Algeria vs taifa stars

Nao ZNZ wakiongozwa na Waziri Shamhuna wamekwisha kwenda Zurich yalipo makao makuu ya FIFA wakiomba wawe wanachama huru ili wapeleke timu yao kwenye mashindano ya AFRICA na KOMBE LA DUNIA;wanataka kutambulika kama shirikisho huru la soka na wao!

sasa kama na mikoa inataka kuomba uanachama fifa hii sasa ni baraaa kubwa, basi na mwanza nao waombe tehe tehe heeeeeee
 
Junius;

Naoma ufafanuzi wako,wale Mafirauni wa Misri ya kale ina maana hawakuwa waarab?
Waarabu wamekuja Misri karne nyingi sana baada ya Mafirauni kuondoka, Mkuu wewe google tu kama una shaka.
anakurupuka tu shauri ya ilimu yake kuwa ya magumashi, hajui hata analoliongea huyu
haya wewe mwenye elimu twambie huo uhusiano wa waarabu na mafirauni?
 
Mafirauni wa kale walikuwa waafrika weusi ndugu yangu Anyisile obheli, soma historia usiseme usiyoyajua.
wewe nawe unaongea nini? kwa kuwa waafria ndiyo kuliwanyima kuwa waarabu kwa utaifa? nyie ni vipi? nani kawambia kuwa uarabu ni weupe?
 
Waarabu wamekuja Misri karne nyingi sana baada ya Mafirauni kuondoka, Mkuu wewe google tu kama una shaka.

haya wewe mwenye elimu twambie huo uhusiano wa waarabu na mafirauni?
hizo ni elimu zenu za michenzani tu
 
hizo ni elimu zenu za michenzani tu

Anyisile unajua historia wewe? mafirauni walikuwa waafrika weusi, niambie waarabu walivamia mwaka gani misri na mafirao walianza mwaka gani.Bila shaka hujui na sitashngaa kwamba hujui.

Jibu sasa hivi , waarabu walivamia misri mwaka gani?
himaya za mafirauni zilianza mwaka gani?
 
Mkuu huyu 'mlokole' atakusumbuwa, muulize habari za misukule atamwaga razi sasa ivi hapa...historia wapi na wapi!!
 
Mtabishaana na mshindi hapatikani! Turudi kwenye sehemu ya msingi Tanzania 1- 1 Algeria... Kazi wakija kwetu...
 
Mtabishaana na mshindi hapatikani! Turudi kwenye sehemu ya msingi Tanzania 1- 1 Algeria... Kazi wakija kwetu...

Enhee...tuendeleeni sasa...kwa ari ile waliyonayo wachezaji mechi za nyumbani nawapa advantage kubwa ya kushinda
 
Kwa michezaji yetu ilivo milevi siwezi ku guarantee kushinda wakija
 
Bravo Taifa Stars..............

Sikuamini macho yangu jana nilivyowaona Stars wanavyocheza. Kwanini nasema hivyo kwa sababu:

1. Algeria huwezi kabisa kuilinganisha na Tanzania lakini Taifa Stars walivyocheza wamenipa faraja sana. Kumbuka Algeria walikuwa World Cup na katika hali ya kawaida algeria walitakiwa washinde.
2. Wachezaji walikuwa na confidence ya kutosha kitu ambacho sijategemea kutoka Taifa Stars.
3. Tulifanya mashumbulizi yenye akili kuliko Algeria wenyewe na Build up ya Taifa Stars ya kufika golini alikuwa fantastic!!!

Bravo Taifa Stars nina Imani Kubwa Poulsen ataifikisha mbali sana Stars.................
 
Kwa kweli kiwango tulichoonyesha ni cha kujivunia sana I am sure hata timu ikirudi home watapewa motisha. Impact ya professional players like Nizar anayecheza Canada ilionekana wazi pale kati, Danny Mrwanda anayeshezaVietnam alishirikiana vema na Ngassa kushambulia kwa kushtukiza,Henry Joseph anayekipiga Norway alingara kwenye dimba la kati kama defensive midfielderna hata Idrisa wa Sofapaka ya Kenya nae alicheza vizuri sana.Pia kocha huyu inabidi asibweteke na wachezaji wa Yanga na Simba pekee maana kipa Kado wa Mtibwa kama sikosei amecheza vizuri sana alikuwa na confidence golini, mipira ya adhabu alikuwa anaitime vizuri na kuiokoa na hata mashti ya kushtukiza aliyacheza na kuwapaga vyema mabeki wake. Tulicheza kwa kujihami maana tupo ugenini na mara tu Nizar au Henry Joseph walipopokonya mipira mara chache walijaribu kupeleka mbele kwa Ngassa na Mrwanda ambao wote wana kazi kujaribu kushambulia. Nadhni tukicheza nyumbani tutaendeleza ari ile ile na kushambulisa sana kwa malengo na ama kwa hakika tutapata matokeo mazuri, mwisho yule refa wa Togo hakuchezesha fair alitoa faulo nyingi sana langoni mwetu zilizozaa kona zaidi ya 20 na hata pale wachezaji wetu walipofanyiwa faulo yeye alieleleza kwetu mpaka kocha Poulsen alikuwa akitikisa kichwa muda mwingi wa mchezo kwa kutokubaliana na maamuzi ya mchezo. Timu inabidi iwe hii japo kwenye safu ya ushambuliaji kocha anaweza kumpumzisha Mrwanda na Babi na kuwaingiza Boko na Mgosi ili walete chachu ya kutafuta mabao hasa kipindi cha pili. Ngoja tusubiri kocha Poulsen atauzungumziaje mchezo ule na yapi atafanya kuboresha timu kwa mechi zinazofuata.
 
Mkuu karibu tena ututabirie mchezo unaofuata maana naona uko makini kwelikweli.

Hawa wa diziani hizi ndio walewale wanaoshabikia soka la wanaume wenzao kule England na Spain wanachangia hata Ronaldo au Roonay akikohoa huku kwenye kuonyesha uzalendo hutawaona na hata ukiwaona wanatoa utabiri mbovu kwa manajidai wanaijua sana Taifa stars ya kufungwa fungwa ovyo pasi kujua kuwa hata sie taifa dogo kisoka tunakuwa taratibu.
 
Bravo Taifa Stars, wakija bongo hawatatoka jamani tuwaombee wachezaji na kocha maana mpira siku zote ni spiriti ya wachezaji. T,stars wakicheza kama timu nina uhakika hawa waarabu hawatatoka, mzee wa kudondoka dondoka nina uhakika atakuwa naye ndani na nyuma, ila pale hatadondoka nina uhakika.,yy kwake jagwani tu
 
Mkuu karibu tena ututabirie mchezo unaofuata maana naona uko makini kwelikweli.

Hawa wa diziani hizi ndio walewale wanaoshabikia soka la wanaume wenzao kule England na Spain wanachangia hata Ronaldo au Roonay akikohoa huku kwenye kuonyesha uzalendo hutawaona na hata ukiwaona wanatoa utabiri mbovu kwa manajidai wanaijua sana Taifa stars ya kufungwa fungwa ovyo pasi kujua kuwa hata sie taifa dogo kisoka tunakuwa taratibu.
 
Hivi MAXIMO alikuwa hamuoni huyu dogo Shaban Kado,nashangaa na hao wabongo walioko kwenye benchi la ufundi walikuwa hawamjui huyo dogo hadi Maximo anamchagua yule kipa ***** anayecheza Msumbiji.
Kwa sasa mpira tuanuweza lakini fitina hatuziwezi
 
http://news.bbc.co.uk/sport2/hi/football/africa/8968999.stm

Tanzania hold Foxes in Algiers in Nations Cup qualifier



Saadane's Foxes looked a pale shadow of their World Cup side

Tanzania halted Algeria's confident bandwagon in its tracks as they held them to a 1-1 draw in their opening 2012 Africa Cup of Nations qualifier in Algiers on Friday.
The Taifa Stars threatened to spring a major shock in the Group D game on 33 minutes when striker Jerson Tegete fired home a free-kick from 30-yards.
But Adlene Guedioura's goal on the on the stroke of half-time earned a draw for the 2010 World Cup finalists coached by Rabah Saadane.
The Desert Foxes looked a pale shadow of the side which harried and hassled England so effectively at the World Cup two months ago.
Tanzania packed their midfield with combative tacklers, which frustrated the North Africans but also removed almost any trace of attacking threat from the Algerians.
The Desert Foxes dominated possession after the break and created a number of chances - but Tanzania's tough and resolute approach merited a reward.
Morocco play Central Africa in group's other game on Saturday.

angalau tunaonekana na kusifika Mungu ibariki Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…