Albert Chalamila: Sasa naunda task force kubwa itakayokuwa na silaha

Task force ni haina maana sanasana ni kuwatajirisha hao washiriki wa task force. Acha mufumo iliyopo iendelee kufanya kazi hata kama ni midhaifu.

Spending kabisa idea ya task force kutokana na niliyoyaona wakati wa Magufuli
 
Ukweli ukanda huo hasa bunju jamaa wa kaisari walijiachia mno na hayo magendo tena ilikuwa wazi wazi na dili za mafuta ya kula hayo. Yaani mpaka unijiuliza hii nchi itakuja kuwa na jamii ya kistaarabu kweli miaka kumi ijayo?.
Hii ipo kule Kisiju na Nyamisati pia.
Serikali inajua.
Polisi wanajua.
TRA wanajua
Usalama wanajua.
 
Kwa nini wamevuliwa nguo?
 
Kama zinapita kutoka Zanzibar kuna shida gani si tumesema sisi ni nchi moja?
 
wawakamate wafanyabiashara wakubwa ambao ndo waagizaji!hao vijana wanaonewa tuu
 
Zanzibar wana Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo KM KM huku Tanganyika tuna Polisi Tanzania PT kama hawa hawafanyi kazi zao eidha kwasababu ya RUSHWA nk. Hata hio "Task Force" ya Chalamila ihaitoweza kuzuia chochote.

Na atakuja Mkuu mwingine mwenye Wazfa nae ataita Vyombo vya Habari na kujifanya kakasirika kweli kweli nae ataanzisha Anti Smuggling Force kwa mbwembwe zaidi ya hizi za Chalamila.

Wakati huo tutakuwa na KMKM POLISI TANZANIA TASK FORCE na ANTI SMUGGLING FORCE nk.na nk. lakini bado Madumu na mifuko ya Sukari ya akina YAKHE yanaingia kama KAWA 😁

Na sio ajabu ukasikia Ufukwe wote Tanga hadi Mtwara wamepewa SUMA JKT😆🙌
 
Acha mufumo iliyopo iendelee kufanya kazi hata kama ni midhaifu.

Huyu mkuu wa mkoa anapenda kuanzisha vikosi visivyo rasmi, kuvipa silaha na kuviamru kufanya oparesheni, mfumo huu wa vikosi vya ulinzi visivyo rasmi ni hatari kwa nchi .State within a state.

Juzi serikali iliazimia jeshi Usu la askari la hifadhi lifutwe au lithibitiwe kwa ukaribu baada ya paramilitary/ Jeshi Usu kuleta dhahama kwa wananchi waishio jirani na misitu / hifadhi za msitu.

Leo mkuu wa mkoa anaunda task force ya kijeshi lisilo rasmi kulinda ukanda wa pwani la bahari ya Hindi lisilo na uniform, command and structure n.k Hii ni hatari.


View: https://m.youtube.com/watch?v=OLjFiQyLs7g
 
Unaunda task force kubwa wewe mkuu wa Mkoa WAKATI Kuna TISS, MAGEREZA,POLISI,UHAMIAJI TPDF.

HAWA WOTE WANAFANYA KAZI GANI NA WAKO WAPI.
Nchi hii ni ngumu sana.
Amri jeshi mkuu Yuko wapi na anafanya nini
 
Mifuko 100 dumu 700 akatafute shughuli hapo sio ziwa viktoria au kule mbeya hapo ni mjini kweli ataondoka kama walivyokwenda wengine!
 
Wenzie wanafuata sheria na mchakato wa jeshi usu, lakini RC Chalamila anaunda makundi yenye kubeba silaha bila utaratibu:

UANZISHAJI JESHI USU

Mheshimiwa Spika, Sehemu ya Sita ya Muswada inapendekeza kufanya marekebisho katika Sheria ya Misitu, Sura ya 323. Kifungu cha 2 kinarekebishwa kwa kuongeza tafsiri ya misamiati mbalimbali ambayo imeonekana ni muhimu kutafsiriwa
ndani ya Sheria hii. Inapendekezwa pia kuongeza kifungu kipya
cha 95A ili kutambua masharti ya vifungu vya 10, 11 na 12 vya
Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori, Sura 283 kuhusu uanzishwaji
wa Jeshi Usu.
Aidha, mapendekezo haya pia yamekusudia
kuwatambua watumishi wa Wakala wa Misitu Tanzania kama
sehemu ya Jeshi Usu. Marekebisho haya yanalenga kuzingatia
uanzishwaji wa Jeshi Usu chini ya Sheria ya Uhifadhi ...

heshimiwa Spika, Sehemu ya Sita ya Muswada
inapendekeza kufanya marekebisho katika Sheria ya Misitu, Sura
ya 323. Kifungu cha 2 kinarekebishwa kwa kuongeza tafsiri ya
misamiati mbalimbali ambayo imeonekana ni muhimu kutafsiriwa
ndani ya Sheria hii. Inapendekezwa pia kuongeza kifungu kipya
cha 95A ili kutambua masharti ya vifungu vya 10, 11 na 12 vya
Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori, Sura 283 kuhusu uanzishwaji
wa Jeshi Usu. Aidha, mapendekezo haya pia yamekusudia
kuwatambua watumishi wa Wakala wa Misitu Tanzania kama
sehemu ya Jeshi Usu. Marekebisho haya yanalenga kuzingatia
uanzishwaji wa Jeshi Usu chini ya Sheria ya Uhifadhi wa
Wanyamapori.
Mheshimiwa Spika,...

Source :
MAELEZO YA MHESHIMIWA PROF. ADELARDUS L. KILANGI,
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI AKIWASILISHA MUSWADA WA
SHERIA YA MAREKEBISHO YA SHERIA MBALIMBALI WA MWAKA 2020
(THE WRITTEN LAWS (MISCELLANEOUS AMENDMENTS)BILL, 2020
KATIKA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…