Albert Mangwea (Special Thread)


Acha kutokwa na mapovu bro, mhuni ni mhuni tu! Kama amekufa kwa overdose ya drugs kwa usikubali au ukaa kimya tu kuliok kuendeleleza ligi isiyo na tija? Zaidi unajidhihirisha na wewe ulivyo mshabiki wa hayo madawa!!
 
mi nadhani tumwache huyu mwenzetu apumzike kwa amani.Ningefurahi kama tungetumia muda huu kuwasema wale ambao tunawafaham wanatumia na bado wanaishi.Tuwakemeee hawa kwa nguvu zote kuwaepusha kukatisha maisha yao

papaa2015 wanaoutumia madawa ya kulevya ni wahanga,wanahitaji msaada wa jamii,wabaya wetu ni wauza dawa za kulevya na wasafirishaji wake ( drug mules), nchi nyingi duniani siku hizi wakikamatwa wanatwangwa za kichwa.
 
Last edited by a moderator:
maoni yako yanafanana na avatar yako.

Hahahaha!!

Pole sana ila Ngwea kazika na watu wanaompenda na walioona mchango wake,wewe ni MNAFKI uliyejificha Nyuma ya Dini

Mtoto uzae na kumlea wewe alafu uje ulaumu watu wengine eti wamemfunza tabia mbaya ulikuwa wapi kumfunza hizo tabia ulizonazo wewe ambazo unaona ni nzuri?

Acha Roho mbaya Mungu unayemuabudu hapendi
 
Masikini TANGANYIKA unapotea kwa kukosa maarifa na kupungukiwa utukufu wa Mungu, vijana wanao kulia vijiweni, wenyekiburi, wazinzi, wafiraji, wasiotii, waongo,wenyekupenda pesa (unga) kuliko kumupenda Mungu. Baba twaomba rehema zako zituokoe zambini

Huyo Baba unaemuomba ndio kakufundisha UNAFKI na kutafuta Umaarufu kwenye Vifo vya watu?

Ngwea aliishi maisha yake na aliona yanampendeza wewe ni nani kumpangia aishi vipi?

Hii Thread ni ya ovyo kabisa kuwahi kuiona hapa hata vijana wa Lumumba wamekuzidi maarifa...
 
Upumbavu wake

Wewe huna busara unatatizo kubwa zaidi hata ya hao wala Unga,

Ungesimama na Ngwea wewe ndio ungeonekana "unajidunga" kutokana na lugha yako

Ngwea hakuitaji msaada wala huruma yako kama angeviitajia angekutafuta na usitake kulazimisha mtu ajutie au asipende kile ambacho wewe hupendi.

Dili na familia yako wasitumie Unga,na wewe ndio uwe kioo chao na waache kufata matendo ya wasanii wetu...ili kesho usije payuka tena hapa kutaka Umaarufu
 
Ndo mana Diamond haachi kufanya ufuska, kwasababu anajua atazikwa kishujaa na viongozi wote wa juu.

Kuna underground kibao wanataman wawe Ngwea au Kanumba. Ufuska na bangi kwenda mbele, wanajua mpesa ita-jam kwa kufurika misaada.
 
Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha! Wote siye marehemu watarajiwa fuaten mambo yenu mnamshobokea marehemu ebu mwacheni msimjadili
 
mnatafuta mazuri ya ngwear, aisee kama jambo mtu haujui ni vyema ukakaa kimya waulizeni wadau wa kwenye music industry watawambia, jiulize ushawahi sikia ngwear ana beef na mtu katika maisha yake yote ya kimziki? jamani hili nalo sio zuri lakuiga kutoka kwake? ngwear amefanya collabo nyingi sana na wasanii wenzake wale wakubwa na wadogo je hili nalo sio jema la kuiga kutoka kwake? tafuteni ngoma inaitwa "jisachi" ya diamond aliyomshirikisha ngwear ni ngoma ya miaka hiyo kabla ya "nenda kamwambie" pamoja na umaarufu wake aliokuwa nao alifanya nyimbo na daimond hii yote ni katika kuhakikisha ana ananyanyua vipaji vidogo

lakini pia hata kazi sikilizeni album yake ya kwanza "aka mimi" ni one of the best hiphop album in tz kuanzia miaka hiyo hadi sasa kuna nyimbo nyingi zenye ujumbe wa kuelimisha jamii kama vile "aka mimi" iliyokuwa ikizungumzia kuhusu ukimwi, kuna "nisikilize" iliyokuwa ikihamasisha wanawake kujituma na kufanya kazi kwa bidii

jamani jamani tumtendee haki ngwear skendo zake za kusema alikuwa anatumia madawa ya kulevya zisiondoe mazuri yake aliyowahi kufanya swala la hukumu tumuachie mungu. ngwear ameondoka na skendo ya kutumia unga sawa ila embu tujiulize ni wangapi wanaondoka na maskendo makubwa na machafu kimya kimya? wangapi wanakufa huku wanadate na wanaume/wake za watu? wangapi wanakufa wakiwa wapokea rushwa wakubwa?

R.I.P ALBERT MANGWEHA
 
Kama huoni mantiki mkuu,unataka kusema jamaa ni mfano wa kuigwa?
 
Equanimity beyond good and evil.

May all beings attain enlightenment.
 
Mimi ni mshaur nasaha wa kujitolea, weka wazi huyo pichani ni nani niweze kumsaidia kabla mambo hayajaharibika!
Huyo ni TID nadhani maana ameonekana mzee.na km anatumia madawa kweli anahitaji msaada ama tutampoteza japo kifo hakichagui.
 

sawa mimi nakubali kwamba yapo mabaya ya ngwear sawa pengine ni mengi ila ninachokataa ni kauli kama ya muanzisha uzi huu eti ngwear hana zuri hata moja hili ndio swala ambalo nalipinga hapa watu wanazungumza mambo kwamba ooh jamaa hakuwa na jema lolote eti kwasababu tu kifo chake kinausishwa na matumizi ya madawa ya kulevya, zis is not fear kabisa tuzungumze mabaya yake lakini pia tuache unafiki kwa kusema ngwear hajaacha jema hata moja

nimalizie kwa kuuliza hivi dhambi ni unga na bangi tu?
 
....watu mbulula wengi....

.... nothing so special Ngwea had.... unga tu.... fuata upepo wengi sana hasa Tz.... hypocrisy at best....
 
duh,huyu dada asife jamani!!bora afe huyo kaka
 
Albert mangwea (R.I.P ) ni moja kati ya wanamuziki wa kizazi kipya ambao nitawakumbuka daima katika siku za uhai wangu,sio kwamba namjua vizuri hapa ila kwa kiasi fulani ni moja ya wanamuziki ambao naweza kukaa na kumuelezea mbele ya watu hasa wasiomjua.

Huyu mwanamuziki namkumbuka sana mara ya kwanza kumuona ilikuwa 1999 ambapo kaka yangu alikuja nyumbani na album yao ya kwanza ambayo walirecord kwenye studio moja mkoani Morogoro chini ya udhamini wa mwalimu mmoja wa kikorea bila kukosea aliyekuwa anafundisha pale mazengo enzi zile masomo ya ufundi. Kipindi hicho ngwea alikuwa anaunda kundi lililokuwa likijulikana kama CFG(Chamber fleva guys) ambapo hilo kundi lilikuwa likiundwa na ngwea,mez-b ambapo kipindi kile alikuwa akijiita QG na jamaa mmoja alikuwa anaitwa maloga ambaye ndio alikuwa kiongozi wa kundi hilo ambaye yeye alikuwa akijiita malo-star.

Hapa ifahamike kuwa chamber squard imekuja baadaye baada ya maloga amajina jigine nzeku kuendelea na masomo,hapa noorah alikuwa kidato kimoja chini ya kina ngwea na dark master yeye aliwatangulia kumaliza alimaliza shule sema ndio vile kishule shule baadaye wakakutana dar na kuunda chamber squard.(nimjuavyo noorah ntaelezea siku nyingine).

Enzi hizo mez-b ambaye alikuwa anajiita QG alikuwa bishoo sana mwenyewe chini alikuwa anavaa viatu fulani kama timberland lakini vilikuwa vya manyoya kama ya mbwa hivi.hawa CFG katika hiyo album yao ya kwanza ambayo ndio ilikuwa kama mwanzo wa safari yao ya muziki iliitwa HESHIMA KWA WOTE ambao kulikuwana nyimbo kama heshima kwa wote kiburi maisha,enzi hizo mezb anarap.

Walifanikiwa kuzindua album yao katika ukumbi wa NK dodoma enzi hizo nakumbuka na miminikiwa mmoja wa watu nilioshuhudia show. Hapa ileleweke kuwa ngwea sio muasisi wa EAST ZOO sema ni mwanamuziki aliyeitangaza vilivyo kutokana na mapenzi yake kwa wana east. East zoo ilianzishwa na jamaa mmoja alikuwa anaitwa amani masinga sasa ni mkaguzi pale duwasa dodoma ambapo alianzisha EAST ZOO kutokana na bifu lake na G-SOLO ambaye yeye ndio alikuwa mwanamuziki mkubwa kipindi hicho Dodoma.siku nikipata muda nitaiongelea East zoo kadri niijuavyo.

Baada ya haponakumbuka marehemu ngwea muziki hakuwa sana alikuwa anacheza sana basket ball ambapo mwaka 2000 alifanikiwa kwenda mpaka kitaifa jijini Mwanza katika mashndano ya UMMISETA. Muda mwingialiutumia yeye kufanya mazoezi ya basket tofauti na malo star ambaye ndio alkuwa kichwakwenye kundi hilo na mez b ambaye alikuwa muuza sura enzi hizo anatembea kila siku na cd mkononi ambapo akikutana na mwanamke lazima amuonyeshe cd yao.

Baada ya ngwea kuja dar ndipo alipoanza sasa kuhustle kwenye muziki hasa baada ya matokeo yake ya form 4 kuwa sio mazuri kwani alipata divion 4 wakati darasani alikuwa ni mmoja kati ya wanafunzi vichwa sana. Bwana malo star ama nzeku yeye aliendelea na masomo hapo ndipo kundi la chamber fleva guys liliposambaratika. QG ama mez b akapata zali la kufanya chorus kwenye nyimbo ya d-knob ambayo walifanya na video ITV enzi hizo za misanya bingi, ile dili ndio ilimpelekea mez-b kupata shavu la kufanya ngoma kwa majani iliyotoka kwa jina la fikiria 2001.

Hapa 2001 noorah baada ya kumaliza shule na yeye akakacha kwenda kwao shinyanga akaja dar ambapo akapata shavu la kufanya verse kwenye nyimbo ya shega tu remix ambapo ndipo chamber squard ikaundwa baada ya kukutana wanafunzi waliomaliza mazengo miaka mbali mbali. Nakumbuka majani akawapa shavu la kutengeneza nyimbo ingine hapa walifanya nyimbo iliyoitwa ahadi ya boss ambayo majani ndipo aliponyoosha mikono kwa ngwea na kuamua kumpa mkataba.japo mkataba wenyewe ulikuwa wa kihuni (MAJANI NA VENTURE NDIO WALIOFAIDI JASHO LA NGWEA) .

Noorah alipata zali yeye la kuwa chini ya sebastian maganga ambapo ndipo alitoa nyimbo ya vijimabo. Miezi 2 kabla ngwea hajatoa geto langu . Mwezi wa 3 mwaka 2003 ambapo majani aliiachia ili ipate kuhit ngwea na yeye awe mmoja wa wanamuziki ambapo walimsindikiza juma nature katika uzinduzi wa ugali hapa ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kupanda kwenye maonyesho makubwa.ikumbukwe katika historia ya bongo fleva 2003 ndio mwaka waliotoka wanamuziki wengi zaidi ya 20 ambapo siku hizi kwa mwaka wakitoka wanamuziki wengi ni 5 (ntakuja kuwataja wanamuziki waliofanikiwa mwaka 2003).

Ngwea ntamkumbuka sana baada ya hapo alifuata na nyimbo ya napokea simu ft dullysykes. Akatoa ndani ya club akiwa amichange kiswahili ikumbukwe ngwea ndio mwanamuziki wa1 kubadilisha nyimbo ya kiingereza kuimba kiswahili.

Baada ya hapo ndipo alipotoa mikasi iliyokuwa kwenye albumya a.k.a mimithe best album up to now ikiwa na nyimbo kumi:
> Mikasi,
> a.k.a mimi ft tid
> Zawadi
> dakika 1
> weekend
> she got a gwan
> geto langu
> mademu zangu
> sikiliza
> napokea simu

Album iliuza sana ambapo kupitia ujanja wa venture aliyekuwa meneja alifanikiwa kununua gari na kujenga hapa ndipo bifu la majani na clouds lilipoanza.

Kwa leo niishie hapa maana naweza andika mpaka kesho ila ngwea ni mwanamuziki ambaye amefanya featuring na wanamuzik wengi sana karibia wote waliokuwa hot enzi hizo

Mungu amlaze maha pema ngwea mfalme wa muziki wa kizazi kipya (moyoni mwangu). Huyu ndio mwanamuziki aliyekuwa anaweza kurap,kuimba kila aina ya muziki uujuao na pia mkali wa mitindo huru na kuimba kiingereza

Kama kuna maswali wapi pa kurekebisha nilipokea unakaribishwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…