BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Msando amesema hayo Mkoani Morogoro wakati akifungua Mafunzo ya siku mbili kwa wanahabari kuhusu namna Bora ya kutoa habari ambayo yameratibiwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania -THRDC, Julai 12, 2022
Aidha, Mkuu huyo Wilaya amewataka wanahabari kujitahidi kuwa watetezi wa Haki za Binadamu bila ya kuwa mashabiki wa kuegemea upande mmoja ili kuepukana na changamoto mbalimbali.
Amesema waandishi wa habari wanapozungumza Masuala ya Haki za Binadamu wasiwe wazito kwa kutozitoa badala yake waangalie mzani na ukweli katika kuhabarisha umma juu tukio wanalotaka kuliripoti.
Naye Jaji Mstaafu Robert Makaramba amewasilisha mada ya wanahabari namna ya kuandika na kuripoti habari za kwenye Mahakama kuwa ni vyema wakaepuka kutoa taarifa ambazo hazijatolewa mahakamani ili kuepusha sintofahamu kwenye jamii.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Albert Msando
Awali akizungumza Wakili Kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu – THRDC, Leopold Mosha amesema mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari namna ya kuandika ma kuripoti taarifa zinazohusiana na haki za Binadamu.
Wakili Mosha amesema kuwa Moja ya majukumu ya Asasi za Kiraia ni kufanya uchechemuzi wa kujua na kupata ufahamu wa Masuala mbalimbali yanayohusu Haki za Binadamu.
Hata katika mafunzo hayo ambayo yanatarajiwa kumalizika Julai 13, 2022 wanahabari wamesisitizwa kutumia fursa hiyo kujiongezea maarifa katika ufanyaji wao wa kazi.
Source: Torch