Ali Kamwe: Sababu 8 zilizoifanya GSM kuvunja mkataba na TFF

Ali Kamwe: Sababu 8 zilizoifanya GSM kuvunja mkataba na TFF

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Andiko la Ali Kamwe

1. Mechi zote za nyumbani zinazoihusisha Simba zimekuwa zikichezwa bila ya nembo ya GSM kwenye mbao za matangazo hii ni kunyume na kifungu namba 4.1 na 4.8 cha makubaliano ya udhamini

2. GSM kwa makusudi imenyimwa haki ya kuonekana kwenye bango la mandhari la wadhamini kwa mikutano yote inayohusisha Simba hii ni kinyume na kifungu namba 4.8 cha makubaliano ya mkataba

3. GSM kwa makusudi imenyimwa haki ya kuonekana kwenye mabango ya mikutano ya kabla na baada ya mechi mwenye mechi zinazoihusisha Simba

4. GSM kwa makusudi imenyimwa haki ya kuonekana kwenye bega la kushoto la jezi za Simba

5. TFF wameshindwa kujibu juu ya malalamiko yetu na kushindwa kurekebisha ukiukwaji wa makubaliano kama tulivyowasilisha taarifa ya ukiukwaji tarehe 14 Desemba 2021

6. TFF imeshindwa kutimiza kanuni zake juu wadhamini

7. Nembo za GSM na Chapa yake zimekuwa haziheshimiwi na maafisa wa TFF mara kwa mara

8. TFF imeshindwa kuweka usawa kwenye mechi za ligi kuu
 
Simba na yanga kucheza na wadhamini wa ligi kuu Wala sio bahati mbaya au sijui kulinda clubs hapana lengo ni kujenga mazingira ya kudhoofisha nguvu ya kipesa kwa timu ndogo ili waweze kuzihonga kirahisi.

Msimu huu timu zilianza kuimarika kwa kutegemea mapato yake nadhani wote tunaona namna timu hizi zinavyookolewa na marefa
Tff ni dhaifu mno na imejaa watu waoga dhidi ya hizi clubs na madudu yataendelea
 
Giesiem ndiye alikuwa anaziimarisha hizi timu ndogo?
Simba na yanga kucheza na wadhamini wa ligi kuu Wala sio bahati mbaya au sijui kulinda clubs hapana lengo ni kujenga mazingira ya kudhoofisha nguvu ya kipesa kwa timu ndogo ili waweze kuzihonga kirahisi
Msimu huu timu zilianza kuimarika kwa kutegemea mapato yake nadhani wote tunaona namna timu hizi zinavyookolewa na marefa
Tff ni dhaifu mno na imejaa watu waoga dhidi ya hizi clubs na madudu yataendelea
 
Ajabu hii
Timu inayodai ina mashabiki wengi Tanzania, Imeingiza faida kuliko timu yoyote msimu uliopita, Ina pesa kuliko timu yoyote inayoshiriki ligi kuu.

Kulazimisha timu ndogo kama SIMBA ivae na kutangaza bidhaa zenu ni ujuha wa hali ya juu kwa nchi yetu kwani kwa YANGA mnapata hasara.
 
Utakuwa na akili fupi, yaan unawezaje kulipa wakati mkataba haujakamilika?.
Uliwezaje kuruhusu mabango ya kampuni yako yawekwe kwenye viwanja wakati ukijua mkataba haujakamilika?

Uliwaruhusu vipi timu 15 zivae logo yako huku ukijua mkataba bado ni incomplete?

Hizo timu zikikuambia kua kwa kipindi ambacho wamevaa hizo jersey zenye nembo yako ziliweza kukusaidia wewe ku brand biashara yako na kuinufaisha kampuni kiujumla utazipinga kwa fact zipi?

Kwanini kipindi cha miezi mitatu wakati hizo timu zinavaa nembo yako hukuzijulisha mapema kwamba kutakuwa na ucheleweshaji wa malipo yao kutokana na mkataba kutokamilika ili wajiandae kabisa wavae wakiwa tayari wanajua hilo?
 
Jamani mbona Huyo Jiesemu Wanamchelewesha....! Akamatwe Mara moja Dhulumati Mkubwa Mhujumu Uchumi!! Timu Zoote hizo 15 azifanyie Uhuni ..! Ashitakiwe Akiwa ndani....Gaidi naye!
 
Logo halisi ya NBC ina Twiga mwenye rangi nyekundu, hiyo anayovaa Yanga ni logo feki. Kama unabisha ubishe tu kishabiki.
WAKATI mwingine tumia kichwa kuwaza sio ushabiki!! Taasisi yoyote inakuwa na miiko na taratibu zake ktk kuendesha mambo, yanga ni taasisi na Moja ya miiko yake nikutokumia rangi nyekundu.

NBC ni taasisi km ni taasisi ina rangi zaidi ya Moja ambazo hutumia Pale wanapofanya biashara na mtu au taasisi nyingine, lengo nikutokuathiriana kibiashara kwa pamoja. Ndio maana hata kwenye hili suala yanga akawa na option yakuchagua rangi na kisheria ni haki yao kimsingi.

Ujinga wetu wtz tunaendekeza ushabiki and not facts.
 
Uliwezaje kuruhusu mabango ya kampuni yako yawekwe kwenye viwanja wakati ukijua mkataba haujakamilika?

Uliwaruhusu vipi timu 15 zivae logo yako huku ukijua mkataba bado ni incomplete?

Hizo timu zikikuambia kua kwa kipindi ambacho wamevaa hizo jersey zenye nembo yako ziliweza kukusaidia wewe ku brand biashara yako na kuinufaisha kampuni kiujumla utazipinga kwa fact zipi?

Kwanini kipindi cha miezi mitatu wakati hizo timu zinavaa nembo yako hukuzijulisha mapema kwamba kutakuwa na ucheleweshaji wa malipo yao kutokana na mkataba kutokamilika ili wajiandae kabisa wavae wakiwa tayari wanajua hilo?
Una shida ya uelewea or una chuki binafs, haya unayoyasema kawaulize TFF ndio wenye mandate yakuamua haya, GSM alikuwa mdhamini na alikuja na condition zake ambazo TFF walikubali kuzitekeleza. Kwahiyo km TFF ameshindwa kutumia terms za mkataba unawezaje kumdai GSM??, Aliyefeli ni TFF timu zinapaswa kuihoji TFF and not GSM.
 
Kwa haya yanayoendelea siku Govt ikiingilia soka sitashangaa
 
Una shida ya uelewea or una chuki binafs, haya unayoyasema kawaulize TFF ndio wenye mandate yakuamua haya, GSM alikuwa mdhamini na alikuja na condition zake ambazo TFF walikubali kuzitekeleza. Kwahiyo km TFF ameshindwa kutumia terms za mkataba unawezaje kumdai GSM??, Aliyefeli ni TFF timu zinapaswa kuihoji TFF and not GSM.
Twende taratibu tubishane kwa facts

Naelewa kwamba TFF ni jipu ila pia naelewa kua GSM alijua kuna mambo hayapo sawa kwenye mkataba ambayo yanapingana na sheria husika

Pamoja na hayo lakini bado GSM hakutaka kufata protocols kwasababu alijua kuna angle ambayo inamnufaisha

Kwa hiyo kama unasema ubovu wa TFF basi usisahau kuzungumzia ukurupukaji wa GSM au tuuite ukengeukaji kwasababu hakuna mtu anayeweza kuamini GSM hakujua kua kuna sheria zinakiukwa
 
Timu zote zinazoshiriki ligi kuu zinaweka nembo ya gsm kasoro Simba tu.
gsm kavunja mkataba kwasababu tu ya Simba kutovaa nembo ya gsm.

Simba ni timu kubwa yenye hadhi ya kuvaa nembo ya gsm.klabu ya Simba ifungue milango kwa gsm wafanye biashara wasikaze msuli kisa gsm anadhamini Yanga.mpira pesa mpira biashara.
 
Hivi unawezaje kumlaum mtu ambaye kaja na pesa kuwekeza na kapewa taratibu Zote zinazohitajika na akazifuata!!.

Km unajua TFF n tatizo hizo lawama kwa GSM n za nini au chuki?, Tuache ujuha kwa mambo yaliyo wazi.
 
Timu zote zinazoshiriki ligi kuu zinaweka nembo ya gsm kasoro Simba tu.
gsm kavunja mkataba kwasababu tu ya Simba kutovaa nembo ya gsm.

Simba ni timu kubwa yenye hadhi ya kuvaa nembo ya gsm.klabu ya Simba ifungue milango kwa gsm wafanye biashara wasikaze msuli kisa gsm anadhamini Yanga.mpira pesa mpira biashara.
Mpira pesa kwa mgao wa 3m kwa mwezi as a team?
 
Back
Top Bottom