Ali Kamwe bila kuicharura Simba ondoka Yanga nenda Azam

Ali Kamwe bila kuicharura Simba ondoka Yanga nenda Azam

NDYO TUPO BUSY ILA WANA SIMBA TUSISAHAU KUMPIGIA KURA BOULAYE DIA[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji2089][emoji2089][emoji2089][emoji2089][emoji2089]
Mmeo ana hali ngumu sana jitahidi kuhamasisha
1664835189727.jpg
 
Yanga bwana sakho aliposhinda kiatu mkasema goal la mchongo kumbe mlikuwa mnaumia kimya kimya sasa hii ya mayele inaonyesha ni jinsi gani mna uchu mabingwa wa kihistoria.
Kwahio na nyie mnaumia sasa hivi?
 
Kwani huwezi promote timu yako bila kuwasema wengine? Hayo mambo ya kizamani ndio yanasabaisha watu wanatukanana bila sababu ya msingi kila mtu apambanie timu yake tuta taniana siku tukiwa na mechi inayo tukutanisha huwezi kua msemaji wa Yanga kila siku unaiongelea Simba huo ujinga wa wa Manara hatutaki
Kabla ya kuacha kuisema Simba au Yanga ukiwa kiongozi wa Simba au Yanga lazima kwanza utafute majibu ya maswali yafuatayo:
1. Utani wa Simba na Yanga ulianzaje?
2. Kwanini Simba na Yanga zina wanachama na mashabiki wengi kuliko timu nyingine Tanzania?
3. Kwanini Simba na Yanga zina mashabiki wengi wanaoingia viwanjani na kununua jezi?
4. Je, utani wa Simba na Yanga unasababisha Simba na Yanga kutokuchukua vikombe vya CAF?
5. Je, ni watu wangapi wameuana au kupigana kwasababu ya utani wa simba na Yanga?
6. Je, mashabiki wa simba na Yanga hawazikani wala kutakiana heri wakati wa matatizo mitaani?

Mara nyingi huwa tunasema do not strengthen the weakest by weakening the strongest.
 
Kama Ali Kamwe hataki mpira huu wa kusemana kati ya Simba na Yanga, atafute timu ambayo iko baridi kidogo kama Azam, Ihefu, au Singida big stars, maana hatakubalika kabisa hapo Yanga.
Acha kumtisha bhana, yeye pia ana namna yake ya usemaji hawezi kuwa kama Jerry au Haji.
 
Acha kumtisha bhana, yeye pia ana namna yake ya usemaji hawezi kuwa kama Jerry au Haji.
Hatusemi awe Jerry au Manara mwingine, lakini utani (humor) wa simba na yanga hana ubavu wa kuuzika. Nimemshangaa eti anaomba radhi kwa kuisemea vizuri Yanga na kuisemea vibaya Simba. Utani wenu ni sehemu ya utamaduni wetu. Utani huu umefika ngazi zote za jamii kuazia mitaani, bungeni, mahakamani hadi Ikulu. Unatuunganisha, unatutambulisha na unatusahaulisha shida zetu kwa muda. Shida iko kwa wale ambao wanauchukulia utani huu kama uhasama kamili. Watu wasiotaniana ni rahisi sana kuuana kama vile Somalia, Ethiopia, Rwanda na kwingineko
 
Back
Top Bottom