Albert Mangwea (Special Thread)

Albert Mangwea (Special Thread)

Wanafki wakujifanya wanakumbatia Biblia humu wamejaa sana...hata hiyo Biblia yenyewe hakuna wanachojua humo ndani kwasababu wao ndo wakwanza kutenda maovu...

Ngwea kazikwa na watu wanaompenda na ndo maliochangishana hizo hela zote za msiba(japo na wanafki kama wahumu walikuwepo),kasindikizwa na watu

Kama na wewe unataka ndugu yako azikwe kama Ngwea hakuna shida nani anakuzuia!

Ngwea aliamua kuishi maisha anayoona yalimfaa na wala hakuwahi kumshaur mtu aishi hayo maisha na hii habari ya msanii kioo cha jamii ni Ujinga ishi maisha yako...wote walioenda kumzika Ngwea wanakula unga...?!!

Ngwea alipenda kapendwa na ataendelea kupendwa kama inakuuma sana na wewe anza kula Madawa....HATERS!!!!!
 
Jiulize kwanza kaz ya Ngwea ilikuwa ipi??moja ya mazur aliyoyafanya ni katuburudisha sana na nyimbo zake tena sana hayo ni mazur.Ni mmoja kat ya wasanii ambao nilikuwa napenda sana kusikiliza nyimbo zake hayo ni mazur mkuu au unataka mazur yap?Kingine fwatilia 80% ya wanamzik dunian kila mtu anaskendo zake.Ngwea angekuwa anaimba nyimbo za dini hapo tungemraumu

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Mtungiiiiii!!!!!!!!!!...........Mikasi!!!!!!!!!!!!>>>> Brunt!!!!!!!!!!!!!
Je ndio yalikuwa maisha yake???????
 
Mtoa mada ni mpumbavu wa mwisho alafu anavyojishaua hapa ili aonekane anabusara ni ujinga,

Unauongelea nani kwa ukali ungeanza kutupa background ya familia yako wale wote waliokufa walikufa na nini na wewe unamema gani mpaka kumnyooshea mtu kidole?

Unataka sifa kwenye mitandao ya kijamii kwa ku-talk shyt bout others ukadhani we ni mjanja kumbe mbwiga tu

Wewe ni nani mpaka ujaji kifo cha mtu mwingine na kuongea mabaya?,Watumia Unga wapo wangapi wangapi uliwashauri??

Mburula kabisa...Kweli Mwana Mtoka Pabaya no Wonder....!!!!!
maoni yako yanafanana na avatar yako.
 
[TABLE="class: tr-caption-container, width: 1, align: center"]
[TR]
[TD]Mama wa Ngwair akizungumza na Mkuu wa Mkoa Morogoro, Joel Bendera, leo mjini Morogoro, kabla ya mazishi ya msanii huyo wa Hip Hop


[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Chunga sana wanasiasa. Wanaangalia maslahi ya kisiasa na kujionesha wanajali watu. naamini unaijua hiyo saikolojia ila unajifanya kama umeisahau vile!
 
watch yo back coz u neva know kwan we hujui aliesema usiue ndo aliesema usiseme uongo so to Him evr tng is equal acha kuyahesabu mabaya ya ngwea na ujiangalie wewe kwanza msipende kutafuta title kwenye mitandao ya kijamii mind yo own bzness
 
Kuvuta sigara, bange, cocain and the like ni tatizo la mtu binafsi na hata kunywa bia, gongo, wine, whisky and the like, lakini tabia zako ndio mazuri na mabaya yako. Hili ni sawa na ukila kunde, maharagwe, choroko, makande haitudhuru wala kutushibisha siye lakini ukinza kutoa hewa chafu ndio tunapohathirika wengine.

Mangweha umeshawahi kusikia kagombana au kawekwa ndani mara ngapi? Tukianza na wasanii wakongwe kama TID, Chidbenz, Kalapina, Duly, Afande Sele, Sugu, ProfJ, RayC na hata huyo Jide alianzaga kurusha ngumi na kurushiana maneno na hata wapenzi wake. Hivi kwani huyu alikuwa achezewi rafu? This guy need respect sio kumdisrespect kama unavyomsema.

Wewe tabia yako yakulakula tu inawachefua wenzio na hujui utakufa kwa kuvimbirwa unamsema mwenzio kafa kwa kujidunga. Acha kuhukumu usijehukumiwa na ni vyema kumsema mtu akiwa hai kuliko keshakufa unafungulia uzi ukae unamsuta marehemu. Si ajabu wewe utafia gesti tena ukiwa umeokota Ambiance kona bar
 
ata maandiko ya vitabu vyote vya Mungu vinakataza kumuhukumu marehemu, kwani hapo alipo hawezi kujitetea..mwache apumzike ata kama ukumpenda Mungu ndio atakaemuhukumu.

Hapa jeneza la Ngwair linaingizwa karubini, ikiwa ni picha inayoonyesha kuwa hatutaweza tena kukutana na msanii huyu hapa chini ya jua. R.I.P Ngwair....



Hapa watu wanakanyagana kwa ajili ya kujipanga mstari kwenda kumuaga marehemu Ngwair, katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro

Ona hii!, kwa vyovyote vile, alikuwa kipenzi cha watu.
 
Umuhimu wake ni hizo nyimbo na video zinazoonesha madem wamebana mat.ako, kuvaa minyororo shingoni, kujirusha kwenye ma pub, kutoboa masikio, na kuvaa mlegezo? kawafunza nini wadogo zetu zaidi ya kuwaharibu? hivi wewe mpagani au? hata kama, huwezi kufikiri faida na hasara? nawe utakuwa ni walewale tu wavuta unga! Uwingi wa watu kwangu ni ukubwa wa uharibifu alioufanya. (Yeye ni binadamu mwenzangu, sifurahii kifo chake bali nahoji umuhimu wake kwenye jamii!)

Kumbe kinachokukera ndio hicho cha kuona mademu wamebana mat. ko na kujirusha kwenye ma pub?
Wewe unataka uwapangia watu namna ya kuishi?

Hao wadogo zako unaouliza marehemu amewafunza nini, ulishindwa kuwafunza wewe ukasubiri marehemu ndio awafunze?

Unauliza mimi ni mpagani au?,Kwani kuwa mpagani ni kosa au hairuhusiwi?, Dini yangu wewe inakuhusu nini?, Au wewe hiyo dini yako inatuhusu nini sisi?, Au nyie ndio waasisi wa udini?

Tanzania haina dini, kama unataka kulazimisha watu kufuata dini nenda kaishi VATICAN au IRANI.
 
Kwangu mimi, kusoma wasifu wa marehemu sio WADHIFA. Na unaongea hivyo kwa kuwa hunijui hata kidogo. Sina kawaida ya kupepesa macho wala kung'ata maneno.

Hii jamii imeharibika na utandawazi kiasi mmeona kwamba, usipoweka wave kwenye nywele na kuvaa suruali chini ya ------ basi wewe hujawa kijana. Mnasifiana ujinga na kuyaacha yaliyo na tunu kwenu.

Huyu kafa kwa ujinga wake na sio kwa kukosa dawa kiasi tumzungumzie kwa hisia za kumuonea huruma. Wote tutakufa kwani kufa ni ada, lkn kufa kipumbavu ni dhalili ya utu wako mwenyewe.

Mmejazana pale uwanjani kila mmoja anasema Mungu amuweke mahali pema peponi, mnasema kwa kumaanisha au kwa mazoea?

Wakati Mandela anasema mwanae amekufa kwa ukimwi ina maana hakuwa mstaarabu? Ustaarabu na unafiki ni mambo mawili tofauti. Nikifa kesho kwa ulevi, walioko nyuma yangu na waambiwe ili wajifunze kuwa unywaji wa pombe sio 'wadhifa' bali ni upuuzi...FULL STOP; NUKTA

goooooood coment!!
 
Dunia tambala bovu! Wahenga walinena,"Hujafa hujaumbika!" Toka niwe na ufahamu wa kujua nini maana ya kifo na kushiriki misibani, mara nyingi marehemu husifiwa hata kama alikuwa mwizi,mzinzi,mchawi,mlevi n.k! Sifa hizi mara nyingi hutolewa na ndugu au jamaa ambao marehemu alikuwa anashirikiana nao katika mema au mabaya!

Ni vizuri ndugu,jamaa na marafiki wakatoa taarifa za kweli zilizosababisha kifo cha marehemu. Kwa mfano marehemu kafa kwa ukimwi,ulevi,TB,nk, hakuna sababu ya kuficha chanzo cha kifo! Nawapongeza wale wote wanaosema sababu za kweli za vifo vya wapendwa wao ili jamii iweze kujifunza.

Kuna jamaa mmoja yupo Tabata Mawenzi. Siku ya msiba alipokuwa akisoma wasifu wa marehumu dada yake,hakuona aibu kusema dada yake kafa kwa UKIMWI! Aliongea mbele ya mume wa marehemu dada yake na familia yake! Kulikuwa na ukimya mkuu sana!! Yahitaji ujasiri!

good coment!!safi sn!!
 
Nadhani hakuna tena haja ya kumzungumzia marehemu, kama ni fundisho basi limeshapatikana cha kufanya wazungumziwe waliobakia wanaotumia madawa ya kulevya ili waweze kusaidiwa nina imani wapo wanaotaka kuacha kutumia lakini hawawezi bila kusaidiwa... Mkimsema marehemu sasa hv haisaidii.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Whitney Huston amekufa kwa Cocaine maiti yake ilipelekwa mahakamani ikahukumiwa kifungo jela au kuchapwa viboko?
Usilete ulimbukeni wako hapa!
Wakati tunamchangua kaka mkuu mwaka ule kwa kura 80% alikuwa ametenda mazuri yepi?
He is just a human being!
 
mi nadhani tumwache huyu mwenzetu apumzike kwa amani.Ningefurahi kama tungetumia muda huu kuwasema wale ambao tunawafaham wanatumia na bado wanaishi.Tuwakemeee hawa kwa nguvu zote kuwaepusha kukatisha maisha yao
 
Ngwea Amepata Mazishi Ya Kishujaaa kwa Sababu amefanyiwa Sana Promo na Clouds ...Siku hizi misiba inafanyiwa Promo Kama biashara vile !!!!!!

clouds walitaka Kutumia msiba wa Ngwea particular kusafisha Taswira Yao Kwa Jamii Baada Ya Ugomvi usioisha na wasanii...lakini mwisho wa Siku hawajafanikiwa kuboresha Taswira Yao kwa jamii kupitia huu msiba..

Kuna Haja Gani ya Kutumia mamilioni kumzika Msanii ambaye hata mlo wake wa Siku alikuwa akipata kwa kuhangaika?

Ningeshangaa sana kama asingejitokeza mtu wa kuilaumu Clouds kuhusu aina ya mazishi aliyopata Ngwair.

Sasa sijui hata ukijamba nayo unailaumu Clouds....SMFH!
 
Kumbe kinachokukera ndio hicho cha kuona mademu wamebana mat. ko na kujirusha kwenye ma pub?
Wewe unataka uwapangia watu namna ya kuishi?

Hao wadogo zako unaouliza marehemu amewafunza nini, ulishindwa kuwafunza wewe ukasubiri marehemu ndio awafunze?

Unauliza mimi ni mpagani au?,Kwani kuwa mpagani ni kosa au hairuhusiwi?, Dini yangu wewe inakuhusu nini?, Au wewe hiyo dini yako inatuhusu nini sisi?, Au nyie ndio waasisi wa udini?

Tanzania haina dini, kama unataka kulazimisha watu kufuata dini nenda kaishi VATICAN au IRANI.

Haya nayo ni maoni. Tanzania ina watu.....!
 
Mimi sijakurupuka, nimekushangaa unapokomenti vitu vya ajabu ajabu, eti maiti ichapwe viboko, nilitarajia labda utakuja kuomba radhi, maana nilihisi labda umepitiwa tu.
Hujafa hujaumbika ndugu, ni Mungu pekee anayejua wewe utakufa kifo cha aina gani, kukejeli marehemu ni dalili za kutindikiwa.

PATHETIC FOOL!


Habari za hujafa hujaumbika hazihusiani na mtu aliyekufa kwa upumbavu wake. Sina hakika na umri wako, lkn kama umefika miaka 30 na bado hizo ndio akili zako basi umekuwa mwili na miaka lakini umri huna.

Ngwea hakufa kwa natural disaster kiasi utuonye kwamba hatujafa hatujaumbika. Huyu mtoto amekufa sababu ya kukosa maonyo. Mnapoanza kutoboa masikio, kuvaa suruali chini ya ------ na kuweka curl kwenye nywele huwa hamjui hatma yake?

Nani alikwambia kuwa ni advantage msiba wako ukihudhuriwa na watu wengi? Idiot, amsha kichwa.

Wewe unategemea aje mtakatifu kutuonya? Eti no one is perfect, YES, that is true na ndio maana nashauri tuonyane wenyewe kwa wenyewe. Mweke pema peponi hata zikisemwa na watu elfu 90, hazikusaidii kitu kwa Mungu.

Jamii ielezwe kwamba Mangwea amekufa kifo cha kijinga, sababu ya kukosa maonyo. Na kwako wewe unayeishi kwa hisia, kumsemea vizuri marehemu hakukufanyi wewe usife. Utakufa TU kwa hiyo tumia muda huu kujiwekea mazingira ya kutokufa kipumbavu kama huyu mwenzetu aliyekosa maonyo.
 
Ningesgangaa sana kama asingejitokeza mtu wa kuilaumu Clouds kuhusu aina ya mazishi aliyopata Ngwair.

Sasa sijui hata ukijamba nayo unailaumu Clouds....SMFH!

Mwenyewe...!!!

Ukweli husemwa...Msiba wa Ngwair Mlitaka kuutumia Kama PR REPAIR.......Wamekufa wasanii wangapi????...
Mbona Kanumba hatukusema.....sema karibuni...mmekaliwa vibaya sana ..
 
Ngwea hakufa kwa natural disaster kiasi utuonye kwamba hatujafa hatujaumbika.

Kwanza umejuaje hajafa kwa "natural disaster?"

Pili, kufa kwa "natural disaster" ndo kukoje?

Tatu, hivi wewe unajua maana ya "natural disaster" kweli?

Huyu mtoto amekufa sababu ya kukosa maonyo.

Una ithibati juu ya hilo dai lako au unaropoka tu kama mlevi wa dengerua? Kama unayo tuwekee hapa.

Mnapoanza kutoboa masikio, kuvaa suruali chini ya ------ na kuweka curl kwenye nywele huwa hamjui hatma yake?

Wamasai wanatoboa masikio na kuvaa yale malubega yao ambapo wengine huwa hawavai hata nguo za ndani na hivyo kuziweka nyeti zao katika hali ya kuweza kuonekana kirahisi. Wao hatma yao nini?

Jamii ielezwe kwamba Mangwea amekufa kifo cha kijinga, sababu ya kukosa maonyo.

Bila shaka yoyote wewe ndiyo jinga, zuzu, zumbukuku, na juha la majuha wote ulimwenguni. Ngwair amekufa kifo cha kijinga kwani unakijua kichomuua? Ulimfanyia wewe hiyo autopsy?

Na kwako wewe unayeishi kwa hisia, kumsemea vizuri marehemu hakukufanyi wewe usife. Utakufa TU kwa hiyo tumia muda huu kujiwekea mazingira ya kutokufa kipumbavu kama huyu mwenzetu aliyekosa maonyo.

Hivi wewe unajua utakufaje hadi uanze kuhukumu vifo vya wenzio kuwa ni vya kipumbavu kana kwamba unajua kwa uhakika wa asilimia 100 kilichomuua?

Ni mtu aina gani wewe? Ebo!!
 
Back
Top Bottom