GE2025 Alex Msama: Mtumishi wa watu mwenye dhamira ya kweli aliyebeba hatima njema ya wananchi wa Ukonga!

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Jina la Alex Mwita Msama halihitaji utambulisho wa makelele mengi.

Alex Msama ameweka alama na nembo isiyofutika katika jamii ya Watanzania. Ameibua , kukuza na kuendeleza vipaji vya wengi kupitia muziki wa Injili.

Kwa miaka mingi, Alex Msama amekuwa kielelezo na mfano hai katika kumtumikia Mungu kwa kuinua na kusaidia waimbaji wa nyimbo za Injili ndani na nje ya nchi.

Leo, sitaki kugusia sana masuala ya nyimbo za Injili,. Lakini ni vyema kuweka kumbukumbu sawa, kwamba katika huduma ya Neno la Mungu kupitia nyimbo za Injili hapa nchini, 'kapteni' na rubani ni Alex Msama.
Tusisahau; unapotaja majina makubwa katika ulingo wa Nyimbo za Injili, kama Rose Muhando, Bahati Bukuku, Jennifer Mgendi, Christopher Mwahangila na wengine wengi, wameufikisha mbali muziki wao wa Injili kupitia 'sapoti' kubwa kutoka kwa Alex Msama.

Alex Msama ni mtumishi wa Mungu katika Roho na Kweli. Matendo yake kwa jamii ni utambulisho na uthibitisho wa hiki ninachokieleza hapa.

Hakuna Mtanzania mtu mzima, mwenye akili timamu asiyejua na kutambua nguvu na matokeo chanya ya Tamasha la Pasaka.

Kwa miaka mingi, Alex Msama amegusa mioyo ya watu wengi, bila kujali dini, ndani na nje ya nchi, kupitia Tamasha la Pasaka.

Kwa miaka mingi, waimbaji wa nyimbo za Injili, wamekuwa wakijipatia riziki nono kupitia Tamasha la Pasaka, huku waimbaji wakubwa kutoka nje ya nchi, nao wamekuwa wakineemeka kupitia Tamasha la Pasaka! Hakika Alex Msama 'ni mtu na nataka'!

Tamasha la Pasaka, hakika limekuwa daraja na kiunganishi kikubwa kati ya wananchi na viongozi wakubwa, katika ngazi mbalimbali.

Alex Msama, kupitia Tamasha la Pasaka, amewakutanisha wananchi na viongozi kama marais, mawaziri wakuu, mawaziri, mabalozi na wakuu wa nchi mbalimbali kutoka Barani Afrika.

Marais kama Hayati Benjamin William Mkapa, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mabalozi wengi waandamizi kutoka nje ya nchi, kwa nyakati tofauti wamejumuika na wananchi kupitia Tamasha la Pasaka.

Alex Msama hana maneno mengi. Ni mkimya, mpole asiye na makuu. Ni mtu mwenye hofu kubwa ya Mungu.
Msama akiona mtu yupo katika shida ya uhitaji, moyo wake hububujikwa na machozi ya huruma. Nitaandika mengi kuhusu ALEX MWITA MSAMA.

Tamasha la Pasaka, halipo kwa ajili ya maslahi binafsi ya Alex Msama, bali Tamasha hili limekuwa nuru na faraja kwa Watanzania wengi wenye uhitaji maalum.

Alex Msama, kupitia Tamasha la Pasaka, amekuwa akitoa misaada mbalimbali ya mahitaji muhimu ya kibinadamu, kupitia mapato ya Tamasha la Pasaka.
Alex Msama, bila kuwa na nafasi yoyote ya uongozi seriklini, lakini amekuwa msaada mkubwa kwa jamii ya Watanzania.

Zipo taarifa zisizokuwa na shaka kwamba, asilimia kubwa ya mapato yaliyotokana na Tamasha la Pasaka, Msama amekuwa akijitolea kusaidia jamii ya watu wenye uhitaji. Mfano?; watoto yatima, wazee wasiojiweza na wagonjwa wenye vipato vya chini. Huyu ndiye Alex Msama ninayemfahamu.

Mara kadhaa, nimefanya naye mahojiano juu ya maendeleo na ufanisi wa Tamasha la Pasaka na ukuzaji wa muziki wa Injili.

Msama ni mtu mwenye huruma, hili naweza kulithibitisha mahali popote duniani. Naweza.
Alex Msama anayajua maisha. Anajua shida na changamoto za maisha. Ametoka katika maisha duni, yenye mahangaiko mengi!

Msama anazijua shida nyingi za wananchi, ameziishi kwa vitendo na mateso makubwa!
Msama anapozungumza kutatua shida za wananchi, anamaanisha kutoka moyoni. Haigizi.
Alex Msama hajatoka katika maisha ya mboga saba, hapana. Msama ametoka kwenye maisha ya kula ugali kwa chumvi!

Amelala kwenye ngozi ya Ng'ombe, ameenda shule bila viatu. Msama amesota na maisha, anazijua shida na shurubu za Watanzania wa kipato cha chini!
Palipo na mafanikio au jambo lolote jema, changamoto hazikosi!

Alex Msama amekumbana na maswaibu mengi. Msama amepakwa matope mengi na kila aina ya uchafu!
Alex Msama amekwepa mishale mingi! Amesingiziwa mengi mabaya! Ameitwa kila aina ya majina yasiyofaa, ametukanwa kila aina ya matusi ya kufedhehesha!

Maadui na wafitinishi, wamefanya kila mbinu kwa kuzusha na kusingizia skendo nyingi za hivyo. Lengo ni kumkatisha tamaa na kumvunja moyo Msama. Lakini amekuwa imara na mwenye ngozi ngumu huku akisonga mbele!

Mwaka huu (2025), Alex Msama ametia nia kuwania ubunge katika Jimbo la Ukonga, Ilala Dar es Salaam.
Muda wa kampeni ukifika, nitaandika mengi, lakini kwa hapa itoshe tu kusema, wananchi wa Ukonga watapata mwakilishi wa kweli, kama watafanya uamuzi wa kumpitisha Alex Msama, kuwa Mbunge wao.
Simaanishi kuwa watia nia wengine hawafai, hapana. Nimeandika kuhusu Alex Msama, kadiri ninavyomfahamu, kama Mwandishi wa Habari.

Kwa leo, niishie hapa, kampeni zikianza, nina mengi mazuri ya Alex Msama. NITAANDIKA kwa kirefu. Subiri, Msama ameitendea haki nchi yetu katika kuimarisha na kudumu Umoja, Amani, ushirikiano na Muungano, kwa njia ya kuabudu.
C&PView attachment 3411268
Nikiona maana huwa Malia kabisa..Ni takataka kabisa..huyu Ni tapeli hata mahakama inamjua
 
Rose Muhando kidogo afe masikini. Jitu halina hata huruma. Labda kwa vile CCM ni chama cha....ila hili jamaa linapaswa kuwa ndani!
 
Usitudanganye unatafuta kwa ajili ya tumbo lako na familia yako. Huu ni muda muafaka madaraka yawe kwa mzunguko miaka 5 inatosha na wengine tufaidi. Hizo swaga za eti kutuletea maendeleo lipo kwenye mipango ya nchi na sio wewe mbunge wala mwenyekiti wa Kijiji, kitongoji au mtaa.Tuamke watanzania tusidanganywe na kudanganyika
Yaani hawa kwa sasa ni waajiriwa wa serikali
 
Jina la Alex Mwita Msama halihitaji utambulisho wa makelele mengi.

Alex Msama ameweka alama na nembo isiyofutika katika jamii ya Watanzania. Ameibua , kukuza na kuendeleza vipaji vya wengi kupitia muziki wa Injili.

Kwa miaka mingi, Alex Msama amekuwa kielelezo na mfano hai katika kumtumikia Mungu kwa kuinua na kusaidia waimbaji wa nyimbo za Injili ndani na nje ya nchi.

Leo, sitaki kugusia sana masuala ya nyimbo za Injili,. Lakini ni vyema kuweka kumbukumbu sawa, kwamba katika huduma ya Neno la Mungu kupitia nyimbo za Injili hapa nchini, 'kapteni' na rubani ni Alex Msama.
Tusisahau; unapotaja majina makubwa katika ulingo wa Nyimbo za Injili, kama Rose Muhando, Bahati Bukuku, Jennifer Mgendi, Christopher Mwahangila na wengine wengi, wameufikisha mbali muziki wao wa Injili kupitia 'sapoti' kubwa kutoka kwa Alex Msama.

Alex Msama ni mtumishi wa Mungu katika Roho na Kweli. Matendo yake kwa jamii ni utambulisho na uthibitisho wa hiki ninachokieleza hapa.

Hakuna Mtanzania mtu mzima, mwenye akili timamu asiyejua na kutambua nguvu na matokeo chanya ya Tamasha la Pasaka.

Kwa miaka mingi, Alex Msama amegusa mioyo ya watu wengi, bila kujali dini, ndani na nje ya nchi, kupitia Tamasha la Pasaka.

Kwa miaka mingi, waimbaji wa nyimbo za Injili, wamekuwa wakijipatia riziki nono kupitia Tamasha la Pasaka, huku waimbaji wakubwa kutoka nje ya nchi, nao wamekuwa wakineemeka kupitia Tamasha la Pasaka! Hakika Alex Msama 'ni mtu na nataka'!

Tamasha la Pasaka, hakika limekuwa daraja na kiunganishi kikubwa kati ya wananchi na viongozi wakubwa, katika ngazi mbalimbali.

Alex Msama, kupitia Tamasha la Pasaka, amewakutanisha wananchi na viongozi kama marais, mawaziri wakuu, mawaziri, mabalozi na wakuu wa nchi mbalimbali kutoka Barani Afrika.

Marais kama Hayati Benjamin William Mkapa, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mabalozi wengi waandamizi kutoka nje ya nchi, kwa nyakati tofauti wamejumuika na wananchi kupitia Tamasha la Pasaka.

Alex Msama hana maneno mengi. Ni mkimya, mpole asiye na makuu. Ni mtu mwenye hofu kubwa ya Mungu.
Msama akiona mtu yupo katika shida ya uhitaji, moyo wake hububujikwa na machozi ya huruma. Nitaandika mengi kuhusu ALEX MWITA MSAMA.

Tamasha la Pasaka, halipo kwa ajili ya maslahi binafsi ya Alex Msama, bali Tamasha hili limekuwa nuru na faraja kwa Watanzania wengi wenye uhitaji maalum.

Alex Msama, kupitia Tamasha la Pasaka, amekuwa akitoa misaada mbalimbali ya mahitaji muhimu ya kibinadamu, kupitia mapato ya Tamasha la Pasaka.
Alex Msama, bila kuwa na nafasi yoyote ya uongozi seriklini, lakini amekuwa msaada mkubwa kwa jamii ya Watanzania.

Zipo taarifa zisizokuwa na shaka kwamba, asilimia kubwa ya mapato yaliyotokana na Tamasha la Pasaka, Msama amekuwa akijitolea kusaidia jamii ya watu wenye uhitaji. Mfano?; watoto yatima, wazee wasiojiweza na wagonjwa wenye vipato vya chini. Huyu ndiye Alex Msama ninayemfahamu.

Mara kadhaa, nimefanya naye mahojiano juu ya maendeleo na ufanisi wa Tamasha la Pasaka na ukuzaji wa muziki wa Injili.

Msama ni mtu mwenye huruma, hili naweza kulithibitisha mahali popote duniani. Naweza.
Alex Msama anayajua maisha. Anajua shida na changamoto za maisha. Ametoka katika maisha duni, yenye mahangaiko mengi!

Msama anazijua shida nyingi za wananchi, ameziishi kwa vitendo na mateso makubwa!
Msama anapozungumza kutatua shida za wananchi, anamaanisha kutoka moyoni. Haigizi.
Alex Msama hajatoka katika maisha ya mboga saba, hapana. Msama ametoka kwenye maisha ya kula ugali kwa chumvi!

Amelala kwenye ngozi ya Ng'ombe, ameenda shule bila viatu. Msama amesota na maisha, anazijua shida na shurubu za Watanzania wa kipato cha chini!
Palipo na mafanikio au jambo lolote jema, changamoto hazikosi!

Alex Msama amekumbana na maswaibu mengi. Msama amepakwa matope mengi na kila aina ya uchafu!
Alex Msama amekwepa mishale mingi! Amesingiziwa mengi mabaya! Ameitwa kila aina ya majina yasiyofaa, ametukanwa kila aina ya matusi ya kufedhehesha!

Maadui na wafitinishi, wamefanya kila mbinu kwa kuzusha na kusingizia skendo nyingi za hivyo. Lengo ni kumkatisha tamaa na kumvunja moyo Msama. Lakini amekuwa imara na mwenye ngozi ngumu huku akisonga mbele!

Mwaka huu (2025), Alex Msama ametia nia kuwania ubunge katika Jimbo la Ukonga, Ilala Dar es Salaam.
Muda wa kampeni ukifika, nitaandika mengi, lakini kwa hapa itoshe tu kusema, wananchi wa Ukonga watapata mwakilishi wa kweli, kama watafanya uamuzi wa kumpitisha Alex Msama, kuwa Mbunge wao.
Simaanishi kuwa watia nia wengine hawafai, hapana. Nimeandika kuhusu Alex Msama, kadiri ninavyomfahamu, kama Mwandishi wa Habari.

Kwa leo, niishie hapa, kampeni zikianza, nina mengi mazuri ya Alex Msama. NITAANDIKA kwa kirefu. Subiri, Msama ameitendea haki nchi yetu katika kuimarisha na kudumu Umoja, Amani, ushirikiano na Muungano, kwa njia ya kuabudu.
C&PView attachment 3411268
Sawa ila kura hapati
 
Comments za awali hakika zimekamilisha hili la " JF the home of great thinkers " mleta mada hii ndo tunaita kuchamba kwingi...! Hii nchi kwa ilipofikia aina ya watu hasa viongozi na wasimamizi wa mambo kama alex wengi sana! nina uhakika huyu kashindwa kula vizuri na wenye mamlaka na ndiyo maana kaangushiwa jumba bovu
 
Kaangushiwa jumba bovu gani?

Ova
 
Back
Top Bottom