Alhamisi 50% Simba SC atafungwa au 50% atatoka Sare na Prisons FC, kwani Wachezaji Waandamizi watamchomesha Kusudi ili afukuzwe

Alhamisi 50% Simba SC atafungwa au 50% atatoka Sare na Prisons FC, kwani Wachezaji Waandamizi watamchomesha Kusudi ili afukuzwe

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kwa niliyohakikishiwa GENTAMYCINE kwa wale Wenzangu ( wana Simba SC ) nawaombeni Mechi ya Alhamisi ya Simba SC dhidi ya Prisons FC msiende na Matokeo yenu na mjiandae mapema Kisaikolojia kwani kuna Miwili Kufungwa au kutoka Sare ila Kushinda tusahau labda tu Mpango huu Usitishwe rasmi Usiku huu ( Leo hii )

Kocha Mkuu Mbrazili Roberto Oliveira hatakiwi tena Kikosini Simba SC hivyo anatengenezewa Mazingira ya Kuchomeshwa ( Kuhujumiwa ) kisha Mashabiki tuchukie na Presha ipande kwa Viongozi na haraka sana Waachane nae aje Kocha Mzawa ambaye Wachezaji wanampenda kwakuwa huwa anawaruhusu Kunywa Bia, kuvuta Bangi na Kutoroka Kambini Usiku kwenda Juliana, Didiz na Beach Kidimbwi na ni Mshikaji wao mno.

Mchana niliahidi kuja na Exclusive Mbili kuhusu yanayojiri Simba SC na hii ni ya Pili na ya mwisho na ichukueni kwa 100% nikimaanisha ni ya uhakika kwani Mfalme wa Taarifa GENTAMYCINE sijawahi Kubahatisha na kamwe sitokuja Kubahatisha.

Haya Wazee wa Kukopi Taarifa zangu hizi GENTAMYCINE The King akina Ricardo Momo, Edo Kumwembe na Watangazaji hadi Wachambuzi wa Habari za Michezo mkiitumia / mkiichukua hapa tafadhali msisahau kutoa Credits kwa niliyeileta mkaijua na kwa Mtandao huu pendwa na tukuka wa JamiiForums sawa?

Nimemaliza.
 
mm89.jpg
 
Timu mbovu tu ile mmesajiri kwa kelele nyingi Wachezaji wenyewe ndio wale wavaa hereni harafu mtoboe CL huko kocha ni mzuri tatizo hamna Scout nzuri ya kutafuta aina ya Wachezaji wanaotakiwa kuwepo Simba mmeferi mpaka mkaamua kumrudisha Mikson ambae uwezo wake ulipungua mpaka Waarabu wakamtoa kwa Mkopo na huko alikotolewa kwa mkopo akawa anakaa Benchi...Simba mshawahi letewa mchezaji Mganda kwenye Uchaguzi wenu sijui hata mnakumbuka hilo...pana viongozi ndio wanawatafuta Wachezaji kwa % ndio maana matumizi makubwa ila hakuna Timu sasa hivi mnazungumzia sijui muunganiko wachezaji bora wanahitaji muunganiko gani? sema mna kelele sana wacha mpotee tu kwanza tutulie
 
Ukizungumzia kulijua soka la ndani kiundani zaidi Basi Genta huna mpinzani


Ukitaka soka la ulaya ,Basi Mimi mchambuzi nguli Sina mpinzani


Ni chuki tu za watu wanashindwa kutupa heshima
 
Ukizungumzia kulijua soka la ndani kiundani zaidi Basi Genta huna mpinzani


Ukitaka soka la ulaya ,Basi Mimi mchambuzi nguli Sina mpinzani


Ni chuki tu za watu wanashindwa kutupa heshima
japo Mimi ni mwana arsenal, ila huo uchambuzi wako ume tuingiza Chaka Sana.

au ndugu zangu Flano, makaveli10 mna semaje??, arsenal bingwa si ali tabiri hamiss😂
 
Back
Top Bottom