Ili kukua zaidi inabidi tukae chini tujifunze ni wapi tunakwama na tuweze kurekebisha siyo huu ujuha ambao tunaufanya saa hizi na kuridhika nao.
 
Mimi najua Mziki Upo Bongo Ao wakina Burna boy Sijui wakina Nani Ata Siwaelewi.
Kwanza Wanaimba kizungu kibaya
Hata Chifu Mangungo hakuona umuhimu wa dhahabu akaamua kubadilisha na shanga na vioo kutoka uajemi akidhani ndiyo vitu muhimu sana kwake. Hivyo wewe unapokuwa huuelewi mziki wa mtu kama Burna Boy sishangai kabisa,.....
 
Mimi hii album nimeiskiliza ila niliangalia ktk angle ya production,yaani biti ya nyimbo zote zimetulia masikioni na zipo ktk viwango vya juu nikajaribu kusikiliza hits songs za nchi yetu nikaja kugundua tuna safari ndefu ya kuproduce nyimbo zenye ubora.

Mpaka najiuliza hivi kwa nini wasiwalipe hela nzuri Master Jay na P Funky hasa upande wa mixing ili wapate nyimbo zenye ubora.

Biti zetu kusema kweli hazipo kwenye std nzuri.Nyimbo nilizo zikubali ile ya Naughty by Nature na Twice as tall ft Youssou N'dour.

Mtu anaimba amabhoko amaguru
 
Hii album ni moto kuna wimbo unaitwa The monster you made aisee wazungu hawataupenda maana umesema kila kitu wazi waafrica tunachofanyiwa
Huu kaimba na mzungu Chris Martin (Jamaa wa Cold-Play), mle ndani kamtukana hadi Mungo Park yule mpelelezi wa kikoloni aliyefia mto Niger. Sasa kazi "Provocative" kama hii ndiyo itamfanya afike mbali kwasababu itazungumziwa sana huko Ulaya na Marekani, kama ile kazi ya Childish Gambino "This is America".

Hahahaha, halafu pale mwishoni kabisa kuna sauti ya Mama yetu Ama Ata Aidoo akiwaponda wazungu kuhusu ukoloni. Yaani aina hii ya utunzi inahitaji mtu aliyekomaa sana kimawazo na kitafakuri....
 
Nakuelewa vizuri kabisa mkuu, ndiyo maana nikasema muziki ni taaluma kama taaluma nyingine, inahitaji utaalamu wa hali ya juu zaidi ya "kuimba tu" ili kufanya kazi ya msanii ifanye vizuri sokoni. Production ni sehemu (A Single Component) tu ya muziki ambayo inabeba kazi ya msanii: Ili kukua zaidi inabidi tukae chini tujifunze ni wapi tunakwama na tuweze kurekebisha siyo huu ujuha ambao tunaufanya saa hizi na kuridhika nao.
Watu wakutusaidia kututoa ktk huo mkwamo tunao(P Funky &Master Jay no) ila wasanii hawataki kuwatumia sababu wanaogopa gharama.

Asikudanganye mtu Wanaija wamewekeza hela nyingi sana kwenye mziki wao,kuanzia promotion mpaka production na mshika dau anaheshimu uweledi wa mwenzake.

Hapa Tanzania msanii anaongea kabisa na kumjibu shit producer "...bila mimi wewe usingekuwa producer mkubwa......",hii kauli ni ya dharau.
 
Watu wakutusaidia kututoa ktk huo mkwamo tunao(P Funky &Master Jay no) ila wasanii hawataki kuwatumia sababu wanaogopa gharama.
Hawa jamaa walikuwa wanajitahidi sana, na walau walikuwa wanajua muziki! Lakini nakumbuka waliwahi kupigwa sana vita na vyombo vikubwa vya burudani.
 
Back
Top Bottom