Albamu mpya ya Burna Boy ni moto mkali sana

Albamu mpya ya Burna Boy ni moto mkali sana

Attachments

Mimi hii album nimeiskiliza ila niliangalia ktk angle ya production,yaani biti ya nyimbo zote zimetulia masikioni na zipo ktk viwango vya juu nikajaribu kusikiliza hits songs za nchi yetu nikaja kugundua tuna safari ndefu ya kuproduce nyimbo zenye ubora.

Mpaka najiuliza hivi kwa nini wasiwalipe hela nzuri Master Jay na P Funky hasa upande wa mixing ili wapate nyimbo zenye ubora.

Biti zetu kusema kweli hazipo kwenye std nzuri.Nyimbo nilizo zikubali ile ya Naughty by Nature na Twice as tall ft Youssou N'dour.
Nikweli mkuu kama mtu nimskilizaji namuelewa mzuri lazima utagundua hilo, kwenye nyimbo zetu zakibongo nikama utaona aidha sauti ya muimbaji iko chini Sana kuliko sauti za vyombo au sauti ya muimbaji iko juu sana nahata vyombo huvisikii.
Kuna msanii wa hapa bongo anaitwa Damian soul anaimba nyimbo Nzuri sana kama hakuna matata, nothing but love lakin shida nihio
 
Screenshot_20200818-091401.jpg
 
Ukiona jamii inang'ang'ana kumdhihaki msanii mwenye uwezo mkubwa kama Lady Jay Dee "Komando" kwa kumlinganisha na mtoto kama Zuchu basi fahamu kwamba kuna tatizo pahala (Like Seriously!!!) . Shida ni kwamba tunachanganya kati ya umaarufu na kipaji na hata hao watangazaji wa burudani wenye dhamana ya kukuza muziki wetu huko redioni hawajui kabisa muziki. Nakumbuka Burna Boy anavyoanza miaka hiyo kuna mtangazaji wa redio kubwa alisema hamuelewi kabisa jamaa, niliishia kusikitika tu.

Burna boy kila siku anakomaa na anajifunza sana, walimu wake wa muziki (Mentors) ni Femi Kuti na Angelique Kidjo sasa mtu kama huyu akifikisha One Billion Streams utashangaa kweli ??? Ukweli ni kwamba muziki ni kama taaluma nyingine na inahitaji kukaa chini na kujifunza kila siku, kitu ambacho watanzania wengi hatutaki kabisa kukisikia (Sauti Sol wanajitahidi sana kwenye hili). Tunaweza kupata Views nyingi You-Tube lakini tusiweze kuacha alama yoyote ile kwenye tasnia ya muziki hapa barani Afrika.
Tanzania huwa tunaangalia view milioni kwa dakika ngapi, hatuangalii content.
 
Hahah mzee umeisikiliza after hours ya the weekend ?

Huyu mtu anasubiria Grammy yake tuu maana mpaka sasa hana mpinzani kwenye album kali
Yaani kitendo cha Burna Boy kulinganishwa na watu kama The Weeknd kinanipa furaha kubwa sana.
 
Back
Top Bottom