Albert Mangwea (Special Thread)

Albert Mangwea (Special Thread)

So cow obama alijenga getho? Ngwair ni bonge la rapper.hapa nasikiliza aminia aliyopewa shavu na binamu!
 
Kama una akili nzuri huwezi kubisha ufalme wa Ngwea kwenye Hiphop.
Nikikumbuka alivyoichanachana biti ya majani akirap verse ya kwanza kwenye nyimbo MSELA aliyoshirikishwa na TMK Wanaume enzi hizo ni noumaaa!!!
Huwa narudiarudia verse ya Ngwea bila kuchoka.
 
Albert mangwea (R.I.P ) ni moja kati ya wanamuziki wa kizazi kipya ambao nitawakumbuka daima katika siku za uhai wangu,sio kwamba namjua vizuri hapa ila kwa kiasi fulani ni moja ya wanamuziki ambao naweza kukaa na kumuelezea mbele ya watu hasa wasiomjua.
Huyu mwanamuziki namkumbuka sana mara ya kwanza kumuona ilikuwa 1999 ambapo kaka yangu alikuja nyumbani na album yao ya kwanza ambayo walirecord kwenye studio moja mkoani Morogoro chini ya udhamini wa mwalimu mmoja wa kikorea bila kukosea aliyekuwa anafundisha pale mazengo enzi zile masomo ya ufundi. Kipindi hicho ngwea alikuwa anaunda kundi lililokuwa likijulikana kama CFG(Chamber fleva guys) ambapo hilo kundi lilikuwa likiundwa na ngwea,mez-b ambapo kipindi kile alikuwa akijiita QG na jamaa mmoja alikuwa anaitwa maloga ambaye ndio alikuwa kiongozi wa kundi hilo ambaye yeye alikuwa akijiita malo-star. Hapa ifahamike kuwa chamber squard imekuja baadaye baada ya maloga amajina jigine nzeku kuendelea na masomo,hapa noorah alikuwa kidato kimoja chini ya kina ngwea na dark master yeye aliwatangulia kumaliza alimaliza shule sema ndio vile kishule shule baadaye wakakutana dar na kuunda chamber squard.(nimjuavyo noorah ntaelezea siku nyingine).

Enzi hizo mez-b ambaye alikuwa anajiita QG alikuwa bishoo sana mwenyewe chini alikuwa anavaa viatu fulani kama timberland lakini vilikuwa vya manyoya kama ya mbwa hivi.hawa CFG katika hiyo album yao ya kwanza ambayo ndio ilikuwa kama mwanzo wa safari yao ya muziki iliitwa HESHIMA KWA WOTE ambao kulikuwana nyimbo kama heshima kwa wote kiburi maisha,enzi hizo mezb anarap.W alifanikiwa kuzindua album yao katika ukumbi wa NK dodoma enzi hizo nakumbuka na miminikiwa mmoja wa watu nilioshuhudia show. Hapa ileleweke kuwa ngwea sio muasisi wa EAST ZOO sema ni mwanamuziki aliyeitangaza vilivyo kutokana na mapenzi yake kwa wana east. East zoo ilianzishwa na jamaa mmoja alikuwa anaitwa amani masinga sasa ni mkaguzi pale duwasa dodoma ambapo alianzisha EAST ZOO kutokana na bifu lake na G-SOLO ambaye yeye ndio alikuwa mwanamuziki mkubwa kipindi hicho Dodoma.siku nikipata muda nitaiongelea East zoo kadri niijuavyo.

Baada ya haponakumbuka marehemu ngwea muziki hakuwa sana alikuwa anacheza sana basket ball ambapo mwaka 2000 alifanikiwa kwenda mpaka kitaifa jijini Mwanza katika mashndano ya UMMISETA. Muda mwingialiutumia yeye kufanya mazoezi ya basket tofauti na malo star ambaye ndio alkuwa kichwakwenye kundi hilo na mez b ambaye alikuwa muuza sura enzi hizo anatembea kila siku na cd mkononi ambapo akikutana na mwanamke lazima amuonyeshe cd yao.
Baada ya ngwea kuja dar ndipo alipoanza sasa kuhustle kwenye muziki hasa baada ya matokeo yake ya form 4 kuwa sio mazuri kwani alipata divion 4 wakati darasani alikuwa ni mmoja kati ya wanafunzi vichwa sana. Bwana malo star ama nzeku yeye aliendelea na masomo hapo ndipo kundi la chamber fleva guys liliposambaratika. QG ama mez –b akapata zali la kufanya chorus kwenye nyimbo ya d-knob ambayo walifanya na video ITV enzi hizo za misanya bingi, ile dili ndio ilimpelekea mez-b kupata shavu la kufanya ngoma kwa majani iliyotoka kwa jina la fikiria 2001. Hapa 2001 noorah baada ya kumaliza shule na yeye akakacha kwenda kwao shinyanga akaja dar ambapo akapata shavu la kufanya verse kwenye nyimbo ya shega tu remix ambapo ndipo chamber squard ikaundwa baada ya kukutana wanafunzi waliomaliza mazengo miaka mbali mbali. Nakumbuka majani akawapa shavu la kutengeneza nyimbo ingine hapa walifanya nyimbo iliyoitwa ahadi ya boss ambayo majani ndipo aliponyoosha mikono kwa ngwea na kuamua kumpa mkataba.japo mkataba wenyewe ulikuwa wa kihuni(MAJANI NA VENTURE NDIO WALIOFAIDI JASHO LA NGWEA) .

Noorah alipata zali yeye la kuwa chini ya sebastian maganga ambapo ndipo alitoa nyimbo ya vijimabo. Miezi 2 kabla ngwea hajatoa geto langu . Mwezi wa 3 mwaka 2003 ambapo majani aliiachia ili ipate kuhit ngwea na yeye awe mmoja wa wanamuziki ambapo walimsindikiza juma nature katika uzinduzi wa ugali hapa ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kupanda kwenye maonyesho makubwa.ikumbukwe katika historia ya bongo fleva 2003 ndio mwaka waliotoka wanamuziki wengi zaidi ya 20 ambapo siku hizi kwa mwaka wakitoka wanamuziki wengi ni 5 (ntakuja kuwataja wanamuziki waliofanikiwa mwaka 2003).
Ngwea ntamkumbuka sana baada ya hapo alifuata na nyimbo ya napokea simu ft dullysykes. Akatoa ndani ya club akiwa amichange kiswahili ikumbukwe ngwea ndio mwanamuziki wa1 kubadilisha nyimbo ya kiingereza kuimba kiswahili.baada yahapo ndipo alipotoa mikasi iliyokuwa kwenye albumya a.k.a mimithe best album up to now ikiwa na nyimbo kumi
Mikasi,
a.k.a mim ft tid
zawadi
dakika 1
weekend
she got a gwan
geto langu
mademu zangu
sikiliza
napokea simu

album iliuza sana ambapo kupitia ujanja wa venture aliyekuwa meneja alifanikiwa kununua gari na kujenga hapa ndipo bifu la majani na clouds lilipoanza.
Kwa leo niishie hapa maana naweza andika mpaka kesho ila ngwea ni mwanamuziki ambaye amefanya featuring na wanamuzik wengi sana karibia wote waliokuwa hot enzi hizo
Mungu amlaze maha pema ngwea mfalme wa muziki wa kizazi kipya(moyoni mwangu)
Huyu ndio mwanamuziki aliyekuwa anaweza kurap,kuimba kila aina ya muziki uujuao na pia mkali wa mitindo huru na kuimba kiingereza
Kama kuna maswali wapi pa kurekebisha nilipokea unakaribishwa
Historia nzuri sana ,hawa jamaa nawakubali mpaka kesho . R.I.P Albert ,mara ya mwisho nimekutana naye 2010 alikuwa sio mtu mwenye furaha kwa udhalimu aliofanyiwa na Venture .

Huyu Nzeku Chipa ninamfahamu sana ,namtafuta muda sasa kama una contact zake naomba uniinbox tafadhali .
 
Historia nzuri sana ,hawa jamaa nawakubali mpaka kesho . R.I.P Albert ,mara ya mwisho nimekutana naye 2010 alikuwa sio mtu mwenye furaha kwa udhalimu aliofanyiwa na Venture .

Huyu Nzeku Chipa ninamfahamu sana ,namtafuta muda sasa kama una contact zake naomba uniinbox tafadhali .

Mkuu hata sijui yupo wapi nzeku mara ya mwisho alikuwa anasoma chuo cha ushirika moshi
 
Nimeipenda hii,kumbe Majani ni kati ya watu waliomfanya Ngwea afe maskini sasa inakuwaje anawasema Cloudz?
 
Una lolote unalofaham kuhusu Huyu jamaa la kukumbukwa na kuenziwa .

Binafsi nafaham na naheshim Kwa mambo haya:-

1. Alikuwa ana uwezo mkubwa sana wa kughan mitindo huru (freestyle) kuliko msanii yeyote aliepata tokea hapa Africa mashariki.

2. Album yake ya A.k.a Mimi ni kati ya album chache kali sana kuwahi kutokea ktk historia ya music wa bongo.

3.Aliipaisha sana Dodoma, ,Area C na east zoo kupitia muziki ,kiasi cha kufanya Dom ikawa inasomeka kwenye Raman ya muziki ,Morogoro ambapo familia yao ilikuwepo na alipokuja zikwa pamoja na Songea chimbuko la ukoo wake kulibak undercover.

4 . Alikuwa mtu wa watu ,with friends waliokuwa wanamthamin sana.

5. Kama binadamu alikuwa na mapungufu yake .lakin hayafanyi niache kumpa heshima yake kila naposikiliza nyimbo zake na kukumbuka uwezo mkumbwa aliokuwa nao.

Pumzika unapostahili brother. Cowbama.
 
Noorah nilimkubali sana zamani kuliko Ngwea!
R.I.P Mangwea
 
Noorah nilimkubali sana zamani kuliko Ngwea!
R.I.P Mangwea

Kwa sauti na style Walipoanza Noorah alikuwa mkali.sema Heshima inakuja Kwa Ng wair uwezo Wake wa kuchange styles za michano , freestyle ulikuwa wa kipekee sana.
 
Kwa matumizi ya bangi madawa ya kulevya na kutoheshimu elimu hivyo hafai kuigwa lakini pia ni muwekezaji kipindi kileeeee alikuwa na bar karibu na lion hotel
 
Angekua mchezaji wa mpira basi anacheza namba zote kuanzia kipa paka forward...ntamkumbuka sana kuna mstari wake 1 alisema siku nikifa pengo halita zibika ni kweli kabisa RIP ngwea

Sent from my BlackBerry 9790 using JamiiForums
 
Nlposkia ngwear katutoka dunian nlitokwa na choZ.nlkuwa nampenda sana mangwear.nlkuwa nampenda alvyokuwa akiimba hasa akchana kwa ki inglishi..nyimbo yake ya.Alma inankumbusha enz zake nyingi.na nnapenda kumquote mistar yake kama vle "hukuwepo wakat nazsaka, so usinpangie kuspend.""cow obama, cow bwoy" rest in peace kaka.mbele yetu nyuma yako.nampenda sana ngwear, he still live inside me.
Return
If
Possible
 
Nlposkia ngwear katutoka dunian nlitokwa na choZ.nlkuwa nampenda sana mangwear.nlkuwa nampenda alvyokuwa akiimba hasa akchana kwa ki inglishi..nyimbo yake ya.Alma inankumbusha enz zake nyingi.na nnapenda kumquote mistar yake kama vle "hukuwepo wakat nazsaka, so usinpangie kuspend.""cow obama, cow bwoy" rest in peace kaka.mbele yetu nyuma yako.nampenda sana ngwear, he still live inside me.
Return
If
Possible

Napenda " we Ngwair mbona huinekani?, vp hauna TV ,ungekuwa na faida nami ungeniona kwa 3D"

Kwenye wimbo No beef ft TID
 
Mwenye Tshirt au anaejua zinapouzwa zile zmeandikwa RIP NGWAIR(BLACK) naomba aniPM.Nahitaji
 
Kwa matumizi ya bangi madawa ya kulevya na kutoheshimu elimu hivyo hafai kuigwa lakini pia ni muwekezaji kipindi kileeeee alikuwa na bar karibu na lion hotel

We ni ----- na Zezeta mkubwa kama Mabwege na Mazezeta wengine.
 
Back
Top Bottom