Albert Mangwea (Special Thread)

Albert Mangwea (Special Thread)

Mwenyewe...!!!

Ukweli husemwa...Msiba wa Ngwair Mlitaka kuutumia Kama PR REPAIR.......Wamekufa wasanii wangapi????...
Mbona Kanumba hatukusema.....sema karibuni...mmekaliwa vibaya sana ..

Alaa...basi wale wote walioshiriki katika huo msiba wa Ngwair....kuanzia wasanii wenzake, ubalozi wa Tanzania huko Afrika Kusini, Sugu kushiriki mazishi, vituo vyote vya redio vilivyoshiriki kuutanganza msiba wake, magazeti yote yaliyoshiriki kuandika habari zake, kampuni ya Global Publishers ambayo ilitoa mchango wa shilingi milioni moja, Bongo Records ambayo ilitoa mchango wa shilingi milioni tano, na wananchi binafsi waliochangia wote hao wameutumia msiba wa Ngwair kujipa promo za kuwanufaisha wao wenyewe na si kwa nia njema tu ya kusaidia binadamu mwenzao.

Mantiki ya kijinga na kijuha sijapata kuisikia. Wangejikalia kimya na kuamua kutojihusisha mngesema, wamefanya kitu mnasema. Ama kweli malimwengu ya walimwengu hayaachi kushangaza.
 

PATHETIC FOOL!


Habari za hujafa hujaumbika hazihusiani na mtu aliyekufa kwa upumbavu wake. Sina hakika na umri wako, lkn kama umefika miaka 30 na bado hizo ndio akili zako basi umekuwa mwili na miaka lakini umri huna.

Ngwea hakufa kwa natural disaster kiasi utuonye kwamba hatujafa hatujaumbika. Huyu mtoto amekufa sababu ya kukosa maonyo. Mnapoanza kutoboa masikio, kuvaa suruali chini ya ------ na kuweka curl kwenye nywele huwa hamjui hatma yake?

Nani alikwambia kuwa ni advantage msiba wako ukihudhuriwa na watu wengi? Idiot, amsha kichwa.

Wewe unategemea aje mtakatifu kutuonya? Eti no one is perfect, YES, that is true na ndio maana nashauri tuonyane wenyewe kwa wenyewe. Mweke pema peponi hata zikisemwa na watu elfu 90, hazikusaidii kitu kwa Mungu.

Jamii ielezwe kwamba Mangwea amekufa kifo cha kijinga, sababu ya kukosa maonyo. Na kwako wewe unayeishi kwa hisia, kumsemea vizuri marehemu hakukufanyi wewe usife. Utakufa TU kwa hiyo tumia muda huu kujiwekea mazingira ya kutokufa kipumbavu kama huyu mwenzetu aliyekosa maonyo.

Duuuu!!!!!!,

Ama umeniporomoshea serukamba za kutosha yani, Kuniambia tu kwamba fool umeona kana kwamba haitoshi ukaona uniongezee na pathetic, hapo katikati ukagonga tena na Idiot,,,,, Hii mvua ya matusi hii, ama kweli mkuu alinipania.

Kutokana na unavyoandika inaonekana mwenzetu sio mjinga, kwa maana huenda ulibahatika kupata elimu nzuri na ya kiwango cha juu, au kama sivyo basi umejaaliwa tu kuwa Genius,,, Na ndio maana unakosoa watu wanaoonekana kufanya vitu visivyopendeza kwa hisia kali na matusi, yakiwemo maoni yangu.

Ninachotarajia kutoka kwako ni initiatives za namna gani tutawaokoa ndugu zetu wanaoathiriwa na madawa ya kulevya,
Ningetarajia uje na mapendekezo na au uishauri serikali na au uanzishe asasi na au NGO kwa ajili ya kutatua tatizo hilo katika jamii yetu, Badala umeng'ang'ana tu kusema upumbavu, kafa kijinga, mpumbavu aliyekufa n,k. n,k, Mimi labda kutokana na u idiot wangu au u pathetic fool wangu sijaona kwa namuna yeyote kama kitendo cha kutukana na kutoa lugha ya kuudhi kwa mtu alitengulia mbele inaweza kusaidia kutatua tatizo.

Jaribu kuelewa; sipingi kusema ukweli wa chanzo cha kifo cha marehemu, napinga matusi na lugha za kejeli kwa marehemu.

Once again, hujui ndugu utakufa kifo gani.
 
Hii tabia ya kuwa mna msifia mtu anapo kufa tuiache MANGWEA hakuwa mtu mzuri ninaimani watu alio washawishi kuingia kwenyekundi la kutumia madawa ni wengi sana, kama tulikuwa tunampenda kwa kiasi hiki, mbona tulimuacha na hakusaidiwa kama RC?,

Yale yale ya Kanumba kufia kwenye uzinzi watu wakamsifu , hopeless Tanzanians (those who cried for the sinner)!
 
Unaweza tueleza mazuri ya kwako kwanza?then tuje kwa mangwair

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kwanza umejuaje hajafa kwa "natural disaster?"

Pili, kufa kwa "natural disaster" ndo kukoje?

Tatu, hivi wewe unajua maana ya "natural disaster" kweli?



Una ithibati juu ya hilo dai lako au unaropoka tu kama mlevi wa dengerua? Kama unayo tuwekee hapa.



Wamasai wanatoboa masikio na kuvaa yale malubega yao ambapo wengine huwa hawavai hata nguo za ndani na hivyo kuziweka nyeti zao katika hali ya kuweza kuonekana kirahisi. Wao hatma yao nini?



Bila shaka yoyote wewe ndiyo jinga, zuzu, zumbukuku, na juha la majuha wote ulimwenguni. Ngwair amekufa kifo cha kijinga kwani unakijua kichomuua? Ulimfanyia wewe hiyo autopsy?



Hivi wewe unajua utakufaje hadi uanze kuhukumu vifo vya wenzio kuwa ni vya kipumbavu kana kwamba unajua kwa uhakika wa asilimia 100 kilichomuua?

Ni mtu aina gani wewe? Ebo!!

Mkuu, hivi kitufe cha "Like" kwenye hii thread wamekitoa au?
Sikioni kabisa.
 
Nakweli yeye si levo yangu, mimi na wewe tujifunze kwa huyo mnae muita matawi yajuu kwani bado tunayo nafasi ya kutubu na kumludia Mungu kabra hatujaporomoka huko juu kwenye matawi na kutumbukia shimoni. tafakari chukua hatua mpendwa mtu wa Mungu

hahahahaha! Kaka mimi muda wote nasoma comment zako ni full kucheka unavochanganya spelling l na r, kudadeki, tukianza kwenye jina lako Mapolomoko au Maporomoko? Haya kwenye quote hapo, kumludia au kumrudia? Bado na comment yako moja umeandika Urimwengu au Ulimwengu?? Hahahahaha ahsante sana kwa kuniongezea siku aisee.. Pamoja sana mkuu
 
Kumbe kinachokukera ndio hicho cha kuona mademu wamebana mat. ko na kujirusha kwenye ma pub?
Wewe unataka uwapangia watu namna ya kuishi?

Hao wadogo zako unaouliza marehemu amewafunza nini, ulishindwa kuwafunza wewe ukasubiri marehemu ndio awafunze?

Unauliza mimi ni mpagani au?,Kwani kuwa mpagani ni kosa au hairuhusiwi?, Dini yangu wewe inakuhusu nini?, Au wewe hiyo dini yako inatuhusu nini sisi?, Au nyie ndio waasisi wa udini?

Tanzania haina dini, kama unataka kulazimisha watu kufuata dini nenda kaishi VATICAN au IRANI.

Now I know the nature of a person im writing to. Enjoy the world.
 
Mimi siwezi kuongelea kuhusu jamaa maana sijui alivyokufa wala kama alikua mvuta unga sijui,
Ila kama alikufa na dhambi wote tunajua kitachofuata ni nini, kama hakufa na dhambi basi wote tunajua pia kitachofuata.
Hilo neno RIP au Mlaze mahalipema peponi ingekua vema kama lisingekua linatumika maana hakuna anayejua aliyekufa kama anastahili adhabu au maisha ya milele, anayejua ni Mungu tu. Napenda kauli ingekua MUNGU MLAZE PANAPOMSTAHILI, Na swala la kutangaza ukweli wa kifo, kama ni kweli mtu kafa kwa madawa sioni sababu ya kupindisha maelezo, ni bora liwe fundisho kuliko kudanganya mbele ya watu, fans wanaosupport mvuta madawa na kupindisha maelezo kichwani si wazima. Once again sijui jamaa alikufaje so I can't judge
 
Hakuna aliye mkamilifu mbele za Mungu. ninacho sisitiza si mtu anakufa ktk uovu badara ya kutoa onyo kwa uovuwake anaanza kusifiwa

Mkuu, wapo walio watakatifu mbele zake tena hapahapa Duniani. Zaburi 16:3
 
Shida yetu Watanzania ni UNAFIKI na kupenda kuambiwa maneno matamu huku ukweli TUNAUKATAA.

Hawa watoto tabia zao tunazijua. Tuachane na marehemu, keshaenda, sasa hivi tunaye huyu Diamond anayetoboa masikio na kuvaa ------ yako nje. Hakuna anayemkemea, ni kumsifia na kumsujudia kila anapopanda jukwaani. Siku atakapokufa, ndio tunakumbuka kuwa Mungu ni mkubwa kuliko Diamond na hapo hapo tunasahau kwamba Mungu haamrishwi.

Haka kamsemo kenu kachafu ka R.I.P kwa watu ambao uchafu wao u dhahiri ni masihara. Ni vyema kumuombea rehema na sio kumwambia Mungu amuweke mahali pema peponi. Kuna mmoja wetu ana mchango wa tofali kwenye ujenzi wa hiyo pepo?

Na wewe Black Bat, unapoambiwa matatizo yako dawa ni kuyaacha na sio kutafuta mifano kwenye matatizo ya mtu mwingine. Kama Michael Jackson hakuwa mwema sio kigezo cha Mtanzania mwenzetu Diamond kuweka ------ nje na kujichubua.

Your right bro 100%, huu ndio ukweli japo inauma.
 
Last edited by a moderator:
Shida yetu Watanzania ni UNAFIKI na kupenda kuambiwa maneno matamu huku ukweli TUNAUKATAA.

Hawa watoto tabia zao tunazijua. Tuachane na marehemu, keshaenda, sasa hivi tunaye huyu Diamond anayetoboa masikio na kuvaa ------ yako nje. Hakuna anayemkemea, ni kumsifia na kumsujudia kila anapopanda jukwaani. Siku atakapokufa, ndio tunakumbuka kuwa Mungu ni mkubwa kuliko Diamond na hapo hapo tunasahau kwamba Mungu haamrishwi.

Haka kamsemo kenu kachafu ka R.I.P kwa watu ambao uchafu wao u dhahiri ni masihara. Ni vyema kumuombea rehema na sio kumwambia Mungu amuweke mahali pema peponi. Kuna mmoja wetu ana mchango wa tofali kwenye ujenzi wa hiyo pepo?

Na wewe Black Bat, unapoambiwa matatizo yako dawa ni kuyaacha na sio kutafuta mifano kwenye matatizo ya mtu mwingine. Kama Michael Jackson hakuwa mwema sio kigezo cha Mtanzania mwenzetu Diamond kuweka ------ nje na kujichubua.
Mkuu nimependa comments zako lkn pamoja na mleta mada. Unajua sisi Watanzania hasa kizazi chetu kipya hiki ni waajabu sana. Yaani tunapenda kupakana mafuta kwa migongo ya chupa. Yani mtu anapambwa kwa sifa za ajabu mpaka unajiuliza huyu mtu kitu gani cha ajabu alichokifanya kwa watanzania hukioni. Mtu kafa kwa kuzidisha starehe lakini watu wanajifanya kupamba na kukwepesha ukweli. HUU NI UNAFIKI WA HALI YA JUU KABISA. Call a spade ''SPADE''. tuache unafiki, huyu kafa kwa madawa ya kulevya, isemwe hivyo na siyo kupamba ujinga. Hakuna alilotufundisha zuri huyu na wengine wenye tabia kama hizo. Starehe huwezi kuzikomesha, kinyume chake zitakukomesha. Tumwombee kheri Mungu amsamehe makosa yake na sisi pia tulio nyuma yake
 
mnatafuta mazuri ya ngwear, aisee kama jambo mtu haujui ni vyema ukakaa kimya waulizeni wadau wa kwenye music industry watawambia, jiulize ushawahi sikia ngwear ana beef na mtu katika maisha yake yote ya kimziki? jamani hili nalo sio zuri lakuiga kutoka kwake? ngwear amefanya collabo nyingi sana na wasanii wenzake wale wakubwa na wadogo je hili nalo sio jema la kuiga kutoka kwake? tafuteni ngoma inaitwa "jisachi" ya diamond aliyomshirikisha ngwear ni ngoma ya miaka hiyo kabla ya "nenda kamwambie" pamoja na umaarufu wake aliokuwa nao alifanya nyimbo na daimond hii yote ni katika kuhakikisha ana ananyanyua vipaji vidogo

lakini pia hata kazi sikilizeni album yake ya kwanza "aka mimi" ni one of the best hiphop album in tz kuanzia miaka hiyo hadi sasa kuna nyimbo nyingi zenye ujumbe wa kuelimisha jamii kama vile "aka mimi" iliyokuwa ikizungumzia kuhusu ukimwi, kuna "nisikilize" iliyokuwa ikihamasisha wanawake kujituma na kufanya kazi kwa bidii

jamani jamani tumtendee haki ngwear skendo zake za kusema alikuwa anatumia madawa ya kulevya zisiondoe mazuri yake aliyowahi kufanya swala la hukumu tumuachie mungu. ngwear ameondoka na skendo ya kutumia unga sawa ila embu tujiulize ni wangapi wanaondoka na maskendo makubwa na machafu kimya kimya? wangapi wanakufa huku wanadate na wanaume/wake za watu? wangapi wanakufa wakiwa wapokea rushwa wakubwa?

R.I.P ALBERT MANGWEHA

Mkuu nimekuelewa ila kumbuka:
Golikipa ukizuia dak 89 na ukaachia kizembedak ya 90 unataoneka mpumbavu mara mia ungefanya huo uzembe za mwanzoni, me na shuhuda 1 ambaye alikuw jiran kijiwe cha ngwea na wenzie walipokuwa wana vuta na kutumia madawa, sasa jiulize ni vijana wangap wameshapotea kw matumiz ya madawa?
Mkuu tafakar ki undanna sio juu juu, yeye angalau alikuw na uwezo kidogo ndio hata akaish kidogo, je hao alikuw nao hawana uwezo unajua wako wapi? Mungu atusamehe na tujitambue.
 
Wapumbavu ni wengi katika jamii kama nyumbu wa serengeti. Bahati mbaya hata baadhi ya viongozi wapo kwenye kundi hilo!
 
Na ningemshangaa angekwenda kuzika wahuni akaacha kazi yake ya safari zisizo na mwisho wala maslahi. Tusikengeuke tukawa kama wazungu, kwa akili kama hizi ndio leo tuna Sir Elton John ambaye ni mke wa mtu. Naye akifa, mtataka heshima kwake
Sioni umuhimu wa kumwita aliyetangulia mbele za haki "mhuni". After all Mwenyezi Mungu hajakupa hayo mamlaka ya kuhukumu. Unaweza ukajiona wewe sio mhuni lakini una mapungufu yako makubwa tu ambayo nayo yanatasfiriwa ni uhuni na wanaokujua.
 
Back
Top Bottom