Albert Msando ‘amwaga’ vifaa vya Corona kwa wanahabari Arusha, adai hali ni mbaya sana

Albert Msando ‘amwaga’ vifaa vya Corona kwa wanahabari Arusha, adai hali ni mbaya sana

Huu ndiyo ukweli na busara, serikali yetu haina mikakati ya kupambana na Corona ila kujilinda wao kisiasa, sababu wanalinda uchumi ili wasishindwe kwenye uchaguzi sababu ya uchumi mbaya wakati dunia nzima imeathirika kiuchumi.

 
Tunakwenda pabaya na kipimo cha uongozi tulionao ni covid19.
 
Mwandishi wa habari atapata wapi mamlaka ya kutoa habari ya Corona? Wakati Kuna mamlaka zilizopewa jukumu.?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nionavyo mimi,waandishi wengi wa habari wa siku hizi sio watafutaji wa habari.Wengi wanasubiri kupewa habari ya kupublish iliyotayarishwa yeye anairusha tu.Hii inapelekea wananchi kufuatilia kupata habari wenyewe.Na ukifuatilia kwa asilimia kubwa utagundua zina ukweli.

Kazi ya waandishi wa habari haina mipaka.Sio taarifa zote Serikali inaweza kuzipata kwa haraka kutokana na hali halisi ya Nchi yetu hasa ukubwa wa vijiji,kaya,kata.wilaya,mkoa.Waandishi wa habari wapo kila mahali.Watoe taarifa kwa wananchi.Pale inapobainika sio za kweli wachukuliwe hatua kwa taratibu za kazi zao.

Na sio mwandishi wa habari,anakutana na mshimo mkubwa umechimbika katikati ya main road akatahadharisha watumiaji,kwake ikawa shida.Kuna umuhimu mkubwa kupitia umoja wa waandishi kuwa na umoja wa kusimamia wanachotakiwa kuripoti bila kuingiliwa na kitu chochote.

Katika hili swala kila mtu analichukua kwa jinsi lilivyomgusa.Mwingine ameondokewa na wapendwa wake wawili au watatu kwenye jamii.Kwa hili tayari kwake hali ni mbaya.Ataendelea hivyo kuwa hali ni mbaya.Akasikia tena kwa jirani kuwa kaondoka mtu bado atasema hali ni mbaya.Sio kwamba watu hawasemi kuwa hali ni mbaya,tofauti tu ni nani kasema na anamwonekano gani katika jamii na kasemea wapi.

Ukweli kama serikali inavyotangaza ugonjwa upo watu wanaondoka tuendelee kupeana elimu.Na Mungu atunusuru.
 
Back
Top Bottom