kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Tanzania ushabiki wa mpira uko juu sana kuliko nchi nyingine zinazotuzunguuka kutokana na aina yetu ya kutaniana kwa kucharurana bila kupigana kati ya Simba na Yanga.
Timu hizi ziko hivyo tangu kuanzishwa kwake na kuingia katika sura mpya wakati wa Jerry Muro na Manara. Leo hii Tanzania inavutia wadau wengi ndani na nje ya Tanzania, kutokana na aina yetu unique ya kushabikia.
Kama Ali Kamwe hataki mpira huu wa kusemana kati ya Simba na Yanga, atafute timu ambayo iko baridi kidogo kama Azam, Ihefu, au Singida big stars, maana hatakubalika kabisa hapo Yanga.
Yeye ni nani hadi abadilishe utamaduni huu unaovutia wawekezaji wengi na mashabiki wengi viwanjani kwenye club hizi?
Ninamtahadharisha kijana wangu ili asije akasema hatujamwambia.