Albert Chalamila: Sasa naunda task force kubwa itakayokuwa na silaha

Albert Chalamila: Sasa naunda task force kubwa itakayokuwa na silaha

Task force ni haina maana sanasana ni kuwatajirisha hao washiriki wa task force. Acha mufumo iliyopo iendelee kufanya kazi hata kama ni midhaifu.

Spending kabisa idea ya task force kutokana na niliyoyaona wakati wa Magufuli
12 February 2024

TASK FORCE / KIKOSI KAZI CHINI YA MKUU WA MKOA, CHAKAMATA WATU KADHAA MKOA WA DAR ES SALAAM

Hayo yasemwa na mkuu wa mkoa wa DSM alipokuwa katika operesheni maalum

View: https://m.youtube.com/watch?v=oHAwL1r-kfw

Mkuu wa mkoa ameyasema mbele ya mkuu wa wilaya ya kinondoni mkoani Dar es Salaam Mhe. Saad Mtambule na maofisa

Sasa task force itajumuisha Polisi, na vikosi vingine siri kwa kuwa inaonesha kuna watu ndani ya vyombo vya umma wanahusika na magendo

Ukanda wa bahari wa kuanzia kusini kwa mkoa wa DSM Mpemba Mnazi hadi Bunju mpakani na Bagamoyo mkoa wa Pwani ni maeneo yanayotumika kuingiza bidhaa za magendo toka Zanzibar.

Na hili pia ni tishio la usalama, maana mbali ya magendo pia silaha, nyaraka za kichochezi, 'hela chafu' n.k zinaweza kuingizwa kwa magendo kipindi hiki tukielekea uchaguzi zikitoka Zanzibar, RC Albert

Vilevile RC Chalamila amesema lazima tulinde kama tulivyo kula kiapo hatuwezi kuruhusu magendo katika Mkoa huu tuko imara sana kwa masilahi mapana ya ustawi wa jamii na amani ya Taifa hili
 
Ukweli ukanda huo hasa bunju jamaa wa kaisari walijiachia mno na hayo magendo tena ilikuwa wazi wazi na dili za mafuta ya kula hayo. Yaani mpaka unijiuliza hii nchi itakuja kuwa na jamii ya kistaarabu kweli miaka kumi ijayo?.
Hii ipo kule Kisiju na Nyamisati pia.
Serikali inajua.
Polisi wanajua.
TRA wanajua
Usalama wanajua.
 
Ngoja waje spin Doctors.

Utawasikia.....

"Oh wanaleta mitutu"
img_20240203_204836-jpg.2893205

Halafu wale wa Utengano nao

"Oh tuuvunje huu Muungano"

...sio hao tu wapo wale watakaosema
"Matumizi mabaya ya madaraka na Rasilimali"

Yaani sijasema bado, hata kataa ndoa nao watadai ...

"Ona hao vijana wenyewe ni mijambazi" Untill proven Innocent.
1707696746947-png.2901348
😁😅

Unauliza mimi nitasema nini?
Kwa nini wamevuliwa nguo?
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Februari 11, 2024 ametangaza kuendelea kwa Operesheni kali ya kudhibiti upitishwaji holela wa bidhaa mbalimbali za magendo katika fukwe za bahari ya Hindi ambapo amesema yoyote atakaye kamatwa adhabu kali itachukuliwa dhidi yake kwa mujibu wa sheria za nchi.
Kama zinapita kutoka Zanzibar kuna shida gani si tumesema sisi ni nchi moja?
 
12 February 2024

TASK FORCE / KIKOSI KAZI CHINI YA MKUU WA MKOA, CHAKAMATA WATU KADHAA MKOA WA DAR ES SALAAM

Hayo yasemwa na mkuu wa mkoa wa DSM alipokuwa katika operesheni maalum

View: https://m.youtube.com/watch?v=oHAwL1r-kfw

Mkuu wa mkoa ameyasema mbele ya mkuu wa wilaya ya kinondoni mkoani Dar es Salaam Mhe. Saad Mtambule na maofisa wa task force kufuatia hali aliyosema RC Albert Chalamila inahitaji aunde na kukiwezesha zaidi kikosi kazi / task force.

Sasa task force itajumuisha Polisi, na vikosi vingine siri kwa kuwa inaonesha kuna watu ndani ya vyombo vya umma wanahusika na magendo

RC Albert Chalamila asema atafurahi silaha atazongeza zikizaa matunda kwa kuwa dola haiwezi kuchezewa, na silaha zikitumika watu wasilaumu wala kupiga kelele.

Ukanda wa bahari wa kuanzia kusini kwa mkoa wa DSM Mpemba Mnazi hadi Bunju mpakani na Bagamoyo mkoa wa Pwani ni maeneo yanayotumika kuingiza bidhaa za magendo toka Zanzibar.

Na hili pia ni tishio la usalama, maana mbali ya magendo pia silaha, nyaraka za kichochezi, 'hela chafu' n.k zinaweza kuingizwa kwa magendo kipindi hiki tukielekea uchaguzi zikitoka Zanzibar, RC Albert Chalamila aonya.

Watuhumiwa Zaidi ya 7 Wakamatwa Dar​

Posted On: February 11th, 2024
View attachment 2901348

- RC Chalamila atangaza Operesheni kali kuendelea maeneo yote ambayo bidhaa hizo hupitishwa.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Februari 11, 2024 ametangaza kuendelea kwa Operesheni kali ya kudhibiti upitishwaji holela wa bidhaa mbalimbali za magendo katika fukwe za bahari ya Hindi ambapo amesema yoyote atakaye kamatwa adhabu kali itachukuliwa dhidi yake kwa mujibu wa sheria za nchi.

RC Chalamila amebainisha bidhaa za magendo zilizokamatwa ni mifuko ya sukari zaidi ya 100, madumu ya mafuta ya kupikia zaidi ya 700 pamoja watuhumiwa zaidi ya 7 ambapo ameagiza watuhumiwa wote wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Aidha RC Chalamila amesema bidhaa hizo zilizokamatwa zimetoka upande wa Zanzibar kuja Tanzania bara kwa kutumia mashua " Kushamiri kwa uingizaji wa bidhaa za magendo ni kulikosesha Taifa mapato lakini pia ni hatari kwa afya za binadamu kwa kuwa bidhaa hizo zinakuwa hazija pimwa ubora" Alisisitiza RC Chalamila.

Vilevile RC Chalamila amesema lazima tulinde kama tulivyo kula kiapo hatuwezi kuruhusu magendo katika Mkoa huu tuko imara sana kwa masilahi mapana ya ustawi wa jamii na amani ya Taifa hili
Ifahamike kuwa bidhaa hizo za magendo zimekamatwa usiku wa kuamkia jana Februari 10 kupitia kikosi kazi cha kudhibiti mtandao mzima wa upitishwaji wa bidhaa za magendo katika fukwe za bahari ya Hindi
Source : https://dsm.go.tz/new/watuhumiwa-zaidi-ya-7-wakamatwa-dar

wawakamate wafanyabiashara wakubwa ambao ndo waagizaji!hao vijana wanaonewa tuu
 
Zanzibar wana Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo KM KM huku Tanganyika tuna Polisi Tanzania PT kama hawa hawafanyi kazi zao eidha kwasababu ya RUSHWA nk. Hata hio "Task Force" ya Chalamila ihaitoweza kuzuia chochote.

Na atakuja Mkuu mwingine mwenye Wazfa nae ataita Vyombo vya Habari na kujifanya kakasirika kweli kweli nae ataanzisha Anti Smuggling Force kwa mbwembwe zaidi ya hizi za Chalamila.

Wakati huo tutakuwa na KMKM POLISI TANZANIA TASK FORCE na ANTI SMUGGLING FORCE nk.na nk. lakini bado Madumu na mifuko ya Sukari ya akina YAKHE yanaingia kama KAWA 😁

Na sio ajabu ukasikia Ufukwe wote Tanga hadi Mtwara wamepewa SUMA JKT😆🙌
 
Acha mufumo iliyopo iendelee kufanya kazi hata kama ni midhaifu.

Huyu mkuu wa mkoa anapenda kuanzisha vikosi visivyo rasmi, kuvipa silaha na kuviamru kufanya oparesheni, mfumo huu wa vikosi vya ulinzi visivyo rasmi ni hatari kwa nchi .State within a state.

Juzi serikali iliazimia jeshi Usu la askari la hifadhi lifutwe au lithibitiwe kwa ukaribu baada ya paramilitary/ Jeshi Usu kuleta dhahama kwa wananchi waishio jirani na misitu / hifadhi za msitu.

Leo mkuu wa mkoa anaunda task force ya kijeshi lisilo rasmi kulinda ukanda wa pwani la bahari ya Hindi lisilo na uniform, command and structure n.k Hii ni hatari.

2023 Mbunge wa Mbarali, Francis Mtega ameibua madai mazito bungeni, akiwatuhumu askari wa wanyamapori (TANAPA), kuwafanyia ukatili mkubwa wananchi, kwa madai ya kuingia hifadhini kinyume cha sheria.

Mbunge huyo akalitaka bunge lisimamishe shughuli zake kwa muda ili kuijadili hoja hiyo kwa dharura, ambapo baadaye Spika Ackson Tulia na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa walilitolea ufafanuzi.

View: https://m.youtube.com/watch?v=OLjFiQyLs7g
 
Unaunda task force kubwa wewe mkuu wa Mkoa WAKATI Kuna TISS, MAGEREZA,POLISI,UHAMIAJI TPDF.

HAWA WOTE WANAFANYA KAZI GANI NA WAKO WAPI.
Nchi hii ni ngumu sana.
Amri jeshi mkuu Yuko wapi na anafanya nini
 
12 February 2024

TASK FORCE / KIKOSI KAZI CHINI YA MKUU WA MKOA, CHAKAMATA WATU KADHAA MKOA WA DAR ES SALAAM

Hayo yasemwa na mkuu wa mkoa wa DSM alipokuwa katika operesheni maalum

View: https://m.youtube.com/watch?v=oHAwL1r-kfw

Mkuu wa mkoa ameyasema mbele ya mkuu wa wilaya ya kinondoni mkoani Dar es Salaam Mhe. Saad Mtambule na maofisa wa task force kufuatia hali aliyosema RC Albert Chalamila inahitaji aunde na kukiwezesha zaidi kikosi kazi / task force.

Sasa task force itajumuisha Polisi, na vikosi vingine siri kwa kuwa inaonesha kuna watu ndani ya vyombo vya umma wanahusika na magendo

RC Albert Chalamila asema atafurahi silaha atazongeza zikizaa matunda kwa kuwa dola haiwezi kuchezewa, na silaha zikitumika watu wasilaumu wala kupiga kelele.

Ukanda wa bahari wa kuanzia kusini kwa mkoa wa DSM Pemba Mnazi hadi Bunju mpakani na Bagamoyo mkoa wa Pwani ni maeneo yanayotumika kuingiza bidhaa za magendo toka Zanzibar.

Na hili pia ni tishio la usalama, maana mbali ya magendo pia silaha, nyaraka za kichochezi, 'hela chafu' n.k zinaweza kuingizwa kwa magendo kipindi hiki tukielekea uchaguzi zikitoka Zanzibar, RC Albert Chalamila aonya.

Watuhumiwa Zaidi ya 7 Wakamatwa Dar​

Posted On: February 11th, 2024
View attachment 2901348

- RC Chalamila atangaza Operesheni kali kuendelea maeneo yote ambayo bidhaa hizo hupitishwa.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Februari 11, 2024 ametangaza kuendelea kwa Operesheni kali ya kudhibiti upitishwaji holela wa bidhaa mbalimbali za magendo katika fukwe za bahari ya Hindi ambapo amesema yoyote atakaye kamatwa adhabu kali itachukuliwa dhidi yake kwa mujibu wa sheria za nchi.

RC Chalamila amebainisha bidhaa za magendo zilizokamatwa ni mifuko ya sukari zaidi ya 100, madumu ya mafuta ya kupikia zaidi ya 700 pamoja watuhumiwa zaidi ya 7 ambapo ameagiza watuhumiwa wote wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Aidha RC Chalamila amesema bidhaa hizo zilizokamatwa zimetoka upande wa Zanzibar kuja Tanzania bara kwa kutumia mashua " Kushamiri kwa uingizaji wa bidhaa za magendo ni kulikosesha Taifa mapato lakini pia ni hatari kwa afya za binadamu kwa kuwa bidhaa hizo zinakuwa hazija pimwa ubora" Alisisitiza RC Chalamila.

Vilevile RC Chalamila amesema lazima tulinde kama tulivyo kula kiapo hatuwezi kuruhusu magendo katika Mkoa huu tuko imara sana kwa masilahi mapana ya ustawi wa jamii na amani ya Taifa hili
Ifahamike kuwa bidhaa hizo za magendo zimekamatwa usiku wa kuamkia jana Februari 10 kupitia kikosi kazi cha kudhibiti mtandao mzima wa upitishwaji wa bidhaa za magendo katika fukwe za bahari ya Hindi
Source : https://dsm.go.tz/new/watuhumiwa-zaidi-ya-7-wakamatwa-dar

Mifuko 100 dumu 700 akatafute shughuli hapo sio ziwa viktoria au kule mbeya hapo ni mjini kweli ataondoka kama walivyokwenda wengine!
 
Wenzie wanafuata sheria na mchakato wa jeshi usu, lakini RC Chalamila anaunda makundi yenye kubeba silaha bila utaratibu:

UANZISHAJI JESHI USU
Mheshimiwa Spika, Sehemu ya Kumi ya Muswada
inapendekeza kurekebisha Sheria ya Ulinzi wa Taifa, Sura ya 192.
Inapendekezwa kutambua katika Sheria Kamati ya Mipango na
Utekelezaji ambayo ni moja ya vyombo vya juu vya utekelezaji wa
shughuli za majeshi. Lengo la marekebisho haya ni kuipa Kamati
hiyo nguvu ya kisheria. Hivyo, inapendekezwa kuongeza kifungu
kipya cha 7A kinachohusu uanzishwaji, majukumu na mamlaka ya
Kamati ya Mipango na Utekelezaji. Kutokana na mabadiliko haya,
inapendekezwa Kamati ya Ulinzi ambayo imeanzishwa kwa
mujibu wa Sheria hiyo ibadilishwe na kuwa Baraza la Ulinzi ambalo
litakuwa chombo cha juu kabisa katika masuala ya Jeshi la
Wananchi.
Mheshimiwa Spika, Sehemu ya Kumi na Moja ya Muswada

Mheshimiwa Spika, Sehemu ya Sita ya Muswada inapendekeza kufanya marekebisho katika Sheria ya Misitu, Sura ya 323. Kifungu cha 2 kinarekebishwa kwa kuongeza tafsiri ya misamiati mbalimbali ambayo imeonekana ni muhimu kutafsiriwa
ndani ya Sheria hii. Inapendekezwa pia kuongeza kifungu kipya
cha 95A ili kutambua masharti ya vifungu vya 10, 11 na 12 vya
Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori, Sura 283 kuhusu uanzishwaji
wa Jeshi Usu.
Aidha, mapendekezo haya pia yamekusudia
kuwatambua watumishi wa Wakala wa Misitu Tanzania kama
sehemu ya Jeshi Usu. Marekebisho haya yanalenga kuzingatia
uanzishwaji wa Jeshi Usu chini ya Sheria ya Uhifadhi ...

heshimiwa Spika, Sehemu ya Sita ya Muswada
inapendekeza kufanya marekebisho katika Sheria ya Misitu, Sura
ya 323. Kifungu cha 2 kinarekebishwa kwa kuongeza tafsiri ya
misamiati mbalimbali ambayo imeonekana ni muhimu kutafsiriwa
ndani ya Sheria hii. Inapendekezwa pia kuongeza kifungu kipya
cha 95A ili kutambua masharti ya vifungu vya 10, 11 na 12 vya
Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori, Sura 283 kuhusu uanzishwaji
wa Jeshi Usu. Aidha, mapendekezo haya pia yamekusudia
kuwatambua watumishi wa Wakala wa Misitu Tanzania kama
sehemu ya Jeshi Usu. Marekebisho haya yanalenga kuzingatia
uanzishwaji wa Jeshi Usu chini ya Sheria ya Uhifadhi wa
Wanyamapori.
Mheshimiwa Spika,...

Source :
MAELEZO YA MHESHIMIWA PROF. ADELARDUS L. KILANGI,
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI AKIWASILISHA MUSWADA WA
SHERIA YA MAREKEBISHO YA SHERIA MBALIMBALI WA MWAKA 2020
(THE WRITTEN LAWS (MISCELLANEOUS AMENDMENTS)BILL, 2020
KATIKA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
 
Back
Top Bottom